Tafuta

Vatican News
Tarehe 6 Mei 2019 Papa Francisko ametoa Komunio ya kwanza kwa watoto 245 katika Kanisa la Moyo Mtakatifu huko Rakovsky nchini Bulgaria Tarehe 6 Mei 2019 Papa Francisko ametoa Komunio ya kwanza kwa watoto 245 katika Kanisa la Moyo Mtakatifu huko Rakovsky nchini Bulgaria  (Vatican Media)

Hija ya kitume:Bulgaria:Hatumwoni Yesu kwa macho bali ni katika macho ya imani!

Baba Mtakatifu Francisko,Jumatatu tarehe 6 Mei 2019 wakati wa hija yake ya kitume nchini Bulgaria,ameadhimisha Ibada ya Misa Takatifu katika Kanisa la Moyo Mtakatifu huko Rakovsky,ambapo ametoa Komunio ya Kwanza kwa watoto 245.Utambulisho wetu:Mungu ni Baba yetu,Yesu ni kaka yetu,Kanisa ni familia yetu,sisi ni ndugu na sheria ni upendo.

Na  Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Baba Mtakatifu Francisko, Jumatatu tarehe 6 Mei 2019 wakati wa hija yake ya kitume nchini Bulgaria, ameadhimisha Ibada ya Misa Takatifu katika Kanisa la Moyo Mtakatifu huko Rakovsky, ambapo ametoa Komunio ya Kwanza kwa watoto 245. Baba Mtakatifu katika mahubiri yake amejikita kwanza kuwasalimia watoto wote ikiwa ni pamoja na  wazazi wao, ndugu na marafiki. Kwa wote amependa kutumia salam wanayoitumia katika nchi yao wakati wa kipindi cha Pasaka:“Christos vozkrese! Maana yake “Kristo amefufuka”. Christos vozkrese! Yaani Kristo amefufuka, Salam hiyo ni kielelezo cha furaha kwa wakristo wote amesema Baba Mtakatifu na wafuasi wa Yesu kwa sabababu  aliyetoa maisha kwa upendo juu ya msalaba ili kuharibu dhambi, amefufuka na kutufanya kuwa watoto wa Mungu  Baba. Na ni furaha kwa wote kwa sababu yeye anaishi na yuko kati yao leo hii na daima.

Hatumwoni Yesu kwa macho bali kwa macho ya imani

Baba Mtakatifu Francisko akiendelea na mahibiri kwa watoto wote, anasema, wamefika kutoka kila kona ya ardhi hiyo nyekundu ili kushiriki sikukuu ya maajabu na ambayo kwa hakika anathibitisha hawatasahau kamwe katika maisha yao, yaani mkutano wao wa kwanza na Yesu katika Sakaramenti ya Ekaristi. Lakini mmojawapo anaweza kuuliza: ni kwa jinsi gani ya kukutana na Yesu aliyeishi kwa miaka mingi na baadaye akafa na akawekwa kwenye kaburi? Kwa kufafanua anasema  ni kweli Yesu alifanya tendo kubwa la upendo kwa ajili ya kuokoa ubinadamu wa nyakati zote. Alibaki kaburini kwa siku tatu, lakini sisi tunajua kutokana na mitume, waliotuahikishia na mashuhuda wengine waliomwona akiwa hai na ambaye  Mungu Baba yake na Baba yetu alimfufua. Na sasa Yesu ni hai, yupo pamoja nao na kwa siku hiyo wanaweza kukutana naye katika Ekaristi. “Hatumwoni kwa macho, lakini tunamwona kwa macho ya imani”, amethibitisha Baba Mtakatifu.

Ninaomba hapa nguo na joho jeupe; Miujiza ilitokana na mtoto aliyepeleka mikate mitano na samaki wawili

Baba Mtakatifu Francisko anasema katika mahubiri: “ninaoomba hapa nguo na joho jeupe: Hii ni ishara muhimu na nzuri kwa sababu ninyi mmevaa nguo za sikukuu. Komunio ya kwanza awali ya yote ni sikukuu, ambayo tunaadhimisha Yesu aliye ipendakeza ibaki karibu nasi daima na ambayo isitengenishwe nasi kamwe. Ni sikukuu ambayo iliwezekana kutokana na mababa zetu, mababu zetu, familia zetu na jumuiya ambayo imewasaidia kukua katika imani”. Ili kuweza  kufika katika mjini wa Rakovsky, wamesafiri kwa mwendo mrefu. Mapadre wao na makatekista waliowaandaa katika mchakato wa katekesi, wamewasindikiza hata katika njia inayowapeleka leo hii kukutana na Yesu na kumpokea katika mioyo yao.  Yeye kama ilivyosemeka katika  Injili ya siku ( Yh 6,1-15), Baba Mtakatifu amesema, siku moja alifanya mmujiza wa mikate mitano na samaki wawili kwa kuwashibisha umati ambao ulikuwa unamfuata na kumsikiliza. Baba Mtakatifu amewauliza swali: je mmeweza kutambua ni kwa jinsi gani miujiza inaanza? Inatoka katika mikono ya mtoto mmoja aliyepeleka kile alicho kuwa nacho, yaani  mikate mitano na samaki wawili (Yh 6,9).

Na wakati huo huo, Baba Mtakatifu amesema, ndiyo mtindo ambao unaowasaidia kutimiza miujiza  ya  kuwafanya wakumbushe wote hasa watu wazima walioko pale juu ya mkutano wa kwanza wa kukutana na Yesu katika Ekaristi  na kuweza kushukuru siku ile. Leo hii Baba Mtakatifu anongeza “ inaturuhusu kufanya  sikukuu kwa upya  na kuadhimisha  Yesu ambaye yupo katika maumbo ya Mkate wa Maisha. Hiyo ni kukuonesha kwamba kuna miujiza ambayo inaweza kuonekana tu iwapo tuna moyo kama wa watoto, wenye uwezo wa kushirikisha, kuota ndoto, kushukuru, kuwa na imani na kuheshimu wengine. Kupata Kumunio ya Kwanza maana yake ni kupenda kuunganika kila siku na Yesu, kukua katika urafiki na Yeye na kutamani ya kwamba hata wengine wanaweza kufurahi, furaha anayotaka kutupatia. Bwana anahitaji watoto ili aweze kutimiza miujiza ya kufikisha furaha yake kwa marafiki wao wengi na familia.

Kushiriki furaha yao ili wakutane na Yesu

Baba Mtakatifuakisisitiza zaidi amependa  kuonesha furaha yake ya kushirikisha nao katika kipindi hicho muhimu na kuwasaidia wakatane na Yesu. Anasema, wao wanaiishi siku kwa dhati katika roho ya urafiki, ya furaha, ya kindugu na umoja kati yao na Kanisa zima ambalo kwa namna ya pekee katika Ekaristi inalezea umoja kidugu kati ya wajumbe wake wote. Utambulisho wetu ni huu; Mungu ni Baba yetu, Yesu ni kaka yetu, Kanisa ni familia yetu, sisi ni ndugu na sheria ni upendo.

Kwa kuhitimisha mahubiri yake, Baba Mtakatifu Francisko, amependa kuwatia moyo ili wasali daima kwa shauku kubwa na furaha ambayo walioyo nayo katika siku hii. Na wakumbuke kuwa hiyo ni sakramenti ya Kumunio ya kwanza lakini  siyo ya mwisho pia wakumbuke kuwa Yesu anawasubiri daima. Kwa maana hiyo anawatakia kuanzia leo hii  iwe kama ndiyo mwanzo wa Komunio nyingi kwa sababu mioyo yao iweze kuwa  daima kama leo hii, yaani katika sikukuu iliyojaa furaha na zaidi kuwa na shukrani.

Kupokea Komunio ya kwanza katika mikono yake

Kabla ya kuwapatia Kumunio ya kwanza katika maumbo mawili ya "mkate na divai", kwa watoto 245, kama paroko anaye wasaidia wadogo, amewashauri wasifikirie kingine, lakini wapokee mwili wa Kristo katika ukimya, na hata kwa mara nyingine kabla ya kwenda kupokea, wawasamehe hata wale ambao wamegombana nao. Kwa maana hiyo mstari mrefu umefika mbele ya Baba Mtakatifu Francisko, ambapo ni kwa mara ya kwanza kutoa  Komunio ya Kwanza akiwa katika ziara yake ya kitume kimataifa na kwa njia ya mikono yake watoto hao wamekutana na kumpokea Yesu.

Shukrani za pekee

Baada ya salam za Askofu Gheorghi Ivanov Jovcev, wa jimbo la Sofia na Plovdiv, ambaye amethibitisha ni kwa jinsi gani watoto wameelewa kuwa:njia ya kumpenda Bwana na jirani siyo ile ya ya kutembea siku moja, bali ni katika  maisha yote, zimefuatia baraka na shukrani za Baba Mtakatifu Francisko kwa wote, kwa maaskofu na familia na hata wote walioshiriki misa hiyo kwa namna ya pekee wagonjwa na wazee. Vile vile shukrani za Papa zimewaendea viongozi wote wa nchi na wote waliochangia kuandaa  maadhimisho hayo, hata kwa kufanikisha ziara yake nchini Bulgaria. Maadhimisho hayo yamefungwa kwa kuwasalimia wadogo ambao wamerushwa mawaridi meupe.

06 May 2019, 11:45