Salam za Papa baada ya sala ya Malaika wa Bwana
Baba Mtakatifu Francisko anathibitisha kwamba kwa kujipatanisha kwa mara nyingine tena, msamaha unatupatia amani na kutufanya tuanze historia iliyo pyaishwa. Kila uongofu wa kweli ni matazamio ya wakati mpya wa maisha mapya, maisha mazuri na maisha yaliyo huru dhidi ya dhambi na kuwa na maisha ya ukarimu. Hatuna hofu ya kuomba msamaha kwa Yesu, kwa sababu yeye anatufungulia mlango wa maisha mapya. Bikira Maria atusaidie kushuhudia wote upendo wa uhuruma ya Mungu ambaye ni katika Kristo anaye tusamehe na kufanya maisha yetu yawe mapya, akitoa fursa na uwezekano mpya wa kujipyaisha daima!
Ujasiri katika ushuhuda wa Yesu na Injili yake
Mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana tarehe 7 Aprili 2019 Baba Mtakatifu Francisko amewasalimia waamini na wote mahujaji kutoka pande zote za dunia, zaidi kama vile wanafunzi kutoka nchi ya Austria na Ufaransa. Aidha wanafunzi kutoka Bologna Genova, hata Torino na Vercelli. Wazo limewaendea vijana wa kipaimara kutoka Settignano, Scandicci, na wengine kutoka jimbo la Saluzzo,Italia waliosindikizwa na Askofu wao Cristiano Bodo. Anawataka wote wawe wajasiri katika ushuhuda wa Yesu na Injili. Kwa kupokea kipaimara wanapaswa wakue daima kwa ujasiri na wawe wajasiri. Amewakumbuka vijana wengine wadogo wenye umri wa miaka 14 kutoka Milano, waamini kutoka Pescara, Napoli na Terni. Kwa wote amewatakia Dominika njema na zaidi wasisahau kusali kwa ajili yake.