Akiwa ziara yake ya Kitume tarehe 7 Mei 2019 Baba Mtakatifu Francisko ameadhimisha Misa Takatifu katika uwanja wa Macedonia Akiwa ziara yake ya Kitume tarehe 7 Mei 2019 Baba Mtakatifu Francisko ameadhimisha Misa Takatifu katika uwanja wa Macedonia 

Hija ya Kitume:Papa anahimiza kuacha Yesu ashibishe njaa na kiu zetu!

Yesu yupo katika sakramenti ya altare na Yesu katika sakramenti ya ndugu.Ndiyo moja kati ya ufafanuzi wa Baba Mtakatifu kwa waamini wa Skopje akiwaalika wajibu mwaliko wa kumfuata Yesu kwa kujikita katika mwendo wa kushinda vizingiti vya kujifunga na kuwa na mazoea.Ametumia mfano wa Mama Teresa aliyekutana Yesu katika Ekaristi na masikini

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Tarehe 7 Mei 2019 wakati wa misa Takatifu katika uwanja wa Macedonia huko Skopje kwa kuongozwa na Injili iliyosomwa ya Yohane katika maneno:“yeye ajaye kwangu hataona njaa, naye aniaminiye hataona kiu kamwe, Baba Mtakatifu Francisko amesisitizia juu ya sakramenti ya altare na sakaramenti ya ndugu, hasa kwa kutoa mfano wa mama Teresa aliyekuwa na njaa ya Mungu na akakutana naye katika Ekaristi na kwa masikini. Baba Mtakatifu Francisko akianza mahubiri anasema: Katika Injili inaonesha karibu na Yesu amezungukwa na umati ambapo machoni pao bado walikuwa na mtazamo wa miujiza ya mikate. Ni moja ya kipindi kilichobaki machoni pa kila mtu na katika mioyo ya Jumuiya ya kwanza ya wafuasi. Ilikuwa ni sikukuu… Sikukuu ya kugundua wingi na wema wa Mungu kwa ajili ya watoto wake ambao wamekuwa ndugu kwa kugawana na kushirikisha mkate. Baba Mtakatifu amewaomba wafikirie muda huo  kama ulivyokuwa wa umati ule!  Jambo fulani lilikuwa limebadilika. Na kwa muda mfupi yupo mtu aliyekuwa na kiu na kwa ukimya akimfuata Yesu wakati wa kutoa neno, alikuwa na uwezo wa kugusa kwa mikono yake na kuhisi kwa mwili wake mmujiza wa kindugu wenye uwezo wa kushibisha na kusaza.

Bwana alikuja kutoa maisha katika dunia

Bwana alikuja kutoa maisha katika dunia na anafanya daima kuchangamotisha hata mahesabu yetu, unafiki wa matarajio na ujujuu wa akili zetu; anaweka mjadala wa mitazamo yetu na uhakika wetu na kutualika ili tuweze  kupitia maono mapya ambayo yanatoa nafasi kwa namna tofauti ya kujenga hali halisi.  “Yeye ni Mkate hai ulioshuka kutoka mbinguni, yeye ajaye kwangu hataona njaa,naye aniaminiye hataona kiu kamwe”.  Hata hivyo  Baba Mtakatifu Francisko ameongeza kusema, umati ule wa watu waligundua kuwa, njaa ya mkate ilikuwa  hata na  matukio mengine ya njaa kama vile, njaa ya Mungu, njaa ya udugu, njaa ya kukutana, ya sikukuu, ya kushirikishana. Baba Mtakatifu anasema, tumezoea kula mkate mgumu wa kutofahamika na kuishia kuwa wafungwa wasioaminika, kubandikwa mabango na ulaghai; tunaamini kwamba tunafanaishwa, au tungeweza kukidhi  kiu yetu na tunaishia kunywa katika tofauti na kutokuwa na hisia; tumejilisha kwa ndoto zinazong’aa na ukuu na kuishia kula kwa kufungwa na upweke; tumekabwa na mawasiliano na kupoteza ladha ya undugu.  Tulitafuta matokeo ya haraka na kwa usalama na tunajikuta tumekandamizwa na ukosefu wa kutokuwa na uvumilivu na wasiwasi. Wafungwa wa mitandao na kupoteza ladha na ladha ya ukweli.

Tuna njaa Bwana ya kukutana na Neno lako lenye uwezo wa kuamkasha matumaini

Akiendelea na mahubiri Baba Mtakatifu anathibitisha kuwa, “Tuseme kwa nguvu na bila hofu”; tuna njaa ya Bwana… Tuna njaa, Bwana njaa ya mkate na njaa ya Neno lako yenye uwezo wa kufungua kufungwa kwetu na upweke wetu; tuna njaa Bwana ya udugu mahali ambalo sintofahamu na kutokuaminiana, ulaghai haujazi meza zetu, na wala kuwa na nafasi ya kwanza katika nyumba zetu. Tuna njaa Bwana ya kukutana na Neno lako lenye uwezo wa kuamsha matumaini, kuamsha upendo  wa hisia ya moyo ili kuanza kutafuta njia za mabadiliko na uongofu. Tunayo njaa Bwana ya kufanya uzoefu kama ule wa umati, wa miujiza ya huduma yako, uwezo wa kuvunja mazoea na kugawana  na kishirikishana kwa uhuruma ya Bwana kwa kila mtu, hasa hasa wale ambao hakuna anaye wajali, ambao wamesahulika au kudharauliwa. Tusema kwa nguvu bila kuogopa tuna njaa Bwana; ya Mkate wa neno lako na  mkate wa udugu!

Aidha Baba Mtakatifu Francisko ameelezea jinsi gani kwa muda kitambo watakwenda mbele ya altare kwa ajili ya kumwilishwa kwa Mkate wa Maisha katika kufuata wito wa Bwana asemaye “yeye ajaye kwangu hataona njaa, naye aniaminiye hataona kiu kamwe” (Gv 6,35). Ni jambo moja tu ambalo Bwana anatuomba: Njooni. Anatualika kujikita katika safari, katika mwendo. Anatushauri kutembea kuelekea kwake ili kuweza kushiriki maisha yake mwenywewe na utume wake mwenyewe. “Njooni” anasema Bwana: kuja huko hakuna maana tu ya kubadilisha nafasi kwenda nyingine, bali ni kuwa na uwezo wa kuacha uondoke na ubadilishwe kwa njia ya Neno lake katika uchanguzi wetu, katika mawazo yetu, katika vipaumbele, ili kufanya ishara zake na kuzungumza kwa lugha yake mwenyewe, “lugha ya mkate ambao ni  upendo, wa kusindikiza, wa kujitolea kwa ukarimu kwa wengine, upendo wa dhati unaodunda ili ukawaida uweze kugeuka halisi.

Njaa ya mkate, njaa ya udugu na njaa ya Mungu

Kila Ekaristi, Bwana anamega Mkate na kugawanya na kutualika sisi tumege na kugawa pamoja na Yeye kwa kushiriki katika miujiza ya mkate ambayo ina maana ya kufika na kugusa kila kona ya mji huo na nchi hiyo, katika ardhi hiyo kwa upendo na  huruma kidogo, anasisitiza Baba Mtakatifu Francisko. Njaa ya mkate, njaa ya udugu, njaa ya Mungu. Ni kwa jinsi gani Mama Teresa alikuwa anatambua vema hayo na alipendelea kuanzisha maisha yake juu ya mihimili miwili yaani: Yesu aliye ndani ya Ekaristi na Yesu aliyeingia ndani ya masikini! Ni upendo tunao upokea  na upendo tunao utoa. Ni mihimili miwili siyo tenganishwa ambayo alifuata katika safari yake kwa lengo la kumaliza njaa na kiu. Alikwenda kwa Bwana na katika kitendo hicho alikwenda kwa ndugu yake aliyedharauliwa, asiye pendwa, mpweke na kusahuliwa; alikwenda kwa kaka yake na akakutana na uso wa Bwana ... Kwa maana alikuwa anajua kuwa upendo wa Mungu na upendo wa jirani ambao wanakuwa pamoja. Kwa aliye  mdogo zaidi tunakutana na Yesu mwenyewe na katika Yesu tunakutana na Mungu”, na upendo huo ndiyo wa kipekee unaoweza kukidhi njaa yake.

Kwa kuhitimisha Baba Mtakatifu amesema leo hii Bwana amefufuka na anaendelea kutambea katikati yetu, mahali ambapo anapita, anacheza na maisha ya kila siku. Yeye anatambua njaa zetu na kutueleza tena: “yeye ajaye kwangu hataona njaa, naye aniaminiye hataona kiu kamwe (Yh 6,35). Anatutia moyo pamoja ili kusimama na kufanya uzoefu wa wingi wa upendo wake; tuache Yeye aweze kushibisha njaa zetu na kiu zetu katika sakramenti ya altare na katika sakramenti ya ndugu.

07 May 2019, 13:01