Tafuta

Vatican News
Tarehe 25 Aprili 2019 Papa Francisko amekutana na wajumbe wa Shirikisho la vyama vya Viziwi Italia (FIAS) Tarehe 25 Aprili 2019 Papa Francisko amekutana na wajumbe wa Shirikisho la vyama vya Viziwi Italia (FIAS)  

Papa kwa viziwi:uwepo wenu ni kujenga jumuiya ya ukarimu na nyumba zilizo wazi!

Baba Mtakatifu Francisko alipokutana na wajumbe wa Shirikisho la Vyama vya Viziwi Italia amehimiza kwamba katika miji,nchi na maparokia ambamo huduma hizo hutolewa,wote wanaalikwa kushinda vizingiti ambavyo daima haviruhusu kupokea kwa ukarimu uwepo wao hai na kwenda zaidi ya mtazamo wa ulemavu huo!

Na Sr Angela Rwezaula - Vatican

Tarehe 25 Aprili 2019, Baba Mtakatifu Francisko amekutana na Shirikikisho la Vyama vya Viziwi nchini Italia wakiwa na familia, marafiki na Rais wa Shirikisho hilo. Katika Hotuba yake anasema kwamba, kwa miaka  sasa Shirikisho lao limeunganisha Vyama ambayo viko katika maeneo yote ya Italia kwa kujikita katika kupambana na utamaduni wa ubaguzi, wakikuza ushirikishi katika mazingira kwa kiasi kikubwa. Kazi hiyo ni ya muhimu anasema Baba Mtakatifu na kwamba, katika kuhakikisha ubora wa maisha ya watu viziwi na ili kushinda ulemavu huo kwa njia ya kuthamanisha ukuu wote, ukiwa pamoja na wa kiroho katika maono ya ufungamanisho wa kibinadamu. Watu viziwi wanaishi kwa hakika na hali ya udhaifu; lakini hii ni sehemu ya maisha anasema Baba Mtakatifu na ambayo inaweza kukubaliwa kwa uchanya. Kile ambacho siyo kizuri, lakini hasa kwa watu wengi wenye uwezo tofauti na familia zao, ni lile ambalo mara nyingi watu wanaishi kwa hali ya kuhukumu na wakati mwingine hata katika jumuiya ya kikristo, kama alivyokumbusha Rais wa Shirikisho hilo katika hotuba yake.

Inawezekana kuwasaidia hata viziwi msaada kamili ambao unazingatia mantiki ya maisha na hatua zake zote

Kutokana na hilo, Baba Mtakatifu anahimiza kwamba katika miji, nchi na maparokia ambamo huduma hizo hutolewa, wote wanaalikwa kushinda daima vizingiti ambavyo haviruhusu kupokea kwa nguvu zote uwepo hai wao na  kwenda zaidi ya mtazamo wa ulemavu huo. Viziwi hao, Baba Mtakatifu anafafanua, wanatufundisha kwamba, ni katika kushinda vizingiti tu na udhaifu, unaweza kweli kuwa mjenzi, pamoja na wahusiano na wanachama wote wa jumuiya ya raia na ile ya Kanisa, ya utamaduni wa makutano na kupambana dhidi ya  mivutano ya sintofahamu zilizoenea. Na kwa maana hiyo inawezekana kubadilisha jamii na jumuiya ili kuweza kuwasaidia hata viziwi kwa msaada kamili, ambao unazingatia mantiki ya maisha na hatua zake zote.

Baba Mtakatifu Francisko aidha anato sifa kwamba katika mantiki ya utamaduni na jamii ya sasa, hata viziwi ni zawadi ya Kanisa: fadhila ya Ubatizo waliyopokea, kila mjumbe wa watu wa Mungu anakuwa mfuasi wa kimisionari. Kila mbatizwa, mahali popote alipo, anafanya kazi katika Kanisa na uwezo wa kufundishwa katika imani yao ambayo ni jambo hai la uinjilishaji ( Wosia wa Evangelii gaudium,120). Kwa maana hiyo hata uwepo wa watu viziwi kati ya wahudumu wa kichungaji wanaunda kwa mujibu wa hali zao ule uwezo wa kuwakilisha rasilimali na fursa ya uinjilishaji. Baba Mtakatifu anawatakiwa hata wao wawe hai na kama alivyo kila mmoja mwanachama, na ili waweze  kushiriki kwa namna timilifu daima ya maisha yao katika  jumuiya yote ya Kanisa. Wanaweza kwa namna ya pekee kugundua na kuzaa matunda na talanta ambazo Bwana aliwapatia, katika Kanisa, ndani ya familia na kwa watu wote wa Mungu!

Uwepo wa Mungu hautambuliwi na masikio, bali kwa imani

Baba Mtakatifu anameeleza kuwa uwepo wa Mungu hautambuliwi na masikio, bali kwa imani; na kwa njia hiyo, anawatia moyo wa kupyaisha imani yao na kuhisi daima ukaribu wa Mungu, ambaye sauti inasikika ndani ya moyo wa kila mmoja na wote wanaweza kusikia. Wanaweza kuwasaidia wote ambao hawasikii sauti ya Mungu na kuwa makini kwa sauti hiyo. Hiyo ina maana ya kubwa ya kuchangia na ambayo kwa viziwi wanaweza kutoa maisha yaliyo hai kabisa kwa Kanisa. Baba Mtakatifu Francisko, amefikiria watu wengi viziwi nchini Italia na duniani Kote. Kwa namna ya pekee wale wanaoishi katika hali ya ubaguzi na umasikini. Anasali kwa ajili yao.

Anasali kwa ajili ya wote ili waweze kupata mchango wao wa dhati ndani ya jamii na kuwa na uwezo wa mtazamo wa kinabii, wenye uwezo wa kusindikiza michakato ya ushirikishwaji na upamoja, uwezo wa kushirikiana katika mapinduzi ya huruma kuu na ya ukaribu. Hata katika Kanisa kuna haja ya uwepo wao katika kuchangia na kujenga jumuiya ambayo nyuma yake kuna ukarimu, nyumba zilizo wazi kwa wote kuanzia na wale walio mwisho. Amewashukuru kwa ziara yao; anawatia moyo waendeleea na furaha katika safari yao na wakati huo huo akiomba wamsindikize hata yeye kwa sala. Amewabariki na Baraka Takatifu!

25 April 2019, 13:00