Tafuta

Baba Mtakatifu amekutana na  jamii ya Warom na Wasinti mjini Vatican wakiwa katika fursa ya Mkutano wao ulioandaliwa huko Divin Amore, Roma Baba Mtakatifu amekutana na jamii ya Warom na Wasinti mjini Vatican wakiwa katika fursa ya Mkutano wao ulioandaliwa huko Divin Amore, Roma  

Papa na jamii ya Warom na Wasinti:Anawahimiza kwenda mbele kwa hadhi bila chuki

Asubuhi tarehe 9 Mei 2019,karibia watu wa jamii ya warom na wasinti 500 wakiwa pamoja na wahudumu wa kichungaji wamesali pamoja na Baba Mtakatifu Francisko mjini Vatican.Hawa ni jamii ya kuhama hama na kati yao wanawake watatu wametoa ushuhuda ambapo Baba Mkatifu ameelekeza njia ya undugu kama dawa ya kushinda hofu ya jirani.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Kukutana na mwingine kwa ajili ya kushinda hofu na kuvunja kuta, ndiyo lengo la Mkutano wa Chama cha Migrantes walio pendekeza kukutana tarehe 9 Mei 2019 kuanzia saa 9.30 -12.00 jioni katika ukumbi wa Madhabahu ya Mama Maria huko Divino Amore Roma. Huu ni mkutano na jamii ya watu wa kuhamahama wajulikanao Warom na Wasinti wanaoishi nchini Italia,ili kushirikishana nao kipindi cha utajiri mkubwa wa utamaduni sikukuu, sanaa na muziki. Baba Mtakatifu Francisko alipokutana  mwaka 2017 na jumuiya ya wahamiaji huko Bologna nchini Italia  alisema kwamba, wengi hawawatambui, hiyo inawafanya kuhisi hukumu, vizuizi na  ubaridi dhidi yao, kwa kuamini wanafanya vizuri, lakini siyo hivyo. Inabidi kuwatazama  kama ndugu, kuwakaribia kuwana upendo na huruma.

Maombi na jumuiya wa Warom na Wasinti mjini Vatican

Asubuhi tarehe 9 Mei 2019, karibia warom na wasinti  500 wakiwa pamoja na wahudumu wa kichungaji wamesali pamoja na Baba Mtakatifu Francisko mjini Vatican. Hawa wamesindikizwa na Kardinali  Gualtiero Bassetti, rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Italia, na wengine walikuwapo ni Kardinali Peter Kodwo Appiah Turkson, Rais wa Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo fungamani ya watu,  Kardinali Angelo De Donatis, makamu Askofu Mkuu wa Roma, Rais wa Tume ya Baraza la Maaskofu Italia kwa ajili ya wahamiaji na Chama cha Migrantes Askofu Mkuu Guerino Di Tora, wa jimbo kuu la  Siena-Val d’Elsa-Montalcino na Katibu Mkuu wa Tume ya Baraza la Maaskofu  Italia kwa ajili ya wahamiaji, askofu Paolo Lojudice, wa jimbo katoliki la  Avezzano na Askofu Pietro Santoro. Katika hotuba ya Baba Mtakatifu Francisko anasema, imepita miaka 50 tangu Mtakatifu Paulo VI aliposema maneno yake huko Pomezia  nje ya Roma kwa Jumuiya ya Warom kuwa: “ninyi hampo pembezoni, bali chini ya mantiki fulani, ninyi mpo katikati, ninyi mko katika moyo”. Kwa maana hiyo: "Leo hii maneno hayo yanasikika tena katika ukumbi wa mkutano huu”.

Matatizo ya umbali wa  akili na moyo

Mara baada ya kusikiliza baadhi ya ushuhuda Baba Mtakatifu amesema  kuwa tatizo halisi, kabla ya kuwa ya kisiasa na kijamii, linatokana na umbali na hili i tatizo la sasa”. “Ikiwa unaniambia kuwa ni tatizo la kisiasa, shida ya kijamii, tatizo la kitamaduni, tatizo la lugha, lakini haya ni mambo ya daraja la pili” kwa sababu tatizo ni tatizo la umbali kati ya akili na moyo na dilo hilo tatizo la umbali”, Baba Mtakatifu amesisitiza.

Raia wa daraja la pili

Kipengele hiki, katika kafafanua watu fulani kutokana na  ubaguzi, Baba Mtakatifu ameeleza kuwa: “ni moja ya mambo ambayo huunda umbali kati ya akili na moyo, ki kukweli kuna wananchi wa daraja  la pili”.  Lakini wanachi wa kweli wa daraja la pili ni wale ambao wanabagua watu, kwa maana hao ndiyo wa daraja la pili kwani  hawajuhi kukumbatia”.

Kutembe kwenda mbele kwa hadhi

Akiendelea kuwatazama jamii hii ya waroma, Baba Mtakatifu  Francisko amekumbuka kuwa, daima wote tunayo hatari hasa ya udhaifu wa kuangukia katika kukuza chuku. Na hivyo amewaomba tafadhali wawe na moyo mkuu zaidi na wasiwe na chuki. Na badala yake waendelee kwenda mbele kwa hadhi. “Hadhi ya familia, hadhi ya kazi hadhi ya kupata mkate wa kila siku. Hiyo ndiyo inapaswa kupelekwa mbele yaani hadhi ya maombi”, amesisitiza.

Njia ya udugu na matumaini yasiyo katisha tamaa

Katika hotuba yake, Baba Mtakatifu Francisko anashutumu vikali njia za kubagua, zile zilizojengwa juu ya  hukumu na maneno. Kutokana na hilo ameelekeza njia ya udugu na ambayo anasema ndiyo ya kufuta kwa kuwa na matumaini ya kweli kwa Mungu wa kweli na ambaye kamwe hadanganyi. “ Ni matumaini ya dhati kwamba kama mwanamke anayejifungua mtoto mpya katika dunia, na kwamba katika kupanda matumaini, kuna uwezo wa  kutengeza   njia, kuunda upeo na kutoa tumaini!

Ushuhuda wa wanawake watatu:chuki,matendo ya nguvu yanayozidi kuongezeka

Wanawake watatu wenye asili ya Waroma waliwakilisha kikundi kikubwa cha wanawake wanaoishi katika maeneo ya pembezoni mwa Roma, ambao wamekumbusha isivykuwa rahisi kwa upande wa Italia ya leo kupata kazi yenye uhakika na hadhi na kuweza kujikumu kiuchumi. Pia wanawake hao wameelezea kuwa, kuna matatizo mengine, yanayoongeza, ambayo yanahusishwa na makazi yasiyofaa, kufukuzwa na kuhamishwa  kwa kulazimishwa kwa njia ya vyombo vya  mamlaka, wakati huo kutokuwepo na njia mbadala za kutosha kwa ajili yao. Hata hivyo  katika shida hizi wanasema: hazituzuii kuwa  matumaini na kwa maana hiyo tunangalia wakati ujao na tumaini. Sisi ni mama  amesisitiza na  hii inatupatia nguvu za  kwenda mbele ili kuboresha hali za maisha yetu watoto wetu.

Baba Mtakatifu Francisko amehitimisha akiwashukuru sana na kuwahikishia sala zake. Amesema kuwa anasoma katika magazeti mambo mabaya na kiukweli anateseka. Kwa mfano amesema: “leo hii nimesoma jambo baya na hivyo ninateseka kwa sababu hii siyo ustaarabu. Upendo ni ustaarabu, kutokana na hiyo lazima kwenda mbele kwa upendo. Amewabariki na kuwaomba wasali kwa ajili yake.

09 May 2019, 14:44