Tafuta

Vatican News
Tarehe 18 Mei 2019 ametangazwa Mwenyeheri mpya  Maria Guadalupe Ortiz huko Madrid Hispania Tarehe 18 Mei 2019 ametangazwa Mwenyeheri mpya Maria Guadalupe Ortiz huko Madrid Hispania  

Papa amemkubuka Mwenyeheri Maria Guadalupe Ortiz de Landàzuri

Mara baada ya sala ya Malkia wa Mbingu Jumapili tarehe 19 Mei 2019 Baba Mtakatifu amemkumbuka Mwenyeheri mpya Maria Guadalupe Ortiz de Landàzuri aliyetangazwa tarehe 18 Mei 2019,katika Misa Takatifu iliyoadhimishwa Jimbo kuu la Madrid,nchini Hispania na Kardinali Angelo Becciu,Rais wa Baraza la Kipapa la kuwatangaza Wenyeheri na Watakatifu.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya sala ya Malkia wa mbingu,amekumbusha waamini na mahujaji wote waliokusanyika katika uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican tarehe 19 Mei 2019 ya kwamba  Jumamosi huko Madri ametangazwa Maria Guadalupe Ortiz de Landázuri, kuwa mwenyeheri ambaye alikuwa ni mlei mwaminifu  wa Shirika la Opus Dei. Aliweza kutoa huduma kwa furaha kwa  ndugu huku  akiunganisha na mafundisho na kutangaza Injili. Ushuhuda wake ni mfano kwa wanawake wakristo wanaojikita katika jamii na katika utafiti wa kisayansi. Baba Mtakatifu amewaomba watu wote wampigie makofi mwenyeheri mpya Guadalupe!

Mwenyeheri Maria Guadalupe Ortiz de Landàzuri alikuwa ni maarufu katika tafiti za sayansi ya kemia na ambaye aliweza kuunganisha taaluma yake na Neno la Mungu katika shughuli yake ya kisayansi. Na zaidi aliweza kujenga  upendo kwa Mungu na jirani!

https://www.vaticannews.va/sw/vatican-city/news/2019-05/mwenyeheri-maria-guadalupe-ortiz-kardinali-angelo-becciu.html

Salam kwa mahujaji wote

Baba Mtakatifu mara baada ya kumkumbuka mwenyeheri mpya pia ametoa salam mbalimbali kwa mahujaji kutoka duniani akianza na Italia, Mexico, California, Haiti; waamini kutoka Cordoba,Hispania, waamini wa Viseu Ureno na wanafunzi kutoka Pamplona na  Lisbona. Aidha amewakumbuka washiriki wa kozi ya wahusika wa jumuiya ya Mtakatifu Egidio kutoka pande zote za dunia na wengine wengi na kwa wote wametakia matashi mema na baraka ya Jumapili. Wasisahau kusali kwa ajili yake!

19 May 2019, 14:15