Tafuta

Papa amepokea hati za utambulisho kutoka kwa mabalozi wapya kutoka Msumbiji, Ethiopia,Thailand, Norway, New Zealand, Sierra Leone, Guinea Bissau na Lussemburg Papa amepokea hati za utambulisho kutoka kwa mabalozi wapya kutoka Msumbiji, Ethiopia,Thailand, Norway, New Zealand, Sierra Leone, Guinea Bissau na Lussemburg  

Papa anahimiza mabalozi wapya ili wawe wahamasishaji wa udugu!

Tarehe 23 Mei 2019,Baba Mtakatifu amepokea hati za utambulisho wa mabalozi wapya wanaowakilisha nchi zao Vatican kutoka Thailand,Norway,New Zealand,Sierra Leone,Guinea,Guinea Bissau,Lussemburg,Msumbiji na Ethiopia.Katika hotuba anawahimiza wawe wahamasishaji wa udugu.Katika kukubaliana kati ya binadamu kunapunguza matatizo ya kiuchumi,kijamii,kisiasa na mazingira mbayo ni tatizo kila kona

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Baba Mtakatifu Francisko, Alhamisi, tarehe 23 Mei 2019 amepokea hati za utambulisho kutoka kwa mabalozi wapya kuwakilisha nchi zao kutoka, Thailand, Norway, New Zealand, Sierra Leone, Guinea, Guinea Bissau, Lussemburg, Msumbiji na Ethiopia. Na akianza hotuba yake amewakaribisha katika fursa hiyo ya kuwakilisha hati za utambulisho kama mabalozi maalum wa Vatican wakiwakilisha nchi zao. Anawaomba wawafikishie salam zake kwa viongozi wakuu wa nchi zao akiwahakikishia sala zake kwa ajili yao na watu wote wanaowahudumia. Baba Mtakatifu amesema, kwa kutumia fursa hiyo katika mwanzo wa utume wao na kutambua michango yao tofauti ambazo nchi zao wanajikita kwa ajili ya wema wa dunia, ametaka kuzungumzia juu ya uwajibikaji ambao kama Vatican wanazingatia hawa kwa ulinzi wa waathirika zaidi kati ya ndugu kaka na dada. Ni dharura, amesisitiza Baba Mtakatifu, ya kuwa makini zaidi kwa masikini wazalendo wote na ambao ni wajibu wa dhati unao fafanuliwa kwa kuzingatia utofauti halali na ambao ni katika kuungana na kuhamasisha maendeleo yao fungamani ya kibinadamu. Baba Mtakatifu amesema Muungano huu una jina halisi:udugu!

Amani inawezekana na udugu una nguvu zaidi ya migawanyiko

Baba Mtakatifu akiendelea na hotuba yake hasa kwa neno la udugu, amesema kutokana na kwamba tunapaswa kukabiliana na changamoto za dunia na ngumu, ni haki kusisitizia umuhimu wa udugu, ili kuweza kufanya kazi pamoja ya kuhakikisha usawa na amani ya kuishi, ambayo si tu kama mkakati wa siasa kijamii, bali kuwa mfano wa mshikamano ule ambao unachimba mzizi kwa kina na shauku za pamoja ili kufikia lengo shirikishi. Na zaidi udugu huo Baba Mtakatifu anasema unaweza kutambulika katika ulimwengu wenye shauku ya urafiki kati ya watu, jumuiya na taifa, japokuwa hauwezi kupatika mara moja. Hata hivyo, amebainisha kuwa somo la maumivu kuhusu mgawanyiko na chuki pia yatufundisha kuwa hata amani daima inawezekana. Ufumbuzi wa migogoro na upatanisho ni ishara chanya ya umoja ambayo ina nguvu zaidi kuliko mgawanyiko na udugu ambao ni wa nguvu zaidi kuliko chuki.

Shukrani za jitihada za jumuiya ya kimataifa katika mapambano ya migogoro ya kisilaha

Ni jambo la kutiwa moyo kusisitiza juu ya jitihada zinazo endelea katika jumuiya ya kimataifa ili kushinda hali za migogoro ya silaha na kuunda michakato ya amani, na kutazama jinsi mazungumzo ya kidugu yanayo hitajika ili kuweza kufikia mtazamo huo wenye thamani. Kwa hakika mazungumzo, uelewa na kuenea kwa utamaduni wa uvumilivu, kumkubali mwingine na kuishi kati ya binadamu wote, unaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa katika kupunguza matatizo ya kiuchumi, kijamii, kisiasa na mazingira mbayo ni tatizo kila sehemu kubwa ya maisha ya binadamu (Hati ya udugu wa kibindamu, Abu dhabu, 4 Februari 2019)Baba Mtakatifu Francisko amehitimisha kwa kusema: “ wakati mnajindaa kufunga vibwewe kwa ajili ya uwajibikaji wa huduma mpya kwa ajili ya mataifa yenu, ninawahakikishia ushirikiano na msaada kutoka katika ofisi mbalimbazi za Vatican”. Aidha amesema: “Muwe na uhakika ya kwamba ninawasindikiza kwa sala na ninawatakia utume mwema ambao ni muhimu. Amewatakia baraka tele ya Mungu na familia zao.

 

 

23 May 2019, 14:53