Tafuta

Vatican News
Papa Francisko: Siku ya Faraja: Mshikamano na Wagonjwa waliolazwa kwenye Hospitali ya Gemelli, Roma. Papa Francisko: Siku ya Faraja: Mshikamano na Wagonjwa waliolazwa kwenye Hospitali ya Gemelli, Roma. 

Papa Francisko: Siku ya Faraja: Mshikamano na Wagonjwa!

Baba Mtakatifu Francisko amewatumia salam za pongezi na baraka zake za kitume, mahujaji kutoka Poland, waliokuwa wanashiriki katika hija kwenye Madhabahu ya Bikira Maria wa Piekari Slaskie. Katika maadhimisho ya Siku ya Faraja, Jumapili tarehe 26 Mei 2019, Papa ameyaelekeza mawazo yake kwenye Hospitali ya Gemelli ili kuhamasisha moyo wa mshikamano na wagonjwa huko Gemelli.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya tafakari wakati wa Sala ya Malkia wa Mbingu, Jumapili, tarehe 26 Mei 2019 kwenye Uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican, amewakumbuka na kuwaombea: waamini na mahujaji kutoka ndani na nje ya Italia waliomiminika kwa wingi kuungana naye kwa Sala ya Malkia wa Mbingu. Ametambua uwepo wa vijana walioimarishwa kwa Sakramenti ya Kipaimara kutoka Jimbo kuu la Genova, lililoko Kaskani mwa Italia.

Kwa namna ya pekee kabisa, Baba Mtakatifu amewatumia salam za pongezi pamoja na baraka zake za kitume, mahujaji kutoka Poland, waliokuwa wanashiriki katika hija kwenye Madhabahu ya Bikira Maria wa Piekari Slaskie. Katika maadhimisho ya Siku ya Faraja, Jumapili tarehe 26 Mei 2019, Baba Mtakatifu ameyaelekeza mawazo yake kwenye Hospitali ya Gemelli ili kuhamasisha ari na moyo wa mshikamano na udugu pamoja na wagonjwa waliolazwa hospitalini hapo! Mwishoni mwa ujumbe wake, Baba Mtakatifu Francisko, amewatakia wote Jumapili njema na kuwaomba kumkumbuka na kumsindikiza katika maisha na utume wake kama Khalifa wa Mtakatifu Petro kwa njia ya sala!

Papa: Wagonjwa Gemelli
26 May 2019, 14:46