Tafuta

Vatican News
Vijana wa jimbo la Aire na  Dax nchini Ufaransa wamekutana na Papa Francisko Vijana wa jimbo la Aire na Dax nchini Ufaransa wamekutana na Papa Francisko   (Vatican Media)

Vijana watambue Kanisa limetembea miaka elfu 2 likishirikisha furaha,matumaini,huzuni na huchungu wa watu!

Tarehe 25 Aprili 2019 Baba Mtakatifu amekutana na vijana wa Jimbo la Aire na Dax kutoka Ufaransa.Ambapo amewaeleza kwamba,anawategemea wao.Na Kanisa linahitaji juhudi,shauku na imani yao!Hata hivyo amesema,Vijana watambue Kanisa limetembea kwa miaka elfu mbili likishirikisha furaha na matumaini,huzuni na huchungu wa watu

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Tarehe 25 Aprili 2019, Baba Mtakatifu Francisko, amekutana na vijana wa Jimbo la Aire na Dax kutoka Ufransa, wakiwa katika fursa ya hija yao mjini Roma. Anamshukuru Askofu Souchu wa Jimbo hilo, kwa hotuba yake na kuwasalimia vijana, akionesha ukaribu wake wa kiroho kwamo  na waamini wote wa jimbo hilo. Kadhalika anashukuru Mungu kutokana na wahusika wa kichungaji kwa vijana, kuanzisha tendo hili kwa ushirikiano na Askofu wao  ambao walipendekeza kuishi uzoefu wa “Siku ya Vijana wa Landes”. Baba Mtakatifu abainisha kwamba ni fursa nzuri sana ambayo inawasidia kupyaisha ndani ya maisha yao ile zawadi ya imani, Mjini Roma katika sehemu walizoishi Mitume Petro na Paulo na mashahidi wengi, na kwamba kati yao kuna  hata vijana ambao walikabiliana na kifo dini, kutokana na kuchagaua kubaki kidete katika imani kwa Yesu Kristo.

Ni jambo la ujasiri kubaki katika imani, maana kwa watu wengi imekuwa vigumu

Baba Mtakatifu Francisko anasema hili ni jambo muhimu zaidi kwa sababu watu wengì leo hii wanafikiri ni vigumu zaidi kukiri ukristo na kuishi  imani katika Kristo. Anao uhakika  kwamba wao kwa hakika wanafanya uzoefu ambao ni mgumu na ambao umegeuka wakati mwingine kuwa majaribu. “Kwa hakika katika mantiki ya sasa, siyo rahisi, hata kwa sababu ya uchungu na ugumu wa masuala ya manyanyaso yaliyo tendwa na baadhi ya wajumbe wa Kanisa. Baba Mtakatifu kurudia kusema kuwa: “leo hii ni vigumu zaidi kuliko nyakati nyingine za Kanisa”. Kwa maana hiyo anawahamasisha wachukue fursa ya hija, ili waweze kugundua kuwa licha ya kuwa ni wajumbe wa  Kanisa , lakini limetembea kwa miaka elfu mbili, kwa kushirikishana furaha na matumaini, huzuni na huchungu wa watu. Na linatambea hivi bila kwenda kwa daktari yoyote kutafuta uzuri (Rej.Wosia wa Christus vivit, 101). Na kwa kuwatazama wao, Baba Mtakatifu anatambua kazi ya Bwana Yesu ambaye haachi kamwe Kanisa lake na kwamba, anaruhusu kwa neema ya ujana wao, shauku zao na talanta ambazo yeye mwenyewe amewazawadia, ili kujipyaisha na kuwa vijana zaidi katika hatua mbalimbali za historia yake.

Vijana waige mfano wa wachungaji wanaowatangulia katika imani

Baba Mtakatifu Francisko aidha amesema, kwa msaada wa wachungaji wao, kaka na dada wakuu katika imani,na kwa mfano wa watakatifu ambao walikabiliana na matatizo ya kweli wakati wa nyakati zao, anawatia moyo ili wabaki wameungana na Bwana, kwa njia ya kusikiliza Neno, kupokea sakramenti, maisha ya kindugu na kwa huduma ya wengine. Katika Kanisa Takatifu na ambalo limeundwa na wadhambi, wanaweza kutambua ni neno lipi na ujumbe upi wa Yesu ambao Mungu anataka kuelekeza Kanisa kwa njia ya maisha yao na ambaye kwake ameungama naye (rej. Wosia Gaudete et exsultate, 24).

Baba Mtakatifu pia amesema katika sura ya  mti wao wa Kanda uliojaa (landes)  na uliowezesha kuponyesha sehemu zenye mabwawa, wao waweze kutanda kama mizizi ya upendo wa Mungu ili kwamba, mahali wanapoishi Kanisa liweze kupendwa. Wajiachie ili wabadilishwe na kupyaishwa na Roho Mtakatifu katika kupeleka Kristo kila mahali na kushuhudia furaha na ujana wa Injili! Katika mfano wa Mtakatifu Vincenti wa Pauli, Landesi kama yeye, waoneshe upendo ambao Mungu amewajalia akipenda kwa nguvu za mikono na jasho lake usoni! Kwa maana hiyo wawe wajenzi wa madaraja kati ya watu, katika kukuza utamaduni  na mazungumzo, kuchangia katika mantiki ya kweli ya udugu wa kibinadamu. Katika umakini wao kwa wadogo na masikini, wao wanaweza kuwasha nyota katika usiku wa wale ambao kwa namna tofauti wamejaribiwa.

Vijana wanaweza kuonesha kuwa Mungu nayo mambo mapya daima

Kwa kuhitimisha, Baba Mtakatifu amesema, wao wanaweza kuonesha  kwa ishara na maneno, kuwa Mungu daima anayo mambo mapya (…) na kwamba anatupeleka pale mahali ambapo binadamu anapatikana lakini  akiwa na majeraha zaidi na mahali ambapo binadamu wote wako chini ya mtazamo kijuu juu tu na hufananisho ili kuendelea kutafuta jibu kuhusu swali la  nini maana ya maisha ( …) Baba Mtakatifu anasema kwamba anawategemea wao. Kanisa linahitaji juhudi zao, shauku zao na imani yao! Katika matumaini hayo, anawakabidhi kwa Bwana na katika maombezi ya Bikira Maria mama wa Buglose na Mtakatifu  Vincenti wa Pauli. Amewabariki kwa Baraka ya Kitume wao na waamini wote wa Jimbo la Aire na Dax. Lakini pia anawaomba wasali kwa ajili yake!

 

25 April 2019, 13:30