Tafuta

Vatican News
Ziata ya kichungaji ya Baba Mtakatifu Francisko katika Parokia ya Mtakatifu Giulio huko Monteverde Ziata ya kichungaji ya Baba Mtakatifu Francisko katika Parokia ya Mtakatifu Giulio huko Monteverde  (Vatican Media)

Parokia ya Mt. Giulio:Inabidi kukarabati hata roho zinapo karibia kuanguka!

Baba Mtakatifu akiwa katika ziara ya kichungaji amekutana hata waliokarabati Kanisa la Mtakatifu Giulio na kuwashukuru,lakini akiwahimiza nao wekarabati daima roho zao.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Ni vizuri kujenga Kanisa, ni zuri sana  Kanisa linakwenda mbele, linakuza fadhila za kikristo kwa njia ya mantendo ya upendo na matendo ya kiliturujia,na utakatifu wa wote. Vile vile ni  lazima kufanya muhimili wa Kanisa ili kuadhimisha Ekaristi. Ndiyo maneno ya Baba Mtakatifu Francisko aliyowaeleza wale waliojikita katika kukarabati Kanisa la Mtakatifu Gulio wakati wa kukutana nao tarehe 7 Aprili 2019 akiwa katika ziara yake ya kichungaji.

Linda utakatifu usianguke

Baba Mtakatifu anasema  kwa kutazama maelezo, na picha walizo muonesha, ameona ni kwa jinsi gani Kanisa lilivyokuwa na hatari ya kuanguka. Kwa hakika lilikuwa katika hatari! Na hiyo amethibitisha kwamba ni lazima kuwa makini katika jumuiya ya Parokia, katika maisha ya fadhila na matendo ya kiliturujia na ili utakatifu usianguke!

Sala nazo zisianguke kama jengo lilivyo anguka

Kadhalika Baba Mtakatifu Francisko amesema kuwa, hata sala zisianguke, kama jinsi unavyoweza kuanguka, na tunapoona kwamba mambo yako vile, lazima kufanya kila njia na kuanza upya ujenzi wa Kanisa la kiroho, yaani ndani mwetu, anasisitiza Papa. Iwapo hakuna udugu wa kiparokia, iwapo kuna maneno maneno, kwa haraka lazima waite kampuni ya kiroho kama walivyoita kampuni ya ujenzi  kukarabati Kanisa hilo. Anashukuru kampuni hiyo ya ujenzi  kwa ajili ya kukarabati Kanisa; anawashukuru hata kwa kazi ya kiroho ya Paroko anayoifanya ili Kanisa liweze kuwa Takatifu. Amehitimisha na kuwabariki.

 

 

 

 

08 April 2019, 10:14