Tafuta

Vatican News
Tarehe 12 Mei 2019, Baba Mtakatifu ameadhimisha Misa Takatifu na kutoa daraja la upadre kwa makuhani 19 Tarehe 12 Mei 2019, Baba Mtakatifu ameadhimisha Misa Takatifu na kutoa daraja la upadre kwa makuhani 19  (Vatican Media)

Baba Mtakatifu amewasihi makuhani wapya 19 wawe karibu na Watu wa Mungu

Baba Mtakatifu ameadhimisha Misa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro na kuwapatia daraja Takatifu mapadre wapya 19. Bwana Yesu ni kuhani na Mkuu wa Agano jipya lakini hata kwa watu watakatifu wa Mungu ambao pia wamewekwa kuwa makuhani amesema Papa.Wateule watakuwa washiriki wa utume wa Kristo,Mwalimu pekee na kuhani katika Ekaristi.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Hawa watoto wetu wameitwa katika daraja Takatifu. Itakuwa vizuri kwetu sisi kutafakari kwa kina kuhusu utume wao watakao fanya katika Kanisa. Ni maneno ya utangulizi wa Baba Mtakatifu Francisko katika misa ya kutoa daraja Takatifu la Upadre kwa mapadre wapya 19 kutoka katika majimbo na mashirika  ya kitawa. Misa hiyo imefanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican tarehe 12 Mei 2019 . Ikiwa ni siku ya Mchungaji mwema sambamba na siku ya 56 ya kuombea miito duniani, Baba Mtakatifu amesema: Bwana Yesu ni kuhani na  Mkuu wa Agano jipya, lakini pia hata kwa watu watakatifu wa Mungu ambao pia wamewekwa kuwa makuhani. Na si kwa bahati mbaya kati ya mitume wake, Bwana Yesu alitaka kuchagua miongoni mwao kwa namna ya pekee, ili waweze kutenda katika Kanisa kwa jina lake, shughuli ya kikuhani kwa watu wote na kuendeleza fumbo lake la utume wa  kikuhani na kichungaji. Kama yeye alivyo tumwa na Baba, ndivyo naye anafanya katika ulimwengu akianzia na Mitume wake, baadaye maaskofu wafuasi wao na mwisho kuwapatia wasaidizi ambao ni mapadre ili kuungana na utume wa kikuhani unaojieleza katika kutoa huduma kwa watu wa Mungu.

Baada ya miaka mingi ya mafunzo na tafakari yao, wanasindikizwa mbele na walimu wao

Baada ya miaka mingi ya mafunzo na tafakari yao na wakuu wao ambao wamewasindikiza  katika njia hii, leo hii wamewakilishwa, ili yeye aweze kutoa Daraja la kikuhani.  Wao watafanana na Kristo Kuhani Mkuu hata Milele au watawekwa wakfu kama makuhani wa kweli wa Agano Jipya na wakati huo wanaunganisha katika ukuhani na Askofu wao mbapo  watakuwa watangazaji wa Injili, wachungaji wa watu wa Mungu na wataadhimisha matendo yote ya ibada, hasa kuadhimisha sadaka ya Bwana yaani Ekaristi. Akiwageukia  wateule, Baba Mtakatifu amesema "mnakaribia kupewa daraja la kikuhani",na kwa maana hiyo wafikirie kwamba kwa kufanya mazoezi ya huduma ya Mafundisho Matakatifu watakuwa washiriki wa utume wa Kristo Mwalimu Pekee. "Hiki siyo chama cha kiutumaduni aukikundi cha kisiasa", anasema Baba Mtakatifu bali wao " wanashiriki huduma ya Kristo"; Watawatangazia wote Neno la Mungu ambalo wamelipokea kwa furaha tangu wakiwa watoto. Na kwa maana hiyo wasome na kutafakari kila mara Neno la Mungu na kuamini kile wachosoma na kufundisha walicho jifunza kwa imani na kuishi kile wanachofundisha. Haiwezekani kufanya mahubiri yao, bila kuwa na sala nyingi na kuwa na  Biblia mkononi. Baba Mtakatifu amehimiza hilo na  kwamba wasisahau!

Wawalishe watu wa Mungu kwa mafundisho yatokanayo na moyo wa sala

Kwa maana hiyo wawalishe watu wa Mungu kwa mafundisho, yatokanayo ndani ya moyo wa sala na ambayo kwa hakika tazaa matunda. Wao wawe sadaka na msaada wa waamini wa Kristo, harufu nzuri ya maisha; wawa watu wa sala na watu wa sadaka, kwa sababu Neno na mfano wao  uweze kujenga nyumba ya Mungu ambayo ni Kanisa. Baba Mtakatifu amesisitiza kwamba waendelea  na huduma  hiyo ya kristo na kutakatifuza. Na kwa njia ya huduma yao, sadaka ya kiroho ya waamini inakamilishwa kwa sababu imeungana na sadaka ya Kristo na kwa ajili ya mikono yao; kwa jina la Kanisa zima, hutolewa kwa njia ya mwili na  damu juu ya altare  katika maadhimisho ya mafumbo matakatifu.

Makuhani wawe makini katika maadhimisho ya Ekaristi

Baba Mtakatifu anawaonya wawe makini katika kuadhimisha Ekaristi takatifu. Watambue kwa dhati kile ambacho wanafanya, waige kile wanacho adhimish, na  kwa sababu ya kushiriki mafumbo ya kifo na ufufuko wa Bwana, wanabeba kifo cha Kristo katika miili yao na kutambea naye katika mambo mapya ya maisha. Bwana alitaka kuwaokoa bure, Yeye mwenyewe alisema: “mmepewa bure na toeni bure kile mlicho nacho” kwa maana  Maadhimisho ya Ekaristi ni hitimisho la bure la Bwana:Baba Mtakatifu amewaomba: tafadhali wasiichafue kwa ajili ya maslahi binafsi.

Katika ubatizo watashirikisha  waamini wapya wa Mungu

Baba Mtakatifu Francisko akiendelea na mahubiri amesema kuwa:“kwa njia ya Ubatizo itawaunganisha waamini wapya, yaani Watu wa Mungu. Kwa njia ya Sakramenti ya kitubio  watasamehewa dhambi kwa jina la Mungu, la Kristo na la Kanisa. “Na hapa, tafadhali, nawaombeni msichoke kuwa wenye huruma”, amesisitiza. Kuwa wenye huruma kama Baba, kama Yesu alivyokuwa mwenye huruma kwetu sote.  Kwa mafuta matakatifu mtawapatia faraja wagonjwa. Mtapoteza muda kwa ajili ya kutembelea wagonjwa. Mtaadhimisha ibada Takatifu na kuinua sala zenu katika masifu mbalimbali na maombi ya siku, vitu ambavyo vitawafanya kuwa na sauti ya Watu wa Mungu na ya binadamu wote”.

Na kwa utambuzi wa kuwa mmechaguliwa kati ya Mungu na kuweka kwa ajili yao, mkiwa mnasubiri mambo ya Mungu, Baba Mtakatifu ameongeza kusema:  fanyeni kazi kwa furaha na upendo, kuwa wazi na  fanya kazi ya makuhani wa Kristo kwa dhati na  kumpendeza Mungu kwa dhati  lakini  si kwa ajili ya mtu binafsi. Furaha ya kikuhani inapatikana kwa njia hiyo, yaani  ya ibada tu katika kutafuta Mungu aliye tuchagua. Na  Hatimaye Baba Mtakatifu amesema, kwa kushiriki katika utume  wa Kristo, Mkuu  na Mchungaji, katika ushirikiano  na Askofu wao, wajibidishe kuunganisha waamini katika familia moja.  Na hiyo ndiyo ukweli  kuwa kuhani, yaani kuwa karibu na Mungu katika sala, karibu na askofu ambaye ni baba wao, karibu na makuhani wengine, kama ndugu, bila malumbano  kati ya mmoja na  mwingine au kuzungumza vibaya mwingine, kuwa karibu na Watu wa Mungu ili waonekane mbele ya macho yao kama Mchungaji mwema, ambaye hakuja kutumikiwa, bali kutumikia na kutafuta kuokoa kilichopotea!

12 May 2019, 12:40