Tafuta

Vatican News
Baba Mtakatifu wakati wa sala ya Malkia wa  Mbingu tarehe 12 Mei 2019 Baba Mtakatifu wakati wa sala ya Malkia wa Mbingu tarehe 12 Mei 2019  (ANSA)

Baba Mtakatifu:Kusikiliza sauti ya Mungu ili kuondokana na njia potofu na ubinafsi!

Wakati wa sala ya Malkia wa Mbingu Baba Mtakatifu amekumbuka wakina mama wote kuwa ni walinzi wa thamani ya familia.Amesali kwa mara nyingine tena kwa ajili ya mapadre,watawa na kwa waamini anawashauri wasikilize sauti ya Mungu inayo sadia kuondokana na njia potofu na tabia za ubinafsi.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Baba Mtakatifu akiwa katika dirisha la Jumba la kitume wakati wa tafakari yake katika Sala ya Malkia wa Mbingu tarehe 12 Mei 2019 amesisitiza juu ya siku ya 56 ya Sala ya Kuombea Miito duniani na  kuzama ujasiri wa kuthubutu kwa ajili ya ahadi ya Mungu. Baba Mtakatifu amesema, kufuata Yesu daima ni hatari, lakini inahitaji ujasiri anashuhuda amesema hayo akiwa anasindikizwa  ubavuni mwake na mapadre wawili wawakilishi kati  ya 19 ambao muda mfupi alimaliza kuwapa Daraja Takatifu la Upadre katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro na Baraka yake!

Ni wangapi Bwana anaendelea kuwaita kama alivyo fanya kwa mitume wake

Baba Mtakatifu amesema: “Wakati nikiendelea kutoa salam kwa makuhani wapya pamoja na familia na marafiki zao, basi ninawaalike kukumbuka ni wangapi Bwana anaendelea kuwaita kwa jina, alifanya hivyo siku moja kwa mitume wake katika ziwa la Galilaya, ili waweze kuwa wavuvi wa watu. Kwa kutazama Injili ya Siku anasema Yesu anajiwakilisha kama rafiki wa kweli na Mchungaji mwema wa watu wa Mungu, na kwamba uhusiano wa Kristo na zizi lake ni ule wa kurudia rudia kuwaita. Kazi yake inajikita katika matendo, kwa maana yeye anatambua kila shauku ya moyo, matumaini  hata kishindwa, kukata tamaa, lakini wakati huo huo, yeye anatoa maisha ya milele, anahifadhi, anatukaribisha na kutupenda kama jinsi tulivyo, tukiwa na wema na udhaifu wetu. Katika  Injili  Baba Mtakatifu anaema yapo matendo mengine ya ushauri kama vile ya kusikiliza na kufuata ambayo yahusu zizi na kuonesha ni kwa namna gani  ya kuweza kutoa jibu  katika mtindo mwema kwa matakwa ya Bwana

Kusikiliza na kutambua sauti ya Bwana

Kusikiliza na kutambua sauti yake kwa hakika inahitaji umakini wa ndani na Yeye kwa maana kwa maana ya kujikita kwa undani zaidi katika sala na kukutana moyo kwa moyo na Mwalimu Mkuu na Mchungaji mkuu wa Roho zetu. Umakini huu Baba Mtakatifu Francisko anasema, unakuza ndani mwetu ule utashi wa kumfuata, katika na ili kuondokana na njia potofu, kuacha kabisa zile tabia za unafiki na kutambea hatimaye katika njia mpya za udugiu na zawadi yetu wenyewe katika kumwinga Yesu pekee yake!

Wahudumu wa Kristo katika Kutangaza Injili

Kwa njia ya kujiki kuwa na mmunga wa ndani na Mungu, Baba Mtakatifu amesema  ndipo inakuja ile furaha ya kutaka kufumata , kuacha upelekwe na yeye katika utimilifu wa Maisha ya Milele. Na kwa njia ya Mama Maria, Baba Mtakatifu Francisko anawakabidhi Makuhani wote na watawa. Kwani :“Yeye aliyejibu tayari wito wa Mungu awasidie  kwa namna ya pekee wale wote ambao wameitwa katika njia ya ukuhani na maisha ya kitawa kuupokea kwa furaha na uwezekano wa mwaliko wa Kristo kuwa wateule wake na wahudumu wwa tangazo la Injili na huduma ya Ufalme wa Mungu katika wakati wetu”.

Maneno yake Baba Mtakatifu kuhusu sikukuu ya mama na Mama wa Fatima

Mara baada ya tafakari yake amewasalimia wahujaji na waamini wote kutoka pande zote za dunia na kuwasalimia kwa namna ya pekee mama wote katika fursa ya sikukuu yao, wakati uwanja mzima wa Mtakatifu Petro ulisikika kwa makofi na vifijo… Baba Mtakatifu amesema: “Katika nchi nyingi leo hii wanaadhimisha Siku ya Mama. Ninapenda kuwasalimia mama wote na wakushukuru kwa makofi mama wote. Hii ni  kwa ajili ya shughuli ya msingi ya kulea watoto na kulinda thamani ya familia. Aidha Baba Mtakatifu Francisko amesema: “Vile vile tukumbuke hata Mama ambao wanatutazama kule mbingunu na wanakesha kwa ajili yetu. Na  Wazo kuu vile vile ni kumwenda Mama yetu wa Mbinguni anaye adhimishwa kesho tarehe 13 Mei kwa jina la  Mama  Yetu wa Fatima. Kwake yeye tujikabidhi ili kuendelea na furaha na ukarimu wa safari yetu.

 

 

12 May 2019, 13:20