Tafuta

Vatican News
Papa Francisko ametuma salam za pongezi kwa Mfalme Naruhito wa Japan. Papa Francisko ametuma salam za pongezi kwa Mfalme Naruhito wa Japan. 

Papa Francisko: Salam za pongezi kwa Mfalme Naruhito wa Japan

Papa Francisko anapenda kumhakikishia sala zake, ili Mwenyezi Mungu aweze kumkirimia: hekima na nguvu ya kulitumikia taifa lake. Mwishoni, mwa salam zake, amempatia Mfalme Naruhito na familia yake, baraka zake za kitume, zikiwa zimesheheni wingi wa amani na ustawi kwa ajili ya Japan. Baba Mtakatifu Francisko tangu ujana wake kama Mtawa, ametamani sana kwenda Japan.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemtumia salam na matashi mema Mfalme Naruhito wa Japan ambaye Mei Mosi, 2019 amesimikwa kuwa Mfalme wa 126 wa Japan, baada ya Baba yake Akihito kung’atuka kutoka kwenye kiti cha kifalme. Anapenda kumhakikishia sala zake, ili Mwenyezi Mungu aweze kumkirimia: hekima na nguvu ya kulitumikia taifa lake. Mwishoni, mwa salam zake, amempatia Mfalme Naruhito na familia yake, baraka zake za kitume, zikiwa zimesheheni wingi wa amani na ustawi kwa ajili ya Japan. Baba Mtakatifu Francisko tangu ujana wake kama Mtawa, ametamani sana kwenda Japan na anatarajia kwamba, panapo majaliwa, pengine, iko siku ataweza kutembelea Japan.

Mfalme Naruhito amekula kiapo cha kuhakikisha kwamba, anatekeleza dhamana na wajibu wake wa kulinda na kudumisha umoja wa Taifa; ataendelea kujikita zaidi katika kukuza na kudumisha ustawi, maendeleo na mafao ya wananchi wa Japan katika ujumla wao, bila kusahau amani duniani ambayo ni chachu ya maendeleo fungamani ya binadamu. Tukio hili limehudhuriwa na viongozi wakuu wa Serikali ya Japan, kama kielelezo cha amani, matumaini na maendeleo ya Japan. Kadiri ya Katiba ya nchi ya Japan, Mfalme ni alama umoja wa Kitaifa!

Papa: Japan
03 May 2019, 15:03