Tafuta

Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko akikutana na wahudumu wa majumba ya makumbusho ya Kanisa ya Italia amehimiza haki ya uzuri wa  utamaduni kwa wote hasa masikini Baba Mtakatifu Francisko akikutana na wahudumu wa majumba ya makumbusho ya Kanisa ya Italia amehimiza haki ya uzuri wa utamaduni kwa wote hasa masikini   (ANSA)

Baba Mtakatifu Francisko:Wote wanayo haki ya kuona uzuri na zaidi walio masikini zaidi!

Baba Mtakatifu Francisko amekutana na wajumbe 400 wa Chama cha majumba ya makumbusho ya Kikanisa nchini Italia na kupendelea kuzungumza nao kwaida na hotuba yake amewakabidhi.Anawashukuru kwa kazi yao na shauku,taaluma na upendo kwa ajili ya Kanisa,katika majumba ya makumbusho ya majimbo na katika taasisi za dini Italia.

Na Sr. Angela Rwezaula -Vatican

Baba Mtakatifu Francisko tarehe 24 Mei 2019 amekutana na wajumbe wa Chama cha Majumba ya makumbusho ya Kanisa la Italia wakiwa na Rais wao, mkurugenzi wa kitaifa wa majengo ya kikanisa na Ibada wa Baraza la Maaskofu Italia, pamoja na wahudumu na watu wa kujitolea katika majimbo katoliki na Taasisi za dini nchini Italia karibu watu 400. Baba Mkatifu amependa kuzungumza nao bila kusoma hotuba yake na kuwakabidhi ili wajisomee wenyewe. Katika hotuba aliyo wakabidhsi anasema kuwa chama chao kinashuhudia jibu la dharura ya kuandaa na kujikita katika mazungumzo na idadi kubwa ya hali halisi ya majumba ya makumbusho, makubwa  na madogo yaliyoko nchini Italia. Hii ni shukrani  kwa Mungu kwa huduma ambayo inazidi kukua. Majumba ya makumbusha ya kikanisa kwa dhati yanaunganishwa na utume unaofafanana wa kutoa taarifa inayoonekana katika mchakato uliofanyika kwa karne nyingi za Kanisa katika ibada, katekesi, masomo na kutoa upendo (barua kuhusu  kazi ya kichungaji ya majumba ya makumbusha ya kikanisa 2001).

Urithi wa kihistoria,kisanii na kutamaduni

Baba Mtakatifu Francisko aidha akikumbusha katika Wosia wake wa Laudato si, anasema amejikita juu ya urithi wa kihistoria, kisanii na kiutamduni pamoja na urithi wa asili kwamba ni sawa sawa kuwa huko hatarini. Hiyo ni sehemu ya utuambulisho wa pamoja katika sehemu na msingi kwa ajili ya kujenga mji wa kuishi. Lazima kufungamanisha historia, utamaduni, usanifu wa mahali fulani, kulinda utambulisho wake asili kwa kufanya mazungumzo kwa njia ya lugha ya kiufundi na lugha ya watu mahalia. Ni utamaduni wa maelewano (rej LS n.143). Kwa njia hiyo ni muhimu majumba ya makubusho yaweze kuzingatia kuwa na mahusiano mema na sehemu mahali ambapo wamechimba mizizi, kushirikiana na Taasisi nyingine zinazofanana nazo. Majumba ya makumbusho yana nafasi nzuri katika maisha ya watu kwa kuunda nafasi zilizo wazi katika mahusiano kati ya watu, mahali pa kuleta pamoja ukaribu na fursa ya kutengeneza jumuiya. Katika vituo vikubwa vinapendekeza kutoa fursa ya utamaduni na kwa kuwakilisha historia ya mahali pale. Katika miji midogo  BababMtakatifu anasema inasaidia kwa dhati kudumisha utambulisho wake ambao unafanya kujisikia nyumbani. Daima wanasaidia kukuza mtazamo wa uzuri. Sehemu za miji na maisha ya watu wanahisi majumba ya makumbusho yenye kuwawezesha kuonja uzuri huo kama kilelelezo cha maisha ya watu, na malewano na mazingira, kukutana na kusaidiana kwa pamoja. ( Laudato si' 50).

Kazi yao ni yenye shauku ya kueneza utamaduni na sanaa

Baba Mtakatifu Francisko ameelezea juu ya kazi yao kama shauku yao katika utamaduni, historia, sanaa ya kuitambua na kuilinda. Wao wana shauku kwa ajili watu wa ardhi yao ambao wanatoa huduma na  wanaweza kweli kuonesha taaluma yao. Lakini pia hata shauku ya Kanisa na utume wake. Majumba ya makumbusha ambayo wao wanawalikisha uso wa Kanisa, matunda ya kisanii na kiufundi wito wake wa kutangaza ujumbe ambao ndiyo Habari Njema. Ujumbe ambao si kwa wote wamechaguliwa lakini kwa ajili ya wote. Wote wana haki ya utamaduni mzuri! Baba Mtakatifu amathibitisha kuwa na  zaidi wale masikini zaidi na walio wa mwisho ambao lazima wawezo kuonja kama zawadi ya Mungu. Baba Mtakatifu amasema kuwa majumba ya makumbushio ya Kanisa na kwa wote wanashiriki katika maisha ya kichungaji ya kijumuiya kuwasilisha uzuri wa michakato ya ubunifu wa kibinadamu na ambao wanaeleza utukufu wa Mungu. Kwa maana hiyo washirikiane na ofisi mbalimbali za maimbo. Hata katika maparokia na mashule. Baba Mtakatifu Francisko anatoa  mwaliko wa Kanisa nchini Italia kuendelea kutembea katika Wosia wake wa Evangelii gaudium. Na kwamba anafikiri hata wosia mwingine wa mada ya utakatifu kuhusu Gaudete et exsultate ambao kwa namna ya pekee unawatazama wao kwa sababu majumba ya makumbusho ya kikanisa ni sambamaba na utakatifu wa watu wa Mungu. Ni mantiki ya kiajabu amesisitiza.

 

24 May 2019, 13:35