Tafuta

Vatican News
Katika Katekesi yake Baba Mtakatifu amewakumbuka wazee, vijana, wagonjwa na wanandoa wapya Katika Katekesi yake Baba Mtakatifu amewakumbuka wazee, vijana, wagonjwa na wanandoa wapya  (Vatican Media)

Maria Conception Cabrera ni mama wa familia,alishuhudia thamani ya wokovu wa msalaba wa Kristo!

Baba Mtakatifu Francisko wakati wa katekesi yake tarehe 8 Mei 2019 ikiwa ni siku moja baada ya ziara yake ya kitume nchini Bulgaria na Macedonia Kaskazini amependa kuwashirikisha waamini na mahujaji kuotka pande za dunia waliofika katika uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican kuhusu ziara ya 29 ya kitume.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Mara baada ya katekesi yake  tarehe 8 Mei 2019 iliyo jikita kusimilia juu ya ziara yake ya kitume nchini Bulgeria na Macedonia Kaskazini tangu 5-7 Mei 2019, kwa mahujaji na waamini wote waliofika katika kiwanja cha Mtakatifu Petro, Vatican, amekumbusha kuwa, Jumamaosi 4 Mei 2019 katika mji wa Mexico alitangazwa mwenye heri  Maria de la Conception Cabrera, mama wa familia ambaye alishuhudia thamani ya wokovu wa msalaba wa Kristo na kumsaidia kuanzisha taasisi mbalimbali za kitawa na kilei. “Tumshukuru Mungu kwa ajili ya  ujasiri wake na kwa kimpigia makofi mwenye heri Conchita!

Tarehe 8 Mei Sikukuu ya Mama Maria wa Pompei 

Baada ya kutoa salam mbalimbali kwa makundi mengi kutoka duniani kote, hakusahau kwa namna ya pekee vijana, wazee, wagonjwa na wenye ndoa wapya. Amekumbusha kuwa tarehe 8 Mei ni siku ya maombi kwa Mama Maria wa Pompei Mama wa Rosari. “Tumeungana pamoja kiroho na wale wote walioko katika Madhabahu ya Mama ili kwa  mtazamo wake juu ya dunia aweza kutuombe na kwa ajili ya Kanisa zima na wale wote wanaoteseka kiroho na kimwili”.

Kuombea nchi ya Argentina

Vile vile Baba Mtakatifu Francisko amekumbusha kuwa, katika nchi yake Argentina wanaadhimisha Sikukuu ya Mama Yetu wa Lujan (Nuestra Señora de Luján), kwa maana hiyo ameomba kusali wote kwa ajili ya nchi ya Argentina.

08 May 2019, 13:52