Tafuta

Vatican News
Tarehe 6 Mei 2019 Baba Mtakatifu amekutana na Jumuiya Katoliki katika Kanisa la Malaika Mkuu Mikaeli huko Rakovsky Tarehe 6 Mei 2019 Baba Mtakatifu amekutana na Jumuiya Katoliki katika Kanisa la Malaika Mkuu Mikaeli huko Rakovsky  (Vatican Media)

Hija ya kitume:Bulgaria:Kutazama kwa macho ya imani na upendo!

Papa akiwa nchini Bulgaria amekutana na jumuiya katoliki katika Kanisa la Mtakatifu Mikaeli Malaika Mkuu na kuwaalika waamini wasipoteze wakati kwa kulia, badala yake watazame daima jambo la kufanya na la dhati.Ni muhimu kutazama kwa macho ya imani na upendo kwa kufuata nyayo za watakatifu Cyril na Methodius

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Tarehe 6 Mei 2019 Baba Mtakatifu amemtakia sikukuu njema ya kuzaliwa Askofu Ivanov Jovcev wa  Sofia na Plovdiv mwanzoni mwa mkutano wake na jumuiya katoliki ya Rakovsky na pia ikiwa ni sikukuu ya mwajina wake ambapo amewaomba wampigie makofi! Baba Mtakatifu Francisko akiwa katika ziara yake ya kitume nchini Bulgaria na Macedonia ya Kaskazini, mchana amekutana na Jumuiya katoliki ya Rakovsky akiwashukuru kwanza kwa wamakaribisho yao, kwa ngoma na ushuhuda. Na kwamba  wamweleza juu ya tafsiri ya moja kwa moja, hivyo ni sawa namna hiyo.  Baba Mtakatifu amesema, "Askofu Iovcev ameniomba kuwasaidia katika furaha hii ya kukutana na watu wa Mungu na sura elfu moja na karama nyingi ili kutafakari juu ya   kutazama kwa “macho ya imani na upendo”.  Hata hivyo anawashukuru awali ya yote kumfanya yeye mwenyewe aone vizuri na kutambua kidogo zaidi, sababu ya ardhi hiyo iliyokuwa inapendwa sana na yenye maana kwa Mtakatifu Yohane XXIII, mahali ambapo Bwana alikuwa akimwandaa ili aweze kusogea katika nafasi muhimu ya safari  ya Kanisa. Kati yao, inachanua hata urafiki wa nguvu kati ya ndugu waorthodox ambao aliweza kupata msukumo wa kuweza kunza mchakato wa nchi ya kundugu kati ya jumuiya, licha ya ugumu.

Maneno ya Papa Mwema katika hotuba ya mtaguso wa II wa Vatican kunako  1962

Baba Mtakatifu Francisko katika kutafakari juu ya kuwa na "macho ya imani" amependelea kukumbusha maneno ya Papa mwema (Yohane XXIII) ambaye alijua jinsi ya kuimarisha moyo wake na Bwana kwa namna ambayo ungeweza kusema kuwa hakukubaliana na wale waliokuwa  karibu naye lakini  wakitazama mabaya tu na ambao wangeitwa kuwa manabii wa matukio. Kwa mujibu wake ilikuwa ni lazima kuwa na imani katika msaada wa Mungu anaye tusindikiza kila wakati  hata  katikati ya shida; ana uwezo wa kutengeneza miundo mikuu zaidi isiyotarajiwa (Hotuba ya ufunguzi wa Mtaguso II wa Vatican, 11 Oktoba 1962). Watu wa Mungu Baba Mtakatifu Francisko anasema, ni wale ambao wanajifunza kutazama, kuamini, kugundua na kuacha waongozwe na nguvu ya ufufuko. Watambua kwamba zipo hali au kivipindi vya uchungu na kwa namna ya pekee pasipo na haki, lakini hawabki wamejikunyata mikono yao, kwa hofu au kukuza hali halisi za kutoamini na usumbufu kwa maana hali hizo, hazina  maana katika roho, na zaidi zinaleta udhaifu wa matumaini na kuzuia kila aina ya uwezekano wa kupata suluhisho. Watu wa Mungu ni wale wenye ujasiri wa kufanya hatua ya kwanza na kutafuta kwa ubunifu wakiwa mstari wa mbele kushuhudia kwamba upendo haujafa, bali umeshinda vizingiti, anasisitiza Baba Mtakatifu FRanciskp. Wao wanajiweka katika mchezo na ambao wamejifunza kwamba  katika Yesu, Mungu mwenyewe ni kwa  kujikabidhi mikononi mwake. Yeye kwanza alithubutu na kutosa mwili wake ili pasiwepo hata mtu mmoja aweze kuhisi upweke au kuachwa.

Kituo cha wakimbizi kimezaliwa kutokana na utambuzi kuwa sisi sote ni wana wa Mungu

Kufuatana ha hiyo Baba Mtakatifu Francisko ameweza kushirikishana nao uzoefu alio upata asubuhi yake alipotembelea  kambi ya wakimbizi huko Vrazhedebna na kwamba, ni  wakimbizi wa wanaotoka katika nchi mbali mbali duniani ili kutafuta maisha bora zaidi ya waliyoacha, hata kwa watu wa kujitolea. Katika kituo hicho ameambiwa kuwa kimeunda kutokana na kukutana na kuwa na utambuzi ya kuwa kila mtu ni mwana wa Mungu, bila kujali kabila au imani yoyote ya dini. Ili uweze kumpenda mtu hakuna haja ya kujua orodha ya matendo ya maisha yake. Upendo unaanza kwanza  pia na  kutangulia  mbele zaidi  kwa maana ni wa bure!  Kuona kwa macho ya imani, ndiyo wito wa kupita  juu ya vikwazo vingi vyenye kuleta migawanyiko na vigezo kama vile vya kufikiri ni nani wa kupendwa au hapana;  na badala yeke ni kutafuta hali halisi, ili kila mmoja aweze kuhisi kupendwa, hasa wale ambao wamewesahaulia na Mungu kwa maana wamesahuliwa na ndugu. Anayependa hapotezi muda wa kubaki na  kulia tu, lakini daima  anatafuta na kuona kitu cha kutenda kwa dhati kwa ajili ya wengine amesisitiza Baba Mtakatifu kwa waamini wakatoliki.

Tunahitaji kuondoka na  utamaduni wa kivumishi na kuingia katika ukweli

Baba Mtakatifu ametoa onyo kali ya kuwa makini kutokana na kuingia  utamaduni  wa vivumishi, yaani namna ya kuuliza huyo mtu  ni nani, na au namna gani mtu huyo, kwa maana Mungu hataki jambo hili. Huyo ni mtu na sura ya mfano wa  Mungu, kwa maana hiyo  hakuna kigezo kingine! amebainisha Baba Mtakatifu na kuongeza kusema "Tumwachie Mungu mwenyewe na sisi tuweke upendo kwa kila mtu. Lakini hiyo pia ni sawa na  kuacha masengenyo, kwa maana ni rahisi wengi kuangukia katika masengenyo, ya hapa na pale  japokuwa Baba Mtakatifu Francisko amethibitisha kuwa, hazungumzi juu yao kwa sababu ya kujua kuwa, pale hakuna masengenyo, bali ni kufikiria nafasi ambayo masengenyo hayo yanafayika. Ni lazima kuondoka na utamaduni wa vivumishi na kuingia katika hali halisi na ya kweli.

Akiendelea na historia ya wakimbizi Baba Mtakatifu anasema, katika kituo cha wakimbizi  wametambua kuona matatizo, kuyafahamu na kukabiliana nayo; wametambua kutafuta namna ya kung’amua na macho ya Bwana. Kama Mtakatifu Yohane alivyo kuwa akisema: Sijawahi kuona ugumu unaweza kutenda kitu kizuri zaidi”. Ugumu hauwezi kamwe kutenda wema na badala yake ni kuharibu kila kitu. Baba Mtakatifu amefikiria jambo akilini mtu mgumu anaweza kuwa namna gani, na hivyo akawaza  keki, kwamba mtu mbaya anaweza kumwaga siki juu ya keki na kuharibu kila kitu. Watu wagumu uharibu kila kitu,lakini  upendo unafungua daima milango na Papa Yohane  XXIII alikuwa anasema kweli. Sijawahi kuona ugumu unaweza kutenda kitu kizuri zaidi”. Bwana ni wa kwanza kutokuwa mgumu na kukata tamaa na daima anajaribu kufungua njia za ufufuko kwetu sisi wote. Ni jambo zuri zaidi iwapo Jumuiya zetu zinakuwa maeneo ya matumaini! Na mtu mwema mwanamke au  mwanamìume anayetafuta kuunda jumuiya ya matumaini.

Ili kuwa na matumaini kuna haja ya wengine

Baba Mtakatifu amesema ili kuweza kuwa na mtazamo wa Mungu tuna haja ya wengine, tuna haja ya wengine watufundishe kutazama na kuhisi jinsi Yesu anavyotazama na kuhisi; mioyo yetu iweze kudunda na hisia zake. Kwa maana hiyo inahitaji  ushuhuda  wa Mitko na Miroslava wakiwa na malaika wao Biluana aliyesema kuwa, katika parokia  yao imekuwa kama nyumba yao ya pili mahali ambao daima wanakusanyika pamoja, katika sala na msaada wa watu wapendwa na nguvu ya kwenda mbele. Parokia kwa namna hiyo inabadilisha kuwa nyumba kwa njia ya nyumba zote  hasa kuwa na uwezo wa kufanya Bwana aweze kuwapo mahali ambapo kila familia na kila mtu anatafuta kila siku mkate. Pale katika mikatisho ya barabara, Bwana anapatikana mahali ambapo hakutaka kutuokoa kupitia mikataba, badala yake alitaka kuingia kwa kina katika familia zetu na kutueleza kama wafuasi wake: “Amani kwenu”. Baba Mtakatifu Francisko amerudia kuhawahimiza maneno yake ambayo anapenda kuhimiza wanandoa kwamba wasiende  kulala usiku wakiwa wamekasirika hata usiku moja bila kuomba msamaha. Hii ndiyo njia ambayo inaweza kuwasaidia wakristo wote. Ni kweli kwamba katika maisha kuna hali ya kukasirika na kuwa na uchungu rohoni. Lakini lazima kusaidiana moja na mwingine ili kutozima moto wa Roho uliomo ndani mwetu. Kwa wanandoa anapenda kuwambia wasiope kugombane, lakini wakigombana hakuna shida kwa sababu ni kawadia kukasirika na kurusha sahani hewani, la muhimu isimalizike siku bila kuomba msamaha. Lakini hii ni kwasababu gani? Kwa sababu vita baridi ni hatari sana. Inahitaji ishara ya upendo amehimiza.

Baba Mtakatifu anapenda kuwahimiza ili pia awawe na shukrani kwa mapadre na masisita wao ambao wanawasaidia. Watu wa Mungu wanatambua kushukuru Mchungaji wao na kutambua kujifunza  kuwa waaminifu kwa wao na familia kwa njia yake. Iwapo padre au mtu aliyetiwa wakfu hata yeye kama askofu anakwenda mbali na Watu wa Mungu, moyo wake unakuwa wa baridi na kupoteza uwezo wa kuamini kama Watu wa Mungu. Kwa maana hiyo kama anavyopenda kusisitiza  Baba Mtakatifu amesema kuwa:  “watu wa Mungu wanasaidia wenye wakfu, yaani mapadre, maaskofu au watawa kuwa waamini”.

Jumuiya ambayo inasaidia, inasindikiza, inashirikisha na kutajirisha

Jumuiya ambayo inasaidia, inasindikiza, inashirikisha na kutajirisha, kamwe haitengenishi bali kuungana kwa kila mmoja na kujifunza kuwa ishara na baraka ya Mungu kwa wengine. Kuhani bila watu anapoteza utambulisho na watu bila kuwa na wachungaji wake haifai. Muungano wa mchungaji ambaye anasaidia na kupambana kwa ajili ya watu na watu wanasaidia kupambania wachangaji wao. Kila mmoja anajikamilisha  nafsi kwa ajili ya wengine. Na hakuna anayeweza kushi kwa ajili yake binafsi, kwa maana ni kuishi kwa ajili ya wengine. Na hii alikuwa anasema Mtakatifu Paulo kati ya barua zake anasema Baba Mtakatifu kwamba:. “ hakuna aishiye kwa ajili yake binafsi”. Akitoa mfano: ah padre mimi ninajua mtu anayeishi kivyake, je mtu huyo anayo furaha? Ana uwezo wa kutoa maisha kwa ajili ya wengine? Je anao uwezo wa kucheka na wengine?”  kwa hakika watu kama hawa ni wanafiki”, baba Mtakatifu amesema.

Kufuatana na hiyo ni watu makuhani na ambao wakiwa na kuhani wanauwezo wa kusema huu ni mwili wangu utolewao kwa ajili yenu . Na kwa kufanya hivyo ni kujifunza kuwa Kanisa ,familia na  jumuiya inayo karibisha, inasikiliza, inasindikiza, na kungaikia kwa ajili ya wengine, kwa kutoa majibu siyo yaliyo tayarishwa tayari kwenue mkoba, bali katika kutafuta pamoja njia ya mapatano; kutafuta namna ya kuonesha ufalme wa Mungu. Kanisa, familia na  jumuiya wanashikiria fundo mikononi mwake ya maisha na wakati mwingine inawezekana likawa kubwa  lakini wanalipokea na kulipenda! Kanisa ni mama. Mama Kanisa anaishi kwa ajili ya watoto wake na kushiriki matatizo ya watoto wake, kwa kuwapatia majibu yasiyo tayarishwa bado. Mama wengi wakitaka kujibu watoto wao katika hali halisi, wanatoa majibu yanayokuja moja kwa  moja ndani ya midomo yao. Mama wanajibu kwa moyo , yaani moyo wa umama. Ndivyo ilivyo hata Kanisa;  Kanisa ambalo limetengenezwa na sisi sote, watu, makuhani kwa pamoja na maaskofu watawa, kwa pamoja kutafuta njia za maisha, njia za mapatano na  kuonesha Ufalme wa Mungu ambao tayari upo.

Kufuata nyayo za Mtakatifu Syril na Methodius

Kuwa na nyumba zilizofunguliwa, kwa mujibu wa nyayo za Mtakatifu Cyril na Methodius, Baba Mtakatifu anasema, leo hii inatakiwa hata kuwa na ubunifu wa kujiuliza ni kwa namna gani ya kutafsri kwa namna ya dhati na kuelewa kuwa vijana, wengi wanahitaji msaada kwani mara nyingi hawapati majibu ya duku duku zao, mahitaji yao, matatizo yao na majeraha yao ( Christus vivit, 202 ) Kutokana na hiyo tunaombwa kuwa na  juhudi mpya za kutafakari katika matendo ya kichungaji ili kutafuta njia za kuweza kuwafikia rohoni mwao, kutambua matarajio yao  kuwatia moyo katika ndoto zao, kama jumuiya ya familia ambayo inawasaidia, inawasindikize na kuwaalika watazame mizizi ambayo imesimika matumaini.

Baba Mtakatifu amethibitisha kwamba, hatupaswi kuogopa kukabiliana na changamoto mpya, katika hali ambazo tunajitahidi kwa kila njia ili kuhakikisha kwamba watu wetu hawanyimwi ule mwanga na faraja inayotokana na urafiki na Yesu, wa jumuiya ya imani inayo wasaidia, ya upeo wa kila wakati unaovutia na kupyaishwa. Hata hivyo kwa kusisitiza juu ya vijana mara nyingi kupotea mizizi. Leo hii katika dunia yapo makundi mawili ya watu wanaoteseka sana yaani "Vijana" na "wazee". Lazima kukutana nao. Wazee ni mzizi ya jamii yetu , hatuwezi kuwafukuza nje ya jumuiya zetu, wao ni kumbu kumbu hai ya  imani yetu. Vijana wanahitaji mizizi na kumbu kumbu. Inabidi kufanya kila njia ili waweze kuwasiliana kati yao bila kuwa na hofu.

 Nabii Joeli alisema wazee wataota ndoto na vijana kutabiri

Katika kuhimiza zaidi, amekumbuka unabii  wa Joeli aliyetabiri kuwa “wazee wataota ndoto na vijana watatabiri”. Vijana wanapokutana na wazee na wazee na vijana , wanaanza kuishi kwa upya na kurudi kuota, wakati huo  huo vijana wanapata ujasiri kutoka kwa wazee na kwenda mbele na kwa maana hiyo Baba Mtakatifu anashuri kuwa, tuanze kufanya jambo hili muhimu katika maisha yao, kwa maana ya kuwafanya waanze wakati endelevu. Hizi ni ahadi ambazo leo hatupaswi kuwa na hofu hasa kutokuwa na hofu ya hali ambazo zinatujafanya tujitahidii kwa kila hali ili watu waweze kuwa na maana na maisha ( Evangelii gaudium, 49). Hatuna hofu kwamba kurasa nzuri za maisha ya Kanisa ziliandikwa wakati watu wa Mungu walikuwa wanaanza kujikita katika safari ya kutafuta upendo wa Mungu kila wakati katika  historia, katika changamoto ambazo taratibu walikuwa wakikutana nazo. Baba Mtakatifu Francisko amesema, ni vyema kujua kwamba wanaweza kuzingatia historia nzuri waliyo nayo,  lakini ni nzuri zaidi kuwa na dhamiri yao wenyewe ya kuwa wamepewa kuandika kile ambacho kitakuja.  Kurasa hizo hazijaandikwa bado, bali lazima waziandike wao. Wakati endelevu upo mikononi mwao , kitabu cha wakati ujao lazima wakiandike wao.

Wasichoke kwani Kanisa linaelendelea kuzaa japokuwa na vizingiti na uchungu

Baba Mtakatifu Francisko kwa kuhitimisha hotuba yake anawasihi wasichoke japokuwa, Kanisa linaendelea kuzaa hata katikati ya vizingiti, uchungu na umaskini, lakini ni Kanisa Mama ambalo haliishi  kuzaa  watoto wa rdhi hiyo, ambao wanahitaji leo hii katika mwanzo wa  karne ya XXI, kutega masikio katika  Injili na mengine katika moyo wa watu wao. Hata hivyo ameongeza kusema kuwa hajamaliza, kwa maana amewashukuru kwa mkutano huo na akifikiri Mtakatatifu  Yohane amependa kuwapa  baraka kwa kuptia maneno yake ya upendo wa Bwana. Yeye anasema alikuwa ametoa baraka akiwatakia matashi mema,na baraka inayo tambuliwa kuwa ya mwanga wa mwezi. Amewaomba wasali kwa mama Maria sura ya Kanisa kwa lugha yao.... salam Maria 

06 May 2019, 17:15