Tafuta

Ishara ya kwanza ya Parokia inayofanya vizuri, Papa FRancisko anasema inaonekana katika  sala  kwa maana watu wanaposali, na katika parokia inayo sali watu wake wanakua kiroho Ishara ya kwanza ya Parokia inayofanya vizuri, Papa FRancisko anasema inaonekana katika sala kwa maana watu wanaposali, na katika parokia inayo sali watu wake wanakua kiroho 

Parokia ya Mt. Giulio: Parokia inayosali inaonekana katika matendo hai!

Jumapili,tarehe 7 Aprili 2019,Baba Mtakatifu Francisko ametembelea Parokia ya Mtakatifu Giulio Jimbo kuu la Roma,na kutabaruku Altare ya Kanisa wakati wa madhimisha Misa Takatifu.Amekutana na watu wa kujitolea na kuhimiza juu ya sala.Ameonesha ni kwa namna gani unaweza kuona kuwa Parokia ni hai.Ni katika kusali kijumuiya na hata nyumbani.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Baba Mtakatifu Francisko akiwa katika Parokia ya Mtakatifu Giulio Jimbo Kuu Roma tarehe 7 Aprili 2019 jioni alikutana na watu wa kujitolea na wahudumu wa Caritas. Kabla ya hotuba, mwakilishi wa kundi hili kwa niaba ya wote, aliweza kusoma risala yake inayohusu  shughuli kwa ujmla katika parokia. Baada ya ripoti hiyo Baba Mtakatifu Francisko amethibitisha kwamba kwa upande wake, kuna ishara tatu zinazo thibitisha kama parokia inafanya vizuri.

Sala iliyo hai, kwa wanaparokia, hata katika nyumba zao

Ishara ya kwanza ya kuonesha parokia inafanya vizuri ni sala, kwa maana watu wanaposali,na katika parokia inayo sali, watu wake wanakua kwa kusali, hata nyumbani kwao wanasali, hiyo kwa hakika ndiyo ishara ya kwanza! Lakini je unawezaje kuona kweli kama kweli wanasali au hawasali. Hiyo inatokana na kwamba sala inabadilisha kila kitu. Kwa mujibu wa upendo wa kweli, wao kweli wanajionesha kutenda. Kusaidia wale wanaohitaji, ndugu kaka na dada na familia…. Hata mahitaji yaliyofichika, yasiyoonekana, maana Baba Mtakatifu amethibitisha kwamba  walio wengi wana aibu ya kujioneaha lakini wapi wengi sana

Upendo wa kujishughulisha na ndiyo ya kweli ni ishara ya pili

Inahitajika upendo wa kujishughulisha, upendo ulio hai, upendo wa “kusema ndiyo”. “Ndiyo” mimi hapa nina fanya hicho. “ Ndiyo mimi” iliyo hai ni ishara ya pili.  Na ishala ya tatu ni ya upendo ya wa busara.  Je ina maana gani upendo wa busara?  Ni ule wa kupendana na siyo kusemana kati yao. Kwa maana masengenyo  ni ugonjwa wa nguvu sana, iwapo kuna masengenyo katika parokia Baba Mtakatifu anathibitisha kuwa, haiwezekani mambo kwenda vizuri.  Ni tabia ambayo inaingia kichini chini ya kupelekea habari za hapa na pale kuwasema wengine… hiyo hapana, ameonya wasifanya hivyo! Na mwisho wamesali sala ya salama Maria na kuwabariki.

08 April 2019, 10:54