Tafuta

Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko amekutana na viongozi wakuu wa nchi na wanadiplomasia nchini Macedonia ya Kaskazini akiwa katika ziara yake Baba Mtakatifu Francisko amekutana na viongozi wakuu wa nchi na wanadiplomasia nchini Macedonia ya Kaskazini akiwa katika ziara yake 

Hija ya kitume:Kwa viongozi wa nchi wanahimizwa kufuata nyayo za Mt.Teresa!

Katika hotuba ya kwanza nchini Macedonia Kaskazini,Baba Mtakatifu Francisko amejikita kutazama utamaduni wa milenia ya nchi hiyo na zaidi kuwa na mfano wa utulivu wa kuishi kutokana na kutoa makaribisho ya wakimbizi na wahamiaji.Kwa wote anawakumbusha mfano wa kuigwa wa mwanamke aliyezaliwa katika mji wa Skopje Mtakatifu Teresa wa Calcutta!

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Tarehe 7  Mei 2019, Baba Mtakatifu Francisko akiwa katika hatua yake ya kwanza nchini Macedonia Kaskazini, ametoa hotoba yake hasa wa kujikita kutazama utamaduni wa kale wa nchi hiyo na kuona kuwa mfano wa kuigwa wa kushi kwa utulivu japokuwa na kuwa nawakimbizi na wahamiaji. Akiwa mbele ya viongozi wakuu wa serikali raia na wa kidoplimasia katika Ukumbi wa Rais  huko Skopje  kwanza akimshukuru Rais wa nchi kwa maneno ya hotuba  yake na kwa mwaliko wake wa kuweza kutembelea Macedonia Kaskazini, pia hata  kumshukuru hata waziri Mkuu wa nchi. Anawashukuru wawakilishi wa jumumuiya za dini  nchini huo waliokuwapo hata jumuiya  katoliki, ikiwakilishwa na askofu wa  Skopje wa upatriaki wa Mwenye heri Bikira Maria mpalizwa huko Strumica-Skopje, ambayo ni sehemu hai katika shughuli zao za kitume kwa kushirikiana na  furaha na wasiwasi wa kila siku kwa watu wao.

Ni kwa mara ya kwanza mfuasi wa Mtakatifu Petro anakwenda Jamhuri ya Macedonia

Baba Mtakatifu Francisko, anabainisha kwamba ni kwa mara ya kwanza mfuasi wa Petro anakwenda katika Jamhuri ya Macedonia, hivyo anayo furaha ya kupyaisha nao miaka 25 tangu waanze kuwa na  mahusiano ya kidiplomasia na Vatican na ambapo wameweza kuwa na makao yao mara tu baada ya kupata uhuru kunako Septemba 1991. Ardhi yao ni kama daraja kati ya Mashariki na magharibi na ncha ya kuwa na aina nyingi za utamaduni ambao ndiyo unajionesha katika tabia ya kanda hiyo amesema Baba Mtakatifu Francisko. Kwa ushuhudauliopitia  utamaduni wa kibizantini na Ottomani;  kwa ukame wa nguvu kati ya milima na picha zuri za kizamani katika Makanisa, zinazoonesha uwepo wa kikristo tangu mwanzo wa utume; kwa kuonesha wingi  na utamaduni wa milenia ya utamaduni ambao wao wanaishi!

Baba Mtakatifu Francisko amesema kuwa, utajiri wa utamaduni ni kioo cha tunu msingi ambayp inafaa kurithiwa  katika muungano wa tamaduni nyingi na dini nyingi ambazo zinatazama uso wa watu wao. Pia  ni tunda la historiatrajiri, kwa sababu ya uhusiano ambao umekuwapo kwa karne nyingi. Aida akigusia juu ya  utofauti iliopo wa kidini kama vile waorthodox, waislam, wakatoliki, wayahudi na waprotestanti, na wakati huo huo wingi wa makabila kati ya Macedonia, Albania, Serbia, Croatia na watu wengine wa dini nyingine wamwezea kwa dhati kutengeneza picha nzuri sana na ambayo inasiliza kuendeleza uasili, ukiwa ni uzuri wa aina ya peke ya umoja. Hata hivyo anasisitiza kwamba ni uzuri ambao utatakiwa kuangazwa katika kipimo ambacho watatambua kukionesha na kukoanda katika mioyo ya kizazi.

Jitihada nyingi zinazo fanyika ili kila dini na utofauti wa kabila uweze kupata ardhi inayotarajiwa

Baba Mtakatifu anasema, kwamba jitihada nyingi zinazofanyika, ili kila dini na utofauti wa kabila iweze kupata ardhi inayo tarajiwa katika umoja kwa kuheshimu hadhi ya kila mtu na matokeo ya kuhakikisha uhuru msingi, ni mambo ambayo hayatakuwa ya bure, badala yake yatakuwa ni ya lazima kuyapanda na kuyaendeleza kwa ajili ya wakati endelevu wa amani na mafanikio. Hata hivyo Baba Mtakatifu Francisko, amependa kuonesha shukrani za juhudi zilizotimizwa na Jamhuri hiyo, ikiwa pia kwa viongozi wa mikoa katika kutoa mchango mkubwa wa mashirika ya kimataifa,Msalaba Mwekundu, Caritas na baadhi ya Mashirika mengine yasiyo ya kiserikali, ambao wameweza kutoa msada kwa wahamiaji na wakimbizi kutoka katika nchi tofauti za Mashariki.

Wakimbizi wanakimbia vita au hali mbaya ya umasikini wa kukithiri

Hawa wanakimbia vita au hali mbaya ya umasikini wa kukithiri  a zaidi kutokana na matukio ya silaha  na mwaka 2015-2016 waliweza kufika katika mipaka yao, wakitaka kuaeleka Kaskazini ya Ulya na wakapata mahali pa kukumbilia. Baba Mtakatifu amesema, utayari wa mshikamano uliotolewa, uliwasaidia wao walikuwa wamepoteza wapendwa wao wengi zaidi ya nyumba, kazi na nchi zao. Hii ni heshima ya kuzungumza ndani ya mioyo yao kwa kutambua namna ya kujinyima, kutambua mshikamano na ushirikishana mali kama njia ya kila maendeleo ya dhati. Baba Mtakatifu anawataka waendelea kuwa na mshikamano huo kama tunu msingi ya dharura, kwa njia ya watu wa kujitolea katika utoaji wa huduma kwa wale wenye kuhitaji.

Aidha Baba Mtakatifu amependa kutoa shukrani maalum kwa mmoja wa mwanachi mwenye sifa nzuru duniani ambaye aliongozwa na upendo wa Mungu, alifanya upendo kwa wengine kama sheria kuu ya kuwepo kwake na ambapo akaweza kujikita kwa nguvu zote katika huduma ya waliotengwa, waliokataliwa, walio masikini zaidi. “ Ninaelezea wazi kwa mtu ambaye anajulikana kama Mama Teresa wa Calcutta” Baba Mtakatifu amesema. Yeye alizaliwa katika kitongoji cha Skopje mwaka 1910 kwa jina la Anjezë Gonxha Bojaxhiu na alifanya utume wake, kwa unyenyekevu na kujitoa moja kwa moja katika nchini India na kwa njia ya watawa wenzake aliweza kufika katika mipaka mbalimbali ya kijiografia ya uwepo wa watu. Baba Mtakatifu amesema:“Ninayo furaha kubwa kwamba muda si mrefu nitakwenda kusimama kidogo kwa sala mahali kuna jengo la kumbukumbu, katika Kanisa la Moyo Mtakatifu wa Yesu alipozaliwa. Hata hivyo na  wao wanayo furaha kubwa kwa ajili yake mtawa hiyo na hivyo mewashauri waendelee kufanya kazi katika jitihada za kujitolea na matumaini ili watoto wa ardhi hiyo waweze kuiga mifano yake, kugundua na kufikia ukomavu wa wito ambao Mungu ameota kwa ajili yao.

Uhusiano wa kidiplomasia wa nchi ya Macedonia na Vatican

Baba Mtakatifu pia amethibitisha kwamba, tangu nchi ya Macedonia ipate uhuru wake Vatican imeweza kuwasindikiza kwa umakini hatua kwa hatua kwa hatua  ili nchi  iweze kuendelea katika mazungumzo na uelewa kati ya viongozi wa raia na madhehebu ya dini. Mungu awajalie uwezo wa kuonesha kwa watu ukaribu huo na hata kushukuru kwa ziara ya kila mwaka ambapo wawajilishi maalum wanafika mjini Vatican, wakati wa fursa ya watakatifu  Cyril na Metodi. Baba Mtakatifu anawatia moyo ili waendelee katika kufanya nchi yao iwe ya amani, makaribisho na ushiurikishwaji kati ya tamaduni, dini na watu . Kuanzia kila mmoja utambulisho wake na utamaduni wa maisha yao, uraia  wao unaweza kwa namna nyingine kujenga wakati wao wa pamoja kwa kufungua utajiri ambao kila mmoja anakuwa ni mchukuzi wa amani!

07 May 2019, 12:30