Tafuta

Vatican News
Papa amekutana na wajumbe wa Chama cha Mama Yetu wa Cinta, huko Tortosa nchini Hispania na kuwahimiza kuendeleza udugu ambao ni zawadi kutoka kwa Mungu Papa amekutana na wajumbe wa Chama cha Mama Yetu wa Cinta, huko Tortosa nchini Hispania na kuwahimiza kuendeleza udugu ambao ni zawadi kutoka kwa Mungu  (ANSA)

Papa kwa wanachama wa Tortosa anawahimiza wawe chachu!

Utume wa kidugu,upendo na mshikamano kwa wengine katika Kanisa na ndani ya jamii,ndiyo maelekezo ya Baba Mtakatifu Francisko kwa wajumbe wa chama cha Bikira Maria wa Cinta huko Tortosa nchini Hispania aliokutana nao wakiwa katika fursa ya kuadhimisha miaka 400 tangu kuanzishwa kwa chama hicho.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Baba Mtakatifu Francisko  amekutana mjini Vatican, tarehe 12 Aprili 2019 na wajumbe wa chama Bikira Maria wa Cinta huko Tortosa nchini Hispania  wakiwa katika fursa ya kuadhimisha  miaka 400 tangu kuanzishwa kwa chama hicho. Na katika hotuba yake kwa lugha yakispanyola amejikita kukumbusha tangu kuridhiwa kwa Katiba yao na Papa Paulo V,  miaka 400 iliyopita. Ni mahusiano yenye nguvu ya upyaisho anasema, hasa  wakati wa hija yao katika kaburi la Mtakatifu Petro. Ni ishara ya kuungana na ambayo siyo ya wakti uliopita, lakini ambayo inaendelea kudumishwa na kuwa hai leo hii.

Chachu ya mshikamano

Baba Mtakatifu akiendelea na hotuba yake kwa wajumbe wa chama hiki amezungumzaia huu ya  udugu na muungano wake, anawakumbusha kwamba mara nyingi mafratelli wanagombana lakini wanatambua kutunza uhai katika kutafuta wema na ambao hauwezi kwenda kinyume na amani na maelewano kati yao. Iwapo hawafanyi hivyo kwa hakika wanateseka amethibitisha. Mahusiano ya upendo, kama yalivyo ya wanachama  yana waunganisha na Askofu wao, kwa njia yake na Papa  na kuwa zawadi muhimu ambayo inatoa utajiri ,lakini pia hata utume ule wa kuwa chachu ya mshikamano katika jamii!

Kuishi kudugu

Kazi ya wanachama wa Mama Yetu wa Cinta wa Tortosa anasema ni kupeleka udugu kila kona ya jamii. Baba Mtakatifu akumbuka uwepo wao katika hali halisi ya kikanisa katika jimbo mahalia, na kwamba ni ishara inayoonesha kwamba Kanisa ni nyumba ya familia na mahali penye karimu na upendo, mahali ambapo wote kwa namna ya pekee masikini na walio baguliwa wanahisi kuwa sehemu na hawatengwi kamwe au kusukumwa.

Katika kuishi kwa namna hiyo kama ndugu waliounganika, lakini inahitaji jitihada na kujakana binafsi, japokuwa anasisitiza ni vema kabia kufanya hivyo, kwa maana ndiyo ishara mwafaka mbele ya jamii ambayo daima inazidi kugawanyika na siyo ukisasa tu, kwa maana ilikuwa namna hiyo,japokuwa ni dhambi jamii kutugawanya anasema Baba Mtakatifu. Na ndiyo maana kila onesho la udugu na mashikamano unasaidia! Baba Mtakatifu anawatia moyo waendelee katika zoezi hilo na wao ni ishara ya udugu  mbele ya dunia na ambao unatoka kwa Mungu.

 

12 April 2019, 14:56