Cerca

Vatican News
Mkutano wa amani kwa ushiriki wa viongozi wakuu wa madhehebu ya kidini huko Nezavisimost nchini Bulgaria Mkutano wa amani kwa ushiriki wa viongozi wakuu wa madhehebu ya kidini huko Nezavisimost nchini Bulgaria   (ANSA)

Hija ya kitume Buglagaria:Kufuata nyayo za Mt.Francis wa Assisi na kuwa wajenzi wa amani!

Baba Mtakatifu Francisko tarehe 6 Mei 2019 akiwa katika ziara yake ya kitume nchini Bulgaria na Macedonia ya Kaskazini amefanya mkutano wa amani ambapo wameshiriki viongozi wa madhehebu ya kidini chini Bulgaria katika uwanja wa Nezavisimost huko Sofia.Anakazia amani katika nyayo za Mtakatifu Francis wa Assisi

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Kila mmoja katika nyayo za Mtakatifu Francis wa Assisi anaalikwa kuwa mjenzi  wa amani. Amani ambayo tunapaswa kuomba na ambayo tunapaswa kuifanyia kazi, zawadi na zoezi, zawadi na juhudi isiyoisha kila siku na ili kuweza kutengeneza utamaduni ambapo amani  ndiyo inakuwa haki msingi. Ni moja ya mambo msingi ya msisitizo wa Baba Mtakatifu Francisko wakati wa mkutano kwa ajili ya amani kwa ushiriki wajumbe kutoka madhehebu mbalimbali ya dini yaliyopo nchini Bulgaria katika uwanja wa Nezavisimost huko Sofia.

Upendo wa kushuhudia ambao unaheshimu kazi ya uumbaji na kila mtu

Baba Mtakatifu Francisko akianza hotuba yake  hasa mara baada yak usali sala ya Mtakatifu Francis wa Assisi “ Bwana tufanye chombo cha Amani, amesema kuwa wamesali kwa kutumia maneno ya Mtakatifu Francis wa Assisi ambaye alikuwa ni mpenda sana Mungu muumbaji na Baba wa wote. Upendo upendo alioushuhudia ni kama ule ule wa ukweli katika kuheshimu kazi ya viumbe na kila mtu ambaye alikutana naye katika safari yake. Upendo ambao ulibadilisha mtazamo wake katika mwanga ambao unazaliwa kutokana na uhakika binafsi ya kwamba,anapendwa upeo mbali na na mambo yote ( evangelii gaudium), anathibitisha.

Upendo uliompelekea kuwa mjenzi wa kweli wa amani

Baba Mtakatifu Francisko akiendelea na hotuba yake anasema kufuatana na Mtakatifu Francis , hata kwa kila mmoja wetu katika nyayo zake anaalikwa kugeuka kuwa mjenzi na fundi seremala wa amani. Amani ambayo tunapaswa kuomba na ambayo tunapaswa kuifanyia kazi, zawadi na zoezi, zawadi na juhudi isiyoisha kila siku na ili kuweza kutengeneza  utamaduni ambapo amani inakuwa haki msingi. Amani hai na yenye nguvu dhidi ya kila aina ya mtindo wa ubinafsi na sintofahamu, ambazo zinatufanya tutafute faida zetu binafsi na baadhi katika hadhi isiyo kiukwa ya kila mtu.

Amani inatakiwa na inataka tufanye mazungumzo

Amani inatakiwa na inataka tufanye mazungumzo ambayo ni njia ya ushirikiano wa pamoja, uelewa wa pamoja wa mitindo na mantiki zake (Hati ya mwisho ya udugu wa kibinadamua, Abu Dhabi,4 Februari 2019) na ili kuweza kukutana katika kile kinacho unganisha, kuheshimiana kile kinacho tutenganisha na kuwa na ujasiri wa kutia moyo katika kutazama wakati ujao kama nafasi na fursa yenye hadhi hasa hasa kwa ajili ya kizazi kijacho.

Baba Mtakatifu francisko pia anathibi tisha kwa jinsi gani jioni hiyo wameunganika kwa ajili ya kusali mbele ya mienge iliyo washwa na kuletwa na watoto. Hiyo ni ishara ya moto wa upendo ambao umewashwa tayari ndani mwetu na ambao lazima ugeuke kuwa taa ya huruma, ya upendo katika mazingira ambamo tunaishi. Katika moto huo wa upendo, Baba Mtakatifu amesema,“sisi tunataka kuyeyusha barafu ya vita”. Tunafanya tukio hili la amani juu ya uharibifu wa mji wa zamani wa Serdika karibu na  Sofia moyo wa Bulgeria”. Na kwa maana hiyo anaongeza kusema: kutoka hapo wanaweza kuona maeneo ya ibada ya makanisa tofauti ya imani ya dini. Maeneo hayo ni kama ya Mtakatifu Nedelia kwa upande wa ndugu zetu waorthodox, Mtakatifu Yosefu kwa wakatoliki, Sinagogi ya ndugu zetu wayahudi, msikiti wa ndugu zetu waislam na karibu kuna Kanisa la Warmenia.

Zamani maeneo ya Sofia huko Bulgaria ilikuwa ni yenye makundi mbalimbali ya utamaduni na dini

Katika maeneo hayo kwa karne nyingi hasa katika eneo la Sofia huko Bulgaria lilikuwa ni yenye makundi mbalimbali ya utamaduni na dini, kwa ajili ya kukutana na kujadiliana. Kutokana na hiyo Baba Mtakatifu Francisko ameongeza kusema: “sehemu hii inaweza kuwa shala ya kuwakilisha ushuhuda wa amani. Kwa wakati huu sauti zetu zinaungana kwa pamoja na kuonesha shauku hai ya amani: amani iweze kuenekana   duniani kote!  Katika familia zetu, kwa kila mmoja wetu, hasa katika maeneo ambayo sauti zimenyamazishwa na vita, zimesongwa na kutojali, zinapuuzwa kwa usumbufu mkubwa na kukandamizwa na makundi husika yenye kutafuta faida.  Baba Mtakatifu anawahimiza na kuwashauri ya kwamba “Wote tushirikiane ili kuweza kutimiza malengo haya na hasa kwa upande wa  wahusika wa dini, wa siasa na  utamaduni. Kila mmoja mahali  alipo Baba Mtakatifu anashauri asema: “Bwana nifanye chombo cha amani yako”. Na kwa kuhimitimisha ni matarajio ya Baba Mtakatufu Francisko ya kuweza kutimiza ndoto ya Papa Yohane XXIII  katika ardhi ambayo  alitamani amani iwe kama nyumba. “Tufuate shauku kwa njia ya maisha na kusema: “pacem in terris!  Amani juu ya ardhi na kwa watu wote wapendwa wa Bwana”!

07 May 2019, 09:30