Tafuta

Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko amewasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Sofa nchini Bulgaria kuanza hija yake ya kitume nchini Bulgaria na Macedonia ya Kaskazini. Baba Mtakatifu Francisko amewasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Sofa nchini Bulgaria kuanza hija yake ya kitume nchini Bulgaria na Macedonia ya Kaskazini.  (Vatican Media)

Hija ya kitume: Bulgaria & Macedonia ya Kaskazini: Matashi mema!

Baba Mtakatifu Francisko kwa viongozi wote hawa amewatakia: amani, ustawi, maendeleo, neema na baraka; nguvu na furaha ya kweli! Baba Mtakatifu akiwa njiani kuelekea Bulgaria amepata nafasi ya kuzungumza na waandishi wa habari waliko kwenye msafara wake. Amewakumbusha kwamba, wahusika wakuu wa hija hii ni Mtakatifu Yohane XXIII pamoja na Mama Theresa wa Calcutta.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Hija ya kitume ya 29 ya Baba Mtakatifu Francisko nchini Bulgaria na Macedonia ya Kaskazini kuanzia tarehe 5-7 Mei 2019 inaongozwa na kauli mbiu "Pacem in terris" yaani "Amani duniani" pamoja na "Msiogope enyi kundi dogo". Hija hii inapania kukuza na kudumisha misingi ya haki, amani na maridhiano; kwa kujenga na kudumisha utamaduni wa watu kukutana pamoja na utamaduni wa udugu unaofumbatwa katika majadiliano ya kidini, kiekumene na kitamaduni.

Baba Mtakatifu, Jumamosi, tarehe 4 Mei 2019 alikwenda kwenye Kanisa kuu la Bikira Maria mkuu lililoko mjini Roma ili kujikabidhi chini ya ulinzi na tunza ya Bikira Maria “Salus popoli Romani” yaani “Bikira Maria Afya ya Warumi” wakati wote wa hija yake ya kitume!. Baba Mtakatifu akiwa njiani kuelekea Bulgaria, Jumapili, tarehe 5 Mei 2019 ametuma salam na matashi mema kwa Rais Sergio Mattarella wa Italia, Rais Kolinda Grabar-Kitarovic wa Jamhuri ya Watu wa Croatia na Zagreb, Rais Milorad Dodik wa Bosnia na Erzegovina.

Viongozi wengine waliotumiwa salam ni: Rais Milo Dukanovic wa Montenegro pamoja na Rais Aleksandar Vucic wa Serbia Belgrade. Baba Mtakatifu Francisko kwa viongozi wote hawa  amewatakia: amani, ustawi, maendeleo, neema na baraka; nguvu na furaha ya kweli. Baba Mtakatifu akiwa njiani kuelekea Bulgaria amepata nafasi ya kuzungumza na waandishi wa habari waliko kwenye msafara wake. Amewakumbusha kwamba, wahusika wakuu wa hija hii ya kitume ni Mtakatifu Yohane XXIII pamoja na Mama Theresa wa Calcutta. Hii ni hija ya siku tatu, lakini yenye umuhimu sana katika maisha na utume wa Kanisa. Baba Mtakatifu, baadaye amesalimiana na waandishi wa habari waliko kwenye msafara wake na kubadilisha nao mawili matatu! Baadhi ya waandishi wa habari wamempatia Baba Mtakatifu zawadi mbali mbali, ikiwemo Jezi Namba 3 Francesco iliyoandikwa “Team of Hope Bulgaria”.

Papa: Waandishi wa Habari

 

05 May 2019, 13:09