Tafuta

Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko amekutana mini Vatican na wanafunzi elfu tano wa mkoa wa Lazio na Abruzzo wakiwa pamoja na mabingwa wa mpira wa miguu Baba Mtakatifu Francisko amekutana mini Vatican na wanafunzi elfu tano wa mkoa wa Lazio na Abruzzo wakiwa pamoja na mabingwa wa mpira wa miguu  (ANSA)

Baba Mtakatifu:Mpira wa miguu ubaki kuwa mchezi,ni kwaajili ya wema wa kichwa na moyo!

Baba Mtakatifu Francisko amekutana na wanafunzi elfu tano wa Mkoa wa Lazio na Abruzzo,pamoja na mabingwa na makocha wao waliounganika katika tukio la"mpira tunaoupenda".Mpira unatakiwa uwe chombo cha kushirikishana urafiki hata katika majaribu,lakini kwa kile ambacho maoni ya umma wanasema ni mchezo mzuri zaidi duniani.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Baba Mtakatifu Francisko anashukuru Rais  wa Shirikisho Chama cha Mpira  wa miguu Italia kwa maneno yake, alipokuana na washiriki wa Mkutano unaoongozwa na mada “ Mpira tunao upenda” ambapo walikuwa ni wanafunzi elfu tano kutoka Mko wa Lazio na Abruzzo wakiwa pamoja na mabingwa wa mpira, katika fursa Mkutano ulioandaliwa na Gazeti la Michezo na Shirikisho la Mchezo wa Mpira Italia waliokutana na Baba Mtakatifu  tarehe 24 Mei 2019 katika ukumbi wa Paulo VI Vatican. Baba Mtakatifu Francisko katika hotuba yake anasema mchezo ni fursa kubwa ya kujifunza kuwa bora zaidi, kwa sadaka na jitihada lakini zaidi ya hayo bila kuwa peke yako. Inaonesha wazi katika kipindi ambacho kinatawaliwa na wimbi la teknolojia ni rahisi kujibagua lakini pia kujenga mahusiano ambayo ni tofauti kwasababu yako mbali sana na hali halisi.

Ni vizuri kucheza mpira na wengine katika uwanja wa michezo

Baba Mtakatifu amebainisha kwamba ni vizuri kucheza mpira na kuucheza na wengine katika uwanja wa michezo, kujifunza kujenga matendo ya dhati ya mchezo na kama timu ya pamoja. Mpira unageuka kuwa chombo kuwathibitisha watu halisi na kushirikishana urafiki nvilevile kuwa na  fursa ya  kutazamana uso kwa uso, kuchangamotishwa na kujiweka katika majaribu  ya uwezo binafsi. Vile vile amebainsha kuwa, mchezo wa mpira ni wa timu na ambao siyo rahisi kucheza na kuwa peke yako!  Na iwapo unafanyiwa uzoefu huo, inawezekana kabisa kuwa mwema hata kichwa na moyo katika jamii ambayo inazidi kuangaikia na kuweka kitovu cha umimi utafikiri ndiyo msingi pekee…

Maoni ya umma ni kwamba mpira wa miguu ndiyo mchezo mzuri zaidi duniani

Baba Mtakatifu Francisko aidha amesema kuwa, wengi wanathibitisha katika maoni ya umma kwamba, mpira wa miguu ndiyo mchezo mzuri zaidi duniani. Na mara nyingi inasikika sauti zao wanasema:"hakuna kilicho kizuri zaidi ya mpira wa miguu". Lakini kwa bahati mbaya Baba Mtakatifu amebainisha kwamba: tunaona hata katika mchezo wa mpira wa vijana katika viwanja au nje ya viwanja matukio ambayo yanaweka madoa katika uzuri wake. Kwa mfano inaonesha baadhi ya wazazi ambao wanakuwa washibiki kuzidi kiasi au wakuu au makocha… Na kumbe kucheza kunawezesha kuwa na furaha kwa sababu unaweza kuelezea uhuru wako, kushindana kwa njia ya kujifurahisha, unakaa kwa kujifurahia katika muda wako tu,  kwa sababu unapenda, unatekeleza ndoto bila, hata ulazima wa kuwa bingwa. Hata  katika Mkataba wa Haki za Watoto unathibitisha kuwa "Michezo ni haki ya kila mtoto na siyo kuwa bingwa (art 10)".

Wazazi na watu wazima waoneshe watoto wao dhana nzuri ya mchezo

Baba Mtakatifu anawashauri watu wazima/wazazi  na walimu wao kuonesha kwa watoto dhana hii kwamba mchezo ni kujitoa bure na ushirikishwaji. Wawatie moyo wakati mgumu, hasa baada ya kushindwa… wawasaidie kuelewa kuwa hata kupewa adhabu au kwenda kukaa siyo kunyenyekeshwa  bali ni fursa ya kukua na fursa ya mwingine. Na ili waweze kuwa na ladha daima ya kujitoa kwa kadili ya uwezo wao kwa sababu zaidi ya mchezo yapo maisha ambayo yanawasubiri hapo baadaye. Akifoa mfano amesema: Mmoja alisema alikuwa anatembelea ncha ya miguu uwanjani  na ili asikanyake ndoto  takatifu za watoto. Anawaomba wasibadilishe ndoto za vijana kwa kuwakatisha tamaa haraka kwa vikwazo vya hali halisi. Wasisonge maisha na mifano ya kutisha kwa kuwanyima uhuru na kuwajazandoto kama za abunuasi; wasiwafundishe njia za mikato ambazo zinapelekea kupotea katika njia isiyo na mahali pa kutokae katika maisha!

Mabingwa wawasaidie vijana na wasisahau waliko anzia

Hatimaye Baba Mtakatifu amewalenga mabigwa wakuu wa mchezo ambao kwa wengi wa viijana wanaiga mfano. Wasisahau mahali walipoanzia. Katika uwanja wa pembenzoni, katika makutano na vijana wenzao katika jamii ndogo… anawatakia matashi mema wawe daima na shukrani ya kukumbuka historia yao kwa njia ya sadaka, ushindi na kushindaw. Wahisi kuwa wawajibikaji wa elimu, wawasaidie kuwa na mtazamo mwema wa maisha na mshikamano na wale walio wadhaifu, kwa kuwatima moyo vijana, na  walio wakubwa wawe wakubwa ndani hasa ukomavu labda hata kuwa mabingwa wa maisha!

24 May 2019, 13:54