Vatican News
Papa anasema leo hii na kwa wiki nzima,furaha za Pasaka ya ufufuko wa Yesu zinarefushwa kutokana na tendo la kumbumbu ya ufufuko Papa anasema leo hii na kwa wiki nzima,furaha za Pasaka ya ufufuko wa Yesu zinarefushwa kutokana na tendo la kumbumbu ya ufufuko  (AFP or licensors)

PASAKA YA BWANA 2019:Injili zote zinaonesha wazi nafasi ya wanawake!

Ufufuko wa Bwana unajikita katika matukio ya kushangaza ya historia ya binadamu,inayothibitisha ushindi wa Upendo wa Mungu dhidi ya dhambi na kifo na kutoa matumaini ya maisha yetu,msingi thabiti kama mwamba.Ni katika tafakari ya Baba Mtakatifu Francisko wakati sala ya Malkia wa Mbingu Jumatatu 22 Aprili 2019

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Baba Mtakatifu Francisko katika Tafakari yake wakati wa Sala ya Malaika wa Bwana tarehe 22 Aprili 2019, wakati Mama Kanisa tayari yupo katika kipindi cha Pasaka na jumatatu ya pasaka iitwayo ya Malaika, anasema: “Leo hii na kwa wiki nzima, furaha za pasaka ya ufufuko wa Yesu zinarefushwa, mahali ambapo ni katika  tendo la kushangazwa limefanyiwa kumbukumbu jana”.

Wanawake wakiwa na hofu na furaha walikimbia kwa haraka kupelekea habari

Ufufuko wa Bwana, anasema Baba Mtakatifu, unajikita katika matukio ya kushangaza ya historia ya binadamu, inayothibitisha ushindi wa Upendo wa Mungu dhidi ya dhambi na kifo na kutoa matumaini ya maisha yetu, msingi thabiti kama mwamba. Katika siku ya Jumatatu ya Malaika, liturujia ya Injili ya Matayo (28,8-15), inatupeleka moja kwa moja karibu na kaburi wazi la Yesu. Wanawake wakiwa na hofu na furaha walikimbia kwa haraka kupeleka habari kwa wafuasi. Baba Mtakatifu anashauri kwamba,itakuwa vizuri nasi kwenda na wazo katika kaburi wazi la Yesu. Lakini wakati huo huo Yesu akawatokea mitume mbele yao na walimkaribia kwa kumbusu miguu yake na kuabudu, na kuamini kwamba hakuwa kivuli bali mtu kweli na Yesu aliwaondolea hofu zao katika mioyo yao.

Injili zote zinaonesha wazi nafasi ya wanawake:Maria Magdalena

Katika Injili zote zinaonesha wazi nafasi ya wanawake, Maria Magdalena na wengine, kama mashuhuda wa kwanza wa ufufuko, amesisitiza Baba Mtakatifu. Wanaume wakiwa na woga walikuwa wamejifungia katika nyumba kuu. Petro na Yohane baada ya kuhabarishwa na Magdalena, walichomoka haraka kwenda katika kaburi, lakini ambalo lilikuwa limefunguliwa na wazi. Hata hivyo amesema, ilikuwa ni vigumu kufikiria jambo kama hilo la Yesu wa Nazareti! Mungu alimfufua na kumkomboa na uchungu wa kifo (Mdo 2,22-24). Aidha, baada ya Siku Tatu za liturujia ya mateso kabla ya Pasaka, ambazo zimetufanya tuishi fumbo la kifo na ufufuko wa Bwana wetu Yesu Kristo na sasa kwa macho ya imani ni kutafakari mfufuka na anayeishi. Hata sisi tunaalikwa kukutana naye binafsi na kugeuka kuwa waenezaji na mashuhuda.

Kristo tumaini langu amefufuka

Katika utenzi wa Pasaka, unaoimbwa kwa siku hizi, tunaturudia kusema: “Kristo tumaini langu amefufuka! Pamoja na yeye, hata sisi tumefufuka kutoka katika mauti kufikia maisha; kutoka katika utumwa wa dhambi kuufikia uhuru wa upendo. Kwa maana hiyo tuache ili tuweze kuwa  na faraja ya ujumbe wa Pasaka na kuvaa mwanga wake mtukufu, ambao unaondoa giza la hofu na huzuni. Yesu amefufuka na yupo karibu nasi”. Yeye anajionesha kwa wale wote wanaomwomba na kumpenda. Awali ya yote katika sala, lakini hata katika furaha za kuishi kwa Imani na shukrani. Tunaweza kuhisi uwepo wake pia kwa kushirikisha wakati mzuri wa pamoja, wa makaribisho, wa urafiki na kutafakari uoto wa asili. Katika siku hii ya sherehe ambayo kiutamaduni ni ya kufurahia kidogo na ukuu wake, Baba Mtakatifu anathibitisha kwamba, inatusaidia kufanya uzoefu wa uwepo wa Yesu. Kwa kuhitimisha, Baba Mtakatifu anasema: “Tumwombe Bikira Maria ili kuweza kuchota kwa wingi na mikono  yetu amani na utulivu, zawadi ya Mfufuka na ili kuishirikisha na ndugu hasa wale wanaohitaji kutiwa moyo na matumaini.

22 April 2019, 13:00