Tafuta

Vatican News
YOUCAT for kids ni kitabu cha Katekisimu ya Kanisa Katoliki kwa ajili ya watoto, wazazi, walimu na makatekisiti YOUCAT for kids ni kitabu cha Katekisimu ya Kanisa Katoliki kwa ajili ya watoto, wazazi, walimu na makatekisiti 

Utangulizi wa Papa katika kitabu cha Katekesimu ya watoto na wazazi:Injili daima iwe katika familia zetu!

Tangu tarehe 24 Mei 2019,katika maduka ya vitabu ya Mtakatifu Paulo,kipo Kitabu kiitwacho "YOUCAT for Kids.Katekisimu Katoliki kwa ajili ya watoto na wazazi".Kitabu hiki kinajikita kutoa maelekezo na ufafanuzi wa kina kwa wazazi,walimu na makatekisti wote.Utangulizi wa kitabu hiki chenye kurasa 240 umetolewa na Baba Mtakatifu Fracisko.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Tangu tarehe 24 Mei 2019, katika maduka ya vitabu Mtakatifu Paulo kuna Kitabu kiitwacho "YOCAT for Kids", ambcho ni Katekisimu ya Kanisa Katoliki kwa ajili ya watoto na wazazi. Ni mchakato wa safari ya kuelekea katika Kumunio ya kwanza na Kipaimara. Ni kitabu  ambacho kimetolewa utangulizi wake na Baba Mtakatifu Francisko. Ni kitabu chenye kurasa 240 kilichoandaliwa na Baraza la maaskofu wa Australia na kuthibitishwa na Baraza la Kipapa la kuhamasisha Uinjilishaji mpya ambapo umekabidhiwa zoezi kubwa la Katekesi. Katika maneno ya utangulizi wa Baba Mtakatifu Francisko kwenye kitabu cha “YOCAT  for Kids amesema, “ni katekisimu tofauti sana na ile ambayo niliitumia mimi. Kinastahili kwa watoto na wazazi wao ili watoto waweze kutumia muda wao wakisoma pamoja na wazazi wao na kugundua upendo zaidi wa Mungu”.

Kukuza mazungumzo juu ya imani

Baba Mtakatifu Francisko anasema kwa njia hiyo ni Katekisimu mpya ambayo inaelezea mambo msingi wa imani kwa njia ya michoro mizuri sana na lugha inayosahili na kuhamasisha walenga hasa watoto kuanzia maiaka 8-12 ambao wanajiandaa kupokea Komuio ya kwanza na Kipaimara. Mtindo wake wa maswali na majibu kwa mara nyingine unawakilisha mantiki, na masomo ambayo yanarahisisha uelekwa na baadaye sehemu ya chini ya sura katika eneo la mchoro, yapo maelezo ya watoto, makatekesita na walimu ambao wanamotisha mawazo ya kukuza mazungumzo na watoto.

Wazazi, wawakili na shuhuda wasiochoka

Katika utangulizi wa Kitabu hicho Baba Mtakatifu Francisko anasisitiza zaidi juu ya mazungumzo na kusema: “kwa kufungua kursa za  YOUCAT for Kids aanathibitisha: ninajikuta katika milioni ya maswali ya watoto wanayo uliza wazazi na makatekista wao. Ninaamini kitabu hiki ni muhimu kama ilivyo Katekisimu ya  watu wazima, ambapo tunapata majibu ya maswali muhimu zaidi ya maisha: “ulimwengu unatoka wapi? Kwa nini nipo, na kwa kwa lengo lipi tunapaswa kuishi hapa duniani? Ni kitu gani kinatokea baada ya kifo?

Ukurasa baada ya ukurasa ni utajiri mkubwa

Kwa hiyo, anaendelea kuandika kuwa “ni matumaini kwamba kutokana na kusoma misingi ya imani yetu inawezekana kuanzishwa kubadilishana mawazo  yanayoendelea na yenye utajiri kati ya wakubwa na wadogo hivyo anarudia kuwaalika wazazi wao  kujikita muda wao kwa  makusudi mazima kwamba: “Ukurasa baada ya ukurasa, siri ya imani baada ya siri ya imani, swali baada ya swali. Saidieni watoto wenu kugundua upendo wa Yesu!  Hii itawafanya kuwa na nguvu na jasiri”. Kadhalika Baba Mtakatifu amesema:“Ninawakabidhi YOUCAT for kids. Kamwe msichoke kuuliza na kuwasimulia imani yenu. Msibaki  bubu wakati ,mnaulizwa maswali na watoto wenu lakini daima muwe na nguvu ya kuwa wawakili wa imani mliyopokea kutoka kwa wazazi wenu. Kuweni minyororo ya kibinadamu ambayo kutoka kizazi hadi kizazi inahakikisha kwamba Injili daima ipo ndani ya familia zetu, jumuiya zetu na katika Kanisa”.

24 May 2019, 09:46