Tafuta

Baba Mtakatifu Francisko amekutana na washiriki wa Mkutano wa kimataifa wa 'Yes to life' mjini Vatican na kusisitiza kuwa maisha daima ni matakatifu,lazima kuyalinda! Baba Mtakatifu Francisko amekutana na washiriki wa Mkutano wa kimataifa wa 'Yes to life' mjini Vatican na kusisitiza kuwa maisha daima ni matakatifu,lazima kuyalinda! 

Baba Mtakatifu:Maisha ya binadamu ni matakatifu na siyo kufanya utafiti kwa ajili ya kutoa mimba!

Baba Mtakatifu akipokea washiriki wa Mkutano unaoongzwa na“Yes to life":utunzaji wa thamani ya zawadi ya maisha katika hali ya udhaifu,amewashauri wasindikize familia ikiwa ni katika kujiandaa na maombolezo ya mtoto pia katika utunzaji wa mtoto aliye mgonjwa.Jitihada hizo amesisitiza ni katika kutimiza upendo wa familia.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Baba Mtakatifu Francisko amekutana na washiriki wa Mkutano ambao umeandaliwa na Baraza la Kipapa la Walei, Familia na maisha kwa ushirikiano na Chama kimoja kiitwacho "Moyo ndani ya Tone”,  kwa kuongozwa na tema ya "Yes to life: utunzaji wa thamani ya zawadi ya maisha katika hali ya udhaifu”.  Mkutano wa Yes to Life, ulifunguliwa tarehe 22 Mei 2019 na ambao ni mkutano wa kimataifa kuhusu madawa ya watoto  na usindikizwaji kichungaji wa familia ambazo zinasubiri kuzaliwa watoto wenye udhaifu. Lengo la Mkutano huo ni kutaka kutoa kipindi mwafaka cha mafunzo na maelezo ya kisayansi na kichungaji ili kukuza utamaduni wa dhati wa kupokea maisha yanayo zaliwa katika  hali yoyote ile hata isiyo ya kawaida, hususani mtoto mgonjwa au mlemavu. Mkutano huo umeudhuriwa karibu na watu 400 kati yao wakiwemo madaktari, wauguzi, madaktari bingwa wa masuala ya uzazi, vinasaba, elimu viumbe na wawakilishi wengine walei na watu wa dini kutoka katika mabaraza ya maaskofu 70 duniani ili kukabiliana na mada nyeti  juu ya utetezi wa maisha ya binadamu yanayo zaliwa katika hali halisi ya udhaifu!

Watoto ambao kwa kesi nyingine wanaishia katika utamaduni wa ubaguzi

Baba Mtakatifu akianza hotuba yake amewashukuru kufika kwao na salam kwa Kardinali Farrell, Rais wa Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha kwa hotuba yake utangulizi. Anawasalimia washiriki wote wa mkutano wa  kimataifa wa Yes to life! utunzaji wa thamani ya zawadi ya maisha katika hali ya udhaifu”. Aidha anathibitisha kuwa suala hili ni moja ya hali halisi inayotendwa kila siku kwa ajili ya kupokea maisha ya watoto wanaozaliwa katika hali ngumu ya udhaifu. Watoto ambao kwa kesi nyingine, wanaishia katika utamaduni wa ubaguzi ambao hauendani na maisha. Lakini anasisitiza kuwa  hakuna mwanadamu yeyote anayeweza kuingilia kamwe na maisha, wala umri wake, wala hali yake ya afya, wala ubora wa kuwepo kwake. Kila mtoto anayetungwa katika umbu la mwanamke ni zawadi na ambaye anabadilisha historia ya familia nzima kuanzia kwa baba na mama, babu na bibi na ndugu zake wote. Na mtoto huyo anahitaji kupokelewa, kupendwa na kutunzwa. Daima!  Baba Mtakatifu akisikia sauti ya mtoto aliyekuwa analia ukumbi wa mkutano ametoa mfano kwamba, "hata kama wanalia kama huyo... Labda mwingine anaweza kufikiria ni kelele, hapana, tuwe naye  ni muziki ambao wote sisi tunapaswa kuusilikiza". Aidha ameongeza kusema: "Nina uhakika amesikia makofi na ametambua kuwa wote wameweza kumsikiliza".

Lazima kusikiliza watoto hata kama wanasumbua

Lazima kusikiliza daima hata mtoto ambaye anasumbua; hata katika Kanisa watoto wengi wanalia Kanisani, hao wanamsifu Mungu. Kamwe hakuna kumfukuza mtoto anayelia. Asante kwa ushuhuda huo”. Baba Mtakatifu amesisitiza hilo . Akiendelea juu ya masuala ya mimba, Baba Mtakatifu amesema, Mwanamke anapogundua kuwa anasubiri mtoto, mara mmoja anahisi maana kuu ya fumbo la kina. Kwa utambuzi wa uwepo wake, anyekuwa tumbuni kwake, anafanana kuhisi kuwa siyo tena yeye peke yake bali kuwa mama. Kati yake na mtoto wanajenga ule uhusiano wa kweli wa kuelewana kati ya wanadamu ambao wanawasiliana  kati yao tangu kutungwa mimba na kuendelea kukuza uhusiano wao kwa dhati, lakini zaidi mtoto  katika nafsi yake anajaribu kutoa ujumbe ili kuonesha uwepo wake na mahitaji ya mama yake. Na ndiyo hivyo kiumbe binadamu kinageuka kuwa mtoto, kwa kumfanya mwanamke awe kweli mwanamke na mwenye kuwa na subira na mwanae.

Utaalam wa kisasa  unagundua kasoro kuanzia majuma hata ya kwanza

Baba Mtakatifu amebainisha kwamba katika utaalam  wa kisasa wa uzazi, wanao uwezo wa kugundua tangu majuma ya kwanza uwepo wa kasoro na matatizo na wakati mwingine wanaweza kuweka hatari ya maisha ya mtoto na kuondoa utulivu wa mwanamke. Ugunduzi wa kasoro ndogo na ambayo bado hakuna uhakika wa ugonjwa, unabadili maisha ya mwenye mimba na kufanya familia iwe na mahangaiko ya kina na kukata tamaa. Hiyo ni kutokana na ukosefu wa uwezo, hofu ya kuteseka mtoto na familia mzima katika kilio cha ukimya. Kwa maana hiyo wanahitaji msaada katika giza la ugonjwa na ambapo hakuna anayetambua hatima ya uhakika. Na hiyo pia ni kutokana na kwamba mapinduzi ya kila ugonjwa daima ni kitu ambacho hata madaktari mara nyingi hawajuhi na kuweza kuonesha kwa kila kesi ya ugonjwa huo.

Upo uwezekano wa kuwasindikiza wenye matatizo na udhaifu wakati wa ujauzito

Licha ya hayo Baba Mtakatifu Francisko amebainisha kwamba kuna jambo moja la madawa ambalo linatambua na hasa watoto tangu tumboni mwa mama, ikiwa wanaonesha hali ya udhaifu, ni wagonjwa, au  wadogo ambao hawawezi kutibiwa kwa njia ya madawa, operesheni kwa  kuwasaidia au kuwa na uwezo wa kupunguza maumivu ya hali ngumu. Uwezekano huo na uwelewa huo,  unaweza kuwekwa  katika mchakato kwa wote na ili kuweza kuendelea katika hali hii ya kisayansi na kichungaji katika kusindikizwa na wataalam. Kwa njia hiyo ni muhimu kwamba madaktari wanapaswa kuwa na uwezo, si kwa lengo la kuponyesha tu, lakini kwa ajili ya thamani takatifu ya maisha ya binadamu ambayo lengo lake ni  kulinda na ndiyo linabaki tendo mwafaka na la mwisho kwa madaktari.

Taaluma ya udaktari ni utume na wito wa maisha:Madaktari ni zawadi kwa ajili ya familia

Taaluma ya udaktari ni utume na wito wa maisha ambao ni muhimu Baba Mtakatifu Franciko anasisitiza kwamba madaktari wawe na utambuzi kuwa wao ni zawadi kwa ajili ya familia ambazo wamekabidhiwa. Madaktari wenye uwezo wa kutengeneza uhusiano na kubeba maisha ya wengine kwa kukabiliana na uchungu, kuwa na uwezo wa kutuliza na kusindikiza katika kutafuta suluhisho kulingana na hadhi ya kila maisha ya binadamu. Ni kwa sababu hiyo faraja ya kujifungua kwa wazazi ni moja ya mtindo wa kuweza kuitunza na ambao ni wa kibinadamu, kwa sababu unakuza uhusiano na uwajibikaji na mtoto mgojwa ambaye anasindikizwa na wahudumu na familia yake katika mchakato mzima wa kushirikishwa na ambao siyo wa kumwacha kamwe peke yake bali  kumfanya ahisi joto la kibinadamu na upendo.

25 May 2019, 14:56