Tafuta

Vatican News
Tarehe 10 Mei 2019 Baba Mtakatifu Francisko amekutana mjini Vatican na washiriki wa mkutano mkuu wa mwaka wa Mama wakuu wa mashirika ya kitawa kutoka duniani kote Tarehe 10 Mei 2019 Baba Mtakatifu Francisko amekutana mjini Vatican na washiriki wa mkutano mkuu wa mwaka wa Mama wakuu wa mashirika ya kitawa kutoka duniani kote  (Vatican Media)

Baba Mtakatifu kwa wakuu wa mashirika:Utume ni huduma na siyo utumwa!

Baba Mtakatifu,wakati wa kukutana na wakuu wa mashirika ya kitawa ya wanawake kutoka duniani kote tarehe 10 Mei 2019 mjini Vatican,amegusia masuala ya nafasi ya wanawake katika Kanisa,ushemasi,manyanyaso,uwezekano wa ziara ya kitume Sudan Kusini.Wakati huo huo hotuba aliyowakabidhi anakazia suala la kuwa ladha ya chumvi duniani na Neno.

Na Sr. Angela Rwezaula -Vatican

Baba Mtakatifu Francisko wakati wa kukutana na washiriki wa mkutano mkuu wa XXI wa mwaka wa Umoja wa Kimataifa wa Mama Wakuu wa Mashirika (Uisg) amejikita kuzungumzia baadhi ya mada mbalimbali bila kusoma na  hotuba kuikabidhi ili wapate kujisomea wao wenyewe katika mashirika yao, lakini wakati wa kuzungumza kwa ulahisi amegusia masuala ya nafasi ya  wanawake katika Kanisa, suala la ushemasi, manyanyaso,  uwezekano wa ziara ya kitume nchini  Sudan  ya Kusini na mengineyo. Hata hivyo katika suala la manyanyaso amesema kuwa  ni tatizo ambalo haliwezekani kutatuliwa kwa siku moja tu na kwamba mchakato wa kutafuta suluhisho la tatizo hilo bado unaendelea na wanalitambua suala hilo, kwa aibu kubwa lakini aibu yenye kubarikiwa.

Tatizo la manyanyaso haliwezi kutatuliwa wa suluhisho la Kanisa kwa siku moja na nyingine. Mchakato umeanza. Jana Hati nyingine imetolewa na kwa taratibu tunajaribu kufanya mchakato kwa sababu ni jambo ambalo tangu miaka 20 hadi sasa hatukuwa na utumbuzi na tupo tunaatambua sasa, kwa aibu kubwa lakini yenye kubarikiwa.

Ukiukwaji wa madaraka

Aidha Baba Mtakatif akiendelea na mazungumzo na watawa hawa amesema kuwa, unyanyasaji kwa watawa ni tatizo kubwa. Na tatizo kubwa lipo  hata matumizi mabaya ya madaraka, matumizi mabaya ya dhamiri. Baba Mtakatifu amesisitiza, kwa namna ya pekee, watawa wa kike hawapaswi kuwa wajakazi wa nyumba za makuhani. Bali wanapaswa kutekeleza utume wao katika hali ya huduma, na siyo katika ile ya utumwa.

 "Siyo tu unyanyasaji wa kijinsia kwa watawa bali pia matumizi mabaya ya madaraka, matumizi mabaya ya dhamiri. Lazima tupambane dhidi ya hili. Akigusia juu yahuduma ya watawa amesema:tafadhali, huduma ndiyo, utumwa, hapana!.

Ushemasi wa wanawake

Kuhusiana na suala la ushemasi wa kike, Baba Mtakatifu Francisko amekumbusha kuwa, Tume imekabiliana kwa kina tema hiyo. Katika Hati ya Sakramenti”, lakini inahitaji msingi wa kitaalimungu na kihistoria. Katika shughuli hiyo  Kanisa litaendelea mbele. amethibitisha. Lakini iumbukwe hivi karibuni akiwa anamjibi mwandishi wa habari kuhusu suala hili wakati wakati wa mkutano wao wakiwa wanatoka  nchini Macedonia Kaskazini  tarehe 7 Mei 2019, Baba Mtakatifu alisema tume inaendelea na mchakato na hawajafikia tamati na makubaliano ya pamoja, hadi wafikie mwisho wa utafiti ndipo itatolewa jibu gani sahihi la kufanya, lakini kwa sasa bado wamesimama katika kujifunza  zaidi na utafiti.

Kanisa ni mwanamke  na uwezekano wa kutembelea Sudan Kusini

Ni makosa kufikiria kuwa shughuli ya watawa katika Kanisa ni dhamana ya Kanisa na haina maana. Kanisa ni mwanamke hii siyo sura, bali ni hali halisi. Katika Biblia, amekumbusha Baba Mtakatifu kuwa, Kanisa ni mchumba, mchumba wa Yesu. Hata juu ya taalimungu ya wanawake amesisitiza kuwa, lazima iendelee mbele. Aidha  akijibu juu ya swali la mkuu wa shirika wa Sudan ya kusini amesema inawezekana mwishoni mwa  mwaka huu  kwenda. Lakini hii siyo ahadi japokuwa  upo uwezekano katika  fursa labda wakati wa ziara ya kitume nchini Msumbiji, Madagascar na Mauritius. Na ameongeza kusema:“Ninataka kwenda Sudan Kusini kwa maana Sudan ipo rohoni mwangu”.

Hakuna Pasaka bila mateso

Katika hotuba yake aliyo wakabidhi Baba Mtakatifu Francisko amesisitiza kuwa hakuna hata mmoja wa kuwaibia upendo wa kuinjilisha. Hakuna Pasaka bila kuwa na utume wa kutangaza Injili kwa wote. Kwa maana hiyo  Baba Mtakatifu Francisko ametaka kupyaisha wito wake ya kwamba, wasiwe na hofu ya kuwa wachache.  Mbele ya kupungua kwa idadi ya watawa, kwa namna ya pekee wa kike, kuna kishawishi cha kukata tamaa, kataka  kijikabidhi au kujifungia na “kasumba ya kusema tulizoea kufanya hivi”. Kwa mantiki hiyo, Baba Mtakatifu Francisko amerudia kutoa wito wa nguvu kama alivyokuwa amekwisha sema wakati mwingine kuwa, badala yake wawe na hofu ya kutokuwa na maana, kutoonesha mwanga ambao una uwezo kuwangazia wale wote waliolala katika usiku wa giza la kihistoria. Vile vile katika hotuba yake aliyo wakabidhi inasema, wajihadhali ili wasiangukie katika vishawishi wa kujitosheleza na kubadilika kuwa majeshi yaliyo fungwa. Badala yake wanapaswa kukuza mawazo zaidi ya upendo, kwa kuishi na uaminifu wa ubunifu katika karama zao.

Wasiwasi wa migogoro ya kizazi kipya kama hawapeleki ndoto za wazee 

Wasiwasi wa migogoro ya kizazi kipya unajionesha katika hotuba yake hasa anaposema kwamba: ikiwa vijana hawana uwezo wa kupeleka mbele ndoto za wazee na kuzifanya zizae matunda, na wazee wanapokosa kukaribisha kwa ukarimu unabii wa vijana (Joeli 2,28). “Ni kwa jinsi gani napenda kurudia haya, " vijana wanakimbia haraka, lakini wazee wanaelewa mwendo”. Katika jumuiya yoyote ile  kuna ulazima wa kuwa na hekima ya wazee, lakini ambayo ipate kuigwa na nguvu ya vijana….. Hata hivyo kwa niaba yao anawashukuru watawa wote katika taasisi mbalimbali kwa kazi kubwa wanayojikita nayo katika maeneo mengi ya pembezoni wanapoishi. Pembezoni ya elimu, mahali ambapo kuelimisha ni kushinda, ni kushinda kwa ajili ya Mungu; pembezoni mwa utakatifu, mahali ambapo wao ni wahudumu wa ujumbe wa maisha, wa maisha ya hadhi: na pembezoni mwa kazi ya kichungaji katika maonesho mengi ya shughuli hizo kwa kutoa ushuhuda wa maisha yao na Injili ambayo wanaonesha uso wa mama Kanisa. "Asante kwa kile ambacho ninyi mnafanya katika Kanisa. Msiache kamwe kuwa wanawake. Inahitajika kuonesha kuwa ni wanawake" (rej. nguvu ya wito n,111).

Jipyaisheni mara kwa mara katika kukutana na Yesu Kristo mfufuka

Baba Mtakatifu Francisko anawataka wajipyaishe mara kwa mara katika kukutana na Yesu Kristo mfufuka na kwa kufanya hivyo wataweza kuwa mashuhuda wake, kwa kuwapelekea wanaume na wanawake wapendwa wa Bwana kwa namna ya pekee wale ambao wanahisi ni waathirika wa utamaduni wa kibaguzi, ukarimu na faraja ya furaha ya Injili. Maisha ya wakfu kama vile alivyo sema  Mtakatifu Yohane Paulo II na kama ilivyo kwa hali halisi ya yoyote ya Kanisa, katika unyeti wake na ugumu wake, (rej. Wosia wa Kitume wa maisha ya watawa ya Mtakatifu Yohane  Paulo II, n. 13). Baba Mtakatifu Francisko anawahimiza wawe kama chumvi inayotoa ladha ya maisha kwa watu wa jamii. Kufanya kazi bila kuchoka ili wawe  walinzi waingojea asubuhi (rej Is 21, 11-12); ili wawe chachu mahali ambapo wanaishi na kwa kwa kile ambacho wanaishi (rej. Wosia wa KitumeEvangelii gaudium, n. 210). Kuna watu wengi wenye kuhitaji wao na wanasubiri, anasema Baba Mtakatifu!

Kuna watu ambao wanahitaji tabasamu ya rafiki na kuwapa matumaini; mikono yao iweze kuwasaidia katika safari yao; maneno yao yapande matumaini katika mioyo yao; upendo wao kwa mfano wa Yesu ( soma Yh 13, 1-15), uweze kuhudumia majeraha ya kina yanayo sababishwa na upweke na kubaguliwa. Wawe na uwezo wa kuchunguza kwa mara nyingine tena karama zao na kuingia ndani katika mizizi na kuishi katika wakati uliopo  bila kuwa na hofu ya kutembea, wala kuzuia maji yasiweze kutiririka. Maisha ya kitawa ni kama maji: iwapo yametuhama yanachafuka sana. Kwa namna hiyo bila kupoteza kumbu kumbu; ni lazima kuishi wakati uliopo kwa shauku, kwa maana ya kufanya hivyo wataweza kuzuia kukarabati zile itikadi na kila aina ya mawazo mabaya  katika maisha ya kitawa na  katika Kanisa kwa ujumla

Mkutano Mkuu wa XXI wa mwaka  wa  Uisg

Mkutano wa XXI wa Mwaka wa Umoja wa Kimataifa wa Wamama wakuu UISG( Unione Internazionale Superiore Generali (Uisg) ulianza mjini Roma tarehe 6 hadi  10 Mei2019  wakiongozwa na mada  “mpanzi wa matumaini kinabii”. Katika mkutano  huo ulio hitimishwa, ni wameshiriki watawa 850  mama wakuu wa mashirika  kutoka nchi 80 dunia kote. Hata hivyo ulikuwa ni mkutano wa Wakuu wa mashirika ya Kitawa ya wanawake ambayo yameidhishwa kisheria. Ni mkutano mkuu wa kuweza kushirikishana uzoefu na kubadilisha habari mbalimbali. Kwa sasa shirikisho hilo linaundwa na  wajumbe 1900, kutoka zaidi ya nchi 100 na wawakilishi zaidi ya watawa  450,000. Kati ya tema zilizo kabiliwa ni ile ya utamadunisho, wakati endelevu wa maisha ya kitawa, ushirikishwaji wa nyumba yetu ya pamoja unao zungumzwa na Baba Mtakatifu katika  Wosia wa “Laudato Si”na  mazungumzo ya kidini.

/content/dam/vaticannews/pam/audio/agenzie/netia/2019/05/13/10/wakuu-wa-mashirika-uisg-135020077.mp3
11 May 2019, 10:08