Tarehe 6 Mei 2019 Papa akiwa katika ziara ya kitume nchini  Bulgaria na Macedonia ya Kaskazini ametembelea kambi ya wakimbizi huko Vrazhdebna Tarehe 6 Mei 2019 Papa akiwa katika ziara ya kitume nchini Bulgaria na Macedonia ya Kaskazini ametembelea kambi ya wakimbizi huko Vrazhdebna 

Hija ya Kitume:Bulgaria:Dunia ya wahamiaji ni msalaba wa ubinadamu!

Baba Mtakatifu Francisko akiwa katika ziara yake nchini Bulgaria asubuhi tarehe 6 Mei ametembelea Kituo cha wakimbizi huko Vrazhdebna karibu na Sofia mahali ambapo amekutana na watu 50,hawa ni watoto na wazazi wao karibu wengi wanatoka nchini Siria na Iraq.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Baba Mtakatifu Francisko akiwa katika ziara yake nchini Bulgaria asubuhi tarehe 6 Mei 2019 ametembelea Kituo cha wakimbizi karibu na Sofia mahali ambapo amekutana na watu 50 karibu wengi wanatoka nchini Siria na Iraq. Wakati wa salama zake bila mandishi ameshukuru kwa ukarimu wao, pia kuwashukuru watoto kwa wimbo wao mzuri. Baba Mtakatifu Francisko anasema, watoto wanaleta furaha katika safari yao. Safari ambayo daima siyo nzuri na yenye kuwa na uchungu hasa wa kuacha nchi zao, huku wakitafuta namna ya kuingia katika nchi nyingine… Lakini daima kuna matumani... Leo hii dunia ya wahamiaji na wakambizi kidogo ni msalaba, amesema Baba Mtakatifu na kuongeza:msalaba wa ubinadamu, ni msalaba wa watu wengi wanaoteseka… Baba Mtakatifu Francisko aidha amewashukuru wao na utashi wao, wakati huo huo akiwatakia matashi mema hata kwa wazalendo waliowaacha katika nchi zao! Na kwa kuhitimisha amewapa Baraka, lakini pia  wakumbe kusali kwa ajili yake.

Taarifa kutoka kwa Dk Gisotti Msemaji wa vyombo vya habari Vatican

Hatua ya kwanza  katika siku ya Pili ya Baba Mtakatifu Francisko nchini Bulgaria ilikuwa ni kutembelea kituo cha mapokezi ya wakimbizi ambapo Baba Mtakatifu Francisko amepokelewa na Mkurugenzi wa Kituo hicho na Mkurugenzi wa Caritas mbele ya jengo na wakati huo huo  ndani ya ukumbi wa chakula kulikuwapo na watu 50, kati yao ni watoto na wazazi wao! Mkutano ulifanyika kwa namna ya familia na furaha, kwa mujibu wa Msemaji wa mpito wa Vyombo vya habari Vatican Dk, Alessandro Gisotti.

Baba Mtakatifu yupo karibu na mwili unaoteseka

Akiendelea kueezea juu ya mkitano huo Dk Gisotti amesema: Mkutano huo ulikuwa mfupi sana wa dakika karibia 25 tu na ambapo Baba Mtakatifu ameweze kuwasalimia watoto wakiwa ndiyo wako mstari wa mbele. Ukaribu wa mwili unaoteseka wa Kristo, pembezoni ndiyo mada msingi zinazo onekana tangu Baba Mtakatifu Francisko na utume wake, kwa namna ya pekee watoto na kwa kesi kama hii  walio wengi wanatoka Siria na Iraq waliopokelewa katika kituo hiki cha Caritas na ambao wameweza kukutana na Baba Mtakatifu kwa furaha kubwa. Watoto wameweza kumkabidhi Baba Mtakatifu zawadi ya michoro yao ambayo ameipenda sana. Watoto hawa ni kunzia miaka 6-10 umri wa kwenda shule na ambao kwa hakika michoro yao ilikuwa ni nzuri sana, anathibitisha Dk. Gisotti. Baba Mtakatifu Francisko amewaachia picha ya Mama Maria kwa maana msingi, kwani ni Mama anaye wasindikiza katika mateso yao, lakini pia ni mama wa matumaini katika makaribisho hayo ya wakimbizi!

06 May 2019, 10:30