Katekesi ya Baba Mtakatifu Francisko tarehe 8 Mei 2019 ni kuhusu ziara yake ya kitume! Katekesi ya Baba Mtakatifu Francisko tarehe 8 Mei 2019 ni kuhusu ziara yake ya kitume! 

Katekesi:Papa amesimulia juu ya ziara yake ya kitume!

Baba Mtakatifu Francisko wakati wa katekesi yake tarehe 8 Mei 2019 ikiwa ni siku moja baada ya ziara yake ya kitume nchini Bulgaria na Macedonia Kaskazini amependa kuwashirikisha waamini na mahujaji kuotka pande za dunia waliofika katika uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican kuhusu ziara ya 29 ya kitume.

Na Sr Angela Rwezaula  - Vatican

Tarehe 8 Mei 2019 mara baada ya kusoma somo kutoka Injili ya (Luka,12, 22.30-32) isemayo: Akawaambia wanafunzi wake, kwa sababu hiyo nawaambia, msisumbukie maisha yenu, mtakula nini; wala miili yenu, mtavaa nini; kwa maana, hayo yote ndiyo watafutayo mataifa ya duniani, lakini Baba yenu anajua ya kuwa mna haja na hayo. bali utafuteni ufalme wa Mungu, mengine yote mtaongezewa. Msiogope, enyi kundi dogo; kwa kuwa Baba yenu ameona vema kuwapa ule ufalme”. Baba Mtakatifu ameanza katekesi yake kwa kuwasimulia juu ya ziara yake ya kitume ya kina ya  siku tatu katika nchi za Bulgaria na Macedonia Kaskazini. Anamshukuru Mungu aliyemwezesha kutimiza zaira hizi na kupyaisha shukrani za kipekee kwa viongozi wa nchi hizi mbili ambao walimkaribisha kwa shauku kubwa na uwezekano wao mkubwa. Kwa maaskofu, sambamba na Jumuiya  nzima ya Kanisa kwa makaribisho na ibada yao iliyo msindikiza kufanikisha hija yake.

Katika nchi ya Bulgaria ameongozwa na kumbukumbu ya Mtakatifu Yohane XXIII

Baba Mtakatifu amesema kwamba katika nchi ya Bulgaria ameongozwa na kumbukumbu ya Mtakatifu Yohane XXIII ambaye alitumwa katika nchi hiyo kuitembelea kunako mwaka 1925 kama mwakilishi wa kitume wa Vatican. Kwa kuongozwa na mfano wake mwema na upendo wa kichungaji, Baba Mtakatifu anathibitisha  kukutana  na watu na kuwaalika wafanye kama daraja kati ya Ulaya ya Kati, Mashariki na Magharibi akiwa na kauli mbiu: “Pacem in terris”. Na ameaalika wote kutembea katika njia za udugu; na katika njia hiyo kwa namna ya pekee alipata furaha ya kutimiza hatua ya mbele kwa  kukutana na Patriaki wa Kanisa la Kiorthodox Bulgara Neofit na wajumbe wa Sinodi Takatifu. Kwa hakika amesema, kama wakristo, wito wetu na utume wetu ni kuwa ishara na chombo cha umoja na tunaweza kuwa, kwa sababu ya msaada wa Roho Mtakattifu anayetengeza yote na kuunganisha kile ambacho kilitutenganisha au bado kinatutengenisha.

Hata hivyo pia amesema: Kwa sasa nchini Blgaria ni moja ya nchi za uinjilishaji kwa njia ya watakatifu Syril na Methodius ambao Mtakatifu Yohane Paulo II  alipenda kuwaungaisha na Mtakatifu Benedikto kuwa wasimamizi wa bara la Ulaya. Huko Sofia katika Kanisa la Upatriaki wa Mtakatifu Nevkij, Baba Mtakatifu amesema: nilisimama katika sala mbele ya picha ya ndugu wawili watakatifu. Hawa, asili yao ni wagiriki wa Salonika, waliotambua kutumia ubunifu wao wa utamaduni ili kueneza ujumbe wa kikristo kwa waslavi. Hawa walianzisha alfabeti mpya na kutafsiri Biblia katika lugha ya kislavi na maandiko mengine ya kiliturujia. Ka maana hiyo anasema: “ hata leo hii kuna haja ya kuwa na wanjilishaji, wenye shauku na ubunifu, ili Injili iweze kufika kwa wale wote ambao bado hawaitambui na kumwagilia kwa upya ardhi zenye mizizi ya kizamani kikristo na ambayo imenyauka. Katika upeo huo, Baba Mtakatifu Francisko anasema aliadhimisha mara mbili Ekaristi Takatifu na Jumuiya Katoliki nchini Bulgaria, na kuwatia moyo ili wawe na matumaini hai. Anawashukuru tena watu wa Mungu ambao wameonesha imani kubwa na upendo mkubwa.  Tendo la mwisho nchini Bulgaria alilolifanya Baba Mtakatifu na wawakilishi wa madhehebu tofauti, walimwomba Mungu zawadi ya amani, wakati huo huo kikundi cha watoto walikileta mishumaa inayowaka ishara ya imani na matumaini.

Ziara ya Baba  Mtakatifu nchini Macedonia ya Kaskazini

Baba Mtakatifu Francisko akiendelea kusimulia  ufupisho wa ziara yake ya kitume, kwa waamini na mahujaji amesema: huko Macedonia Kaniskazini, amesindikizwa kwa nguvu ya uwepo kiroho wa Mama Teresa  wa Calcutta, ambaye alizaliwa huko Skopje mwaka 1910 na pale  ndipo ilikuwa ni parokia yake, alipokea Sakramenti za kwanza za ukristo na kujifunza kumpenda Yesu. Mwanamke huyo mdogo, lakini aliyekuwa amejaa nguvu ya neema ya mateso yake katika Roho Mtakatifu, tunaweza kuona sura ya Kanisa katika nchi hiyo na katika pebezoni mwa dunia, jumuiya ndogo ambayo kwa neema ya Kristo imegeuka kuwa  nyumba ya makaribisho na mahali ambapo wengine wanapata faraja kwa ajili ya maisha yao. Akiwa katika jumba la makumbusho ya Mama Teresa, amesali kwa uwepo  wa viongozi wengine wa kidini na kukutana na kikundi cha masikini pia kubariki jiwe la kwanza la msingi kwa ajili ya ujenzi wa madhabahu ya Mama Taresa

Nchi ya Macedonia Kaskazini ilipata uhuru 1991

Hata hivyo Baba Mtakatifu amesema Macedonia Kaskazini, ni nchi iliyopata uhuru wake kunako 1991. Vatican imetafuta namna ya kusaidia hatua za mwanzo katika safari yao na kwa maana hiyo katika ziara yake, amependelea kuwatia moyo hasa utamaduni wao wenye uwezo wa kukaribisha na kuwapo makabila mengi na dini; kama vile hata jitihada za kukaribisha na kuwakimbilia kwa kiasi kikubwa wahamiaji na wakimbizi waliofika katika kipindi kigumu cha mwaka  2015 na  2016. Katika nchi hiyo kuna makaribisho makubwa na moyo mkuu amesisitiza! Wahamiaji ndiyo  wanaleta matatizo kwao, lakini wanawapokea na kuwapenda na matatizo yanapata suluhisho. Hii ndilo jambo kubwa la watu hao, kutokana na hivyo  Baba Mtakatifu ameomba wapigiwe makofi… Ni nchi kijana Macedonia Kaskazini kwa mtazamo wa kikatiba anaendelea kusema; nchi ndogo na yenye kuhitaji kujifungulia upeo mkubwa bila kupoteza mizizi yake. Kwa hiyo ilikuwa na maana kubwa ya kukutana na vijana.  Wavulana na wasichana wa imani tofauti ya kikristo, hata  dini nyingine kama vile  waislam kwa mfano ambao wote kwa pamoja wanaunganika ili kuweza kujenga jambo zuri la maisha. Baba Mtakatifu anathibitisha alivyo washauri waote yaliyo makubwa na kujiweka katika mchezo kama kijana Agnes yaani (Mama Teresa),wasikilize sauti ya Mungu inayozungumza katika sala na katika mwili wa ndugu anayehitaji.

Baba Mtakatifu Francisko, pia kufuatana ma mfano huo anasema ni  kwa jinsi gani alivyoshangaza wakati amekwenda kuwatembelea Watawa wa Mama Teresa:“ walikuwa masikini na ameshangazwa kwa upole wa kiinjili wa wanawake hao. Upole huo, unazaliwa kutokana na sala na kuabudu. Mara nyingi sisi wakristo, tunapoteza ukuu huu wa upole na uhuruma na iwapo hakuna upole tunageuka kuwa wagumu na asidi. Watawa hawa walikuwa ni wapole katika huruma na wanatoa upendo bila unafiki. Kwa sababu unatenda matendo ya upendo bila huruma, bila upendo ni kama vile kwenye matendo yetu unamwaga siki ndani ya kikombe. Na kumbe upendo ni furaha na siyo asidi. Watawa wale ni mfano na Bwana awabariki wote,amesisitiza Baba Mtakatifu Francisko.

Vishawishi vya makuhani na watu wengine walio wekwa wakfu

Licha ya ushuhuda wa vijana huko Skopje alio usikiliza ni pamoja na mapadre na watu wenye wakfu. Wanaume na wanawake ambao wametoa maisha yao kwa Kristo. Hata hivyo Baba Mtakatifu amebainisha kwamba, kwa upande wake, awali au baadaye hujitokeza vishawishi vya kufikiria: “kwanini  Bwana watu wangu hawa, zawadi ndogo mbele ya matatizo ya Kanisa na ya dunia?  Kwa upande huo, amewakumbusha kidogo kuwa na  chachu ya kukuza na kidogo manukato safi ambayo yanatoa harufu na kuenea katika mazingira yote. Ndiyo utume wa Yesu wa Ekaristi, mbegu ya maisha mapya kwa ajili ya ubinadmu wote. Katika misa iliyoadhimisha katika uwanja wa Skopje, wameweza kupyaisha kwa mara nyingine tena upendo  wa pembeni mwa Ulaya ya leo, miujiza ya Mungu katika mikate michache na samaki, vilivyomegeka na kushirikisha, kwa kushibisha njaa za wengi. Na kwa wingi wa zawadi za Mungu, Baba Mtakatifu amesema, tukabidhi wakati uliopo na ujao wa watu ambao amewatembelea katika ziara yake ya kitume. Amewaalika kusali kwa Bikara Maria ili aweze kubariki nchi hizo mbili Bulgaria na Macedonia ya Kaskazini. (Salam Maria …)

08 May 2019, 14:28