Tafuta

Vatican News
ROMANIA POPE FRANCIS VISIT PREPARATIONS ROMANIA POPE FRANCIS VISIT PREPARATIONS  (ANSA)

Papa Francisko: Hija ya Kitume Romania: Takwimu za Kanisa

Takwimu za Kanisa Katoliki nchini Romania hadi kufikia tarehe 31 Desemba 2017 zinaonesha kwamba, Kanisa lina jumla ya Maaskofu 18 na Mapadre 2, 057 wanaohudumia Majimbo 13 yanayoundwa na Parokia 2, 031. Kuna jumla ya waseminari wadogo 2, 256 na waseminari walioko seminari kuu ni 599 kwa nchi nzima. Kanisa liko mstari wa mbele katika huduma za elimu, afya, wazee & watoto.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake kwenye mitandao ya kijamii anasema, tarehe 31 Mei 2019, Siku kuu ya Bikira Maria kumtembelea Elizabeth, anaanza hija yake ya kitume nchini Romania, ili kutembea kwa pamoja na ndugu zake wa Kanisa la Kiorthodox pamoja na waamini wa Kanisa Katoliki, kwa kufuata nyayo za mashahidi wa imani! Baba Mtakatifu anawaalika waamini pamoja na watu wote wenye mapenzi mema kumsindikiza katika hija hii ya kitume kwa sala na sadaka zao! Baba Mtakatifu anatarajiwa kuwasili majira ya mchana na kupatiwa mapokezi ya kitaifa, Ikulu. Atamtembelea Rais Klaus Werner Iohannis pamoja na kufanya mazungumzo ya faragha na Waziri mkuu Vasilica Viorica Dancila na baadaye atakuwa na mkutano na viongozi wa serikali, vyama vya kiraia pamoja na wanadiplomasia.

Alasiri, Baba Mtakatifu anatarajiwa kufanya mazungumzo na Patriaki Daniel wa Kanisa la Kiorthodox nchini Romania na hatimaye, kukutana na kuzungumza na wajumbe wa Sinodi ya Kudumu ya Kanisa la Kiorthodox la Romania. Baba Mtakatifu anatarajiwa kutembelea Kanisa kuu la Kiorthodox na kutoa tafakari yake. Majira ya jioni ataadhimisha Ibada ya Misa Takatifu kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu Yosefu, Siku kuu ya Bikira Maria Kumtembelea Elizabeth. Na kwa Ibada hii ya Misa, Baba Mtakatifu atakuwa anahitimisha siku ya kwanza ya hija yake ya kitume, nchini Romania!

Takwimu za Kanisa Katoliki nchini Romani hadi kufikia tarehe 31 Desemba 2017 zinaonesha kwamba, Kanisa lina jumla ya Maaskofu 18 na Mapadre 2, 057 wanaohudumia Majimbo 13 yanayoundwa na Parokia 2, 031. Kuna jumla ya waseminari wadogo 2, 256 na waseminari walioko seminari kuu ni 599 kwa nchi nzima. Kanisa Katoliki nchini Romania liko pia mstari wa mbele katika huduma za elimu, afya, wazee pamoja na kuendesha vituo vya watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu na hatarishi!

Papa: Takwimu
30 May 2019, 16:01