Tafuta

Vatican News
Papa katika katekesi yake anahimiza juu ya msamaha kwa maana bila kusamehe hata Mungu hana msamaha! Papa katika katekesi yake anahimiza juu ya msamaha kwa maana bila kusamehe hata Mungu hana msamaha!  (Vatican Media)

Papa anahimiza kusamehe wengine kutokana na wema tulioupata kutoka kwa Mungu!

Katika mwendelezo wa Katekesi ya Papa anasema,sisi sote ni wadeni mbele ya Mungu na watu wengi ambao wametuzawadia hali ya maisha mema.Utambulisho wetu unajengeka kuanzia na wema tulio upokea.Na Jambo la kwanza ni maisha.Yeye anatupenda upendo upeo zaidi ya sisi tunavyompenda.Tunahitaji kusemehe wengine!

Na Sr Angela Rwezaula - Vatican

Mara baada ya somo lilioandaliwa kutoka Injili ya Matayo 18,21-22 isemayo:Kisha Petro akaja kwa Yesu akamwuliza, “Bwana, ndugu yangu anikosee mara ngapi nami niendelee kumsamehe? Hata mara saba?” Yesu akamjibu, “Sikuambii mara saba, bali saba mara sabini”. Baba Mtakatifu Francisko tarehe 24 Aprili 2019 ameendeleza tafakari ya Katekesi yake kuhusu sala ya Baba yetu, kwamba ni kujikita katika hitimisho la ombi la tano linalohusu:“Kama na sisi tunavyo wasamehe waliotukosea”, (Mt  6,12).  Katika sehemu hii tunaona kuwa ni mtu, ni mwenye deni mbele ya Mungu. Kwake yeye tumepokea kila kitu,kwa maana  ya asili na neema.  Maisha yetu si kwamba yalitamaniwa tu lakini pia yalipendwa.  Kwa hakika hakuna nafasi ya kujidai tunapo unganisha mikono yetu kusali. Na  hakuna “self made man”, yaani watu ambao wamejitengenezwa wenyewe. Sisi sote ni wadeni mbele ya Mungu na kwa watu wengi ambao wametuzawadia hali ya maisha mema.Utambulisho wetu unajengeka kuanzia na wema tulio upokea. Na Jambo la kwanza ni maisha au hapana?... anauliza Baba Mtakatifu.

Anayesali anajifunza kusema asante

Baba Mtakatifu anasema, anayesali anajifunza kusema “ asante” na kumwomba Mungu awe mwema kwake. Na kwa kadiri tunavyo jitahidi, lakini daima tunabaki na deni lisiloisha mbele ya Mungu na ambaye hatuwezi kamwe kumrudishia. Yeye anatupenda upendo upeo zaidi ya sisi tunavyompenda.  Na zaidi hata kwa  jitihada zetu tunazofanya ili kuishi kwa mujibu wa mafundishi ya kikristo, katika maisha, lakini  daima kutakuwapo na jambo ambalo lazima kuomba msamaha. Baba Mtakatifu anasema: “ tufikirie siku zilizopita za uvivu, au wakati mwingine wa kukaa na hasira katika ndani ya moyo… Na huo ndiyo uzoefu, kwa bahati mbaya mara nyingi unatufanya tuombe kwamba: “utusamehe kama dhambizi zetu”. Hata hivyo Baba Mtakatifu anathibitisha, kwa kufikiria vema, maombi hayo yangeweza kuishia katika sehemu ya kwanza tu; lakini kinyume chake Yesu anaongeza sehemu ya pili ambayo inafanya sentesi kuwa moja. Ina maana ya uhusiano wa wema kutoka juu kwa upande wa Mungu unajitamvua zaidi na kutualika kuutafsiri katika uhusiano  mpya ambao tunauishi na ndugu zetu. Mungu ni mwema anatualika sisi sote kuwa wema. Sehemu zote mbili za maombi zinafungamanishwa katika muungano wa huruma yaani “kama”. Tuombe Mungu atusamehe madeni yetu, makosa yetu kama tunavyo wasamehe marafiki, watu wanaishi na sisi, jiran ,  na kwa ajili ya watu ambao wametufanyia mambo yasiyo mema.

Kila mkristo anatambua kuwa kwake yeye upo msamaha wa dhambi

Kila mkristo anatambua kuwa, kwake yeye upo msamaha wa dhambi anasema Baba  Mtakatifu. Yesu alikuwa akiwasimulia wafuasi wake kuhusu sura ya Mungu unavyojionesha katika kilelelezo cha huruma iliyo njema. Anawaambia kuwa: “Vivyo hivyo kutakuwa na furaha mbinguni kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye, kuliko kwa ajili ya wenye haki tisini na kenda ambao hawana haja ya kutubu”. (Rej Lk 15,7.10). Hakuna lolote lenye kuleta wasiwasi katika Injili ya kwamba Mungu hasamehi dhambi hasa kwa yule aliye tayari na anayeomba aweze kukumbatiwa, amethibitisha Baba Mtakatifu Francisko. Lakini neema nyingi ya Mungu namna hiyo daima inawajibisha. Aliyepokea sana, lazima ajifunze kutoa sana na hasiweke kwa ajili yake kile alichopokea.

Vile vile Baba Mtakatifu anafafanua kwamba: Siyo kwa bahati mbaya Injili ya Matayo, mara baada ya kutuzawadia sala ya Baba Baba Yetu, kati ya vielelezo saba, vilivyotumika, anasisitiza hasahasa juu ya msamaha kindugu. “Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi. Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu”, (Mt 6,14-15). Kutokana na hiyo Baba Mtakatifu anasema:lakini hii ina nguvu nafikiri, kwa maana mara nyingine nimesikia watu wanasema: mimi sitomsamehe kamwe yule mtu! Kile ambacho amenifanyia kamwe sitomsamehe”... Lakini iwapo husamehi na Mungu hatakusamehe. Wewe unafunga mlango. Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu anaongeza kusema: Tufikirie, iwapo sisi tuna uwezo wa kusamehe na kama hatusamehi.

Historia ya mama mzee akiwa karibu yak ufa lakini hasamehi walio mkosea

Baba Mtakatifu akiendelea na kateksi yake aidha amesimulia historia moja kwamba akiwa katika jimbo jingine, siku moja padre mmoja alimsimulia akiwa na huzuni kwamba yeye alikwenda kumpatia sakramenti ya mwisho, mzee mmoja ambaye alikuwa anakaribia kifo. Mwanamke huyo hakuwa na uwezo wa kuzungumza, lakini Padre huyo alimuuliza: Je Mama unatubu dhambi zako?  Na yule mama alijibu ndiyo; kwa maana Baba Mtakatifu ameongeza kusema, hasingeweza kuungana lakini alisema ndiyo. Hiyo ilikuwa inatosha! Baadaye Padre huyo aliongeza swali la pili: Je unawasamehe wengine? Lakini mama huyo akiwa karibu ya kufa alijibu hapana. Jibu hili Baba Mtakatifu amesisitiza kwamba lilimfanya Padre  huyo abaki na huzuni sana. Kutokana na mfano huo Baba Mtakatifu amesema: Kama wewe husamehi, Mungu hawezi kukusamehe: tunaweza hata sisi tuliopo hapa, kama tunawasamehe, kama tunao uwezo wa kusamehe.  Lakini kuna wengine wanatafuta sabab kwamba:”kusema ukweli siwezi, kwa sababu mtu yule amenifanyia mabaya mengi…. Lakini kama wewe huwezi, basi mwambie Bwana akupe nguvu ya kuweza; Mwambie Mungu kuwa, nisaidie niweze kusamehe.

Upendo unaita upendo na msamaha unaita msamaha

Hiyo ndiyo kukutana na uthabiti kati ya upendo wa Mungu na ule wa jirani. Upendo unaita upendo, msamaha unaita msamaha. Pia katika Injili ya Matayo tunakutana na neno linalo husu msamaha kindugu (rej. Mt 18, 21-35). Kulikuwa ni mtumishi mmoja aliyekuwa na deni kubwa  kwa bwana wake. Talanta elfu kumi! Hicho kilikuwa ni kiasi kikubwa cha kutoweza kurudisha. Baba Mtakatifu anaongeaza kusema “ sijuhi ni kiasi gani kwa wakati wa sasa, lakini ni mamilioni ya fedha eh”… Lakini ukatokea muujiza, kwa mtumishi huyo, kwani  hakupokea adhabu ya kulipa, lakini alisamehewa  lile deni lote. Hii ilikuwa neema isiyotarajiwa! Lakini tazama mtumwa yule mara baada ya kutoka hapo, mara moja akamwona mmoja wa ndugu zake aliyekuwa na deni la dinari mia akamkamata, akamshika koo, akisema nilipe uwiwacho.  Japokuwa kiasi hicho hakuwa nacho, lakini alimsihi amvumilie, japokuwa hakutaka, kusikiliza sababu zake. Na mwisho Bwana alimwita huyo jamaa na kumhukukumu. Hii ni kwa sabababu iwapo huna juhudi za kusamehe, hutapata msamaha: iwapo hujitahidi kupenda, pia hutaweza kupendwa, Baba Mtakatifu amesema.

Yesu anajihusisha na uhusiano kwa nguvu ya msamaha

Yesu anajikita katika mahusiano ya binadamu kwa nguvu ya msamaha. Siyo kila kitu katika maisha kinapata suluhisho la haki. Na zaidi mahali ambapo ni kuwekwa pembeni ubaya, mmoja lazima afanye zaidi ya kile kinachotakiwa, ili kuweza kuanza kwa upya historia ya neema. Ubaya unatambua visasi vyake. Na iwapo hauvunjwi, ipo hatari ya kuenea sana  na kusonga dunia nzima. Baba Mtakatifu anatoa mfano kwamba Katika sheria ya mkato inasema kile ambacho umenifanyia mimi nami nina kurudishia, na wakati mwingine ishara hizo zinafanyika au hapana? Na ambazo wote tunazitambua, ameuliza Baba Mtakatifu. Lakini Yesu anabadilisha sheria hiyo kwa njia ya upendo na kwa maana hiyo kile ambacho Mungu amenifanyia, mimi ninakurudishia wewe! Baba Mtakatifu ametoa ushauri kwamba: Tufikirie leo hii, katika wiki ya Pasaka ambayo ni nzuri, iwapo mimi nina uwezo wa kusamehe na kama ninahisi kutokuwa na uwezo, niombe kwa Bwana anipatie neema ya kusamehe, kwa maana ni neema. Kwa kuhitimisha Baba Mtakatifu anasema: Mungu anatoa kwa kila mkristo neema ya kuandaa historia ya wema katika maisha ya ndugu zake, hasa hasa wale ambao wanatimiza kile kisichopendeza na chenye makosa. Katika neno moja, ni mkumbatio na  tabasamu, hivyo tunaweza kuonesha wengine kile ambacho tumepokea tunu zaidi. Je ni tunu gani ambayo sisi tumeipokea? Ni  Msamaha ambao sisi tuna uwezo wa kuutoa kwa wengine. Asante

 

24 April 2019, 13:50