Vatican News
Tarehe 27 Aprili Papa amekutana na Marais wa Umoja wa Wilaya nchini Italia Tarehe 27 Aprili Papa amekutana na Marais wa Umoja wa Wilaya nchini Italia   (Vatican Media )

Papa Francisko:Wilaya ziwe msimamizi wa utunzaji wa nyumba yetu!

Tarehe 27 Aprili 2019,Baba Mtakatifu francisko amekutana na Marais wa Umoja wa Wilaya za Italia ambapo amesisitiza ulazima wa kufikiria shughuli za kukarabati na utunzaji hasa katika kuweka usalama wa mashule,barabara na mazingira.Mambo haya anasisitiza ni kitovu kinachostahili umakini zaidi.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Baba Mtakatifu Francisko amekutana na Marais wa Umoja wa Wilaya za Italia, tarehe 27 Aprili 2019. Anamshukuru rais wa Umoja huo kwa maneno ya hotuba yake ya kuwakilisha lengo la mkutano huo. Pia anawashukuru kwa ukarimu wa sadaka ambayo wameitoa katika mfuko wa Kitume, ambapo mchango huo  anasema ni kwa ajili ya kuwasaidia wenye kuhitaji.

Nyakati zetu zimetawaliwa na maendeleo ya haraka, teknolojia na sayansi

Pamoja na hayo Baba Mtakatifu anasema suala la mahitaji ndilo limempa fursa ya kuanza hotuba yake katika mantiki ya nyakati zetu, zenye tabia ya kuwa na maendeleo ya haraka na unyeti wa teknolojia na  kwa ajili ya mandeleo ya utafiti wa kisayansi katika dhana tofauti. Mambo haya yanaonekana kwamba sayansi, ufundi na uhuru wa kuanzisha mambo ndiyo yenye kuwa na  uwezo wa kutoa jibu katika mahitaji ya watu na katika jamii  ili  kuweza kuzuia kila tukio la kuacha wengine pembezoni kwa kutoa maisha ndani ya jamii ya umoja  na isiyo kuwa na umasikini wala ubaguzi.

Lengo hili linatakiwa kuwa la ushiriki kwa makundi na vyama vya kiraia 

Licha ya hayo yote, lakini Baba Mtakatifu anathibitisha kwamba, hali halisi inabaki kuwa ni ngumu. Kuongezeka kwa fursa hizo unakwnda kinyume na ongezeko la mahitaji ya kuweza kutosheleza hasa katika kambi ambazo lazima ziingiliwe kati kwa haraka. Ni matatizo ambayo yanastahili kufikiriwa na jitihada za nguvu zaidi na rasilimali ili kuchanganua uwezekano wa kupata suluhisho. Mbele ya faida na mambo mengine yaliyopo ya maendeleo, takwimu katika sekta tofauti zinaonesha kuwa bado kuna ongezeko la ukosefu wa uwiano sawa kwa wale ambao wapo pembeni  na ambao wanahitaji jitihda za kiakili na mshikamano kwa wote ili waweze  kukabaliana na hali zao. Lengo hili linatakiwa kuwa la ushiriki kwa makundi na vyama vya kiraia na wakati huo huo  kuwa na utambuzi na kuendelea na matendo tofauti kwa ngazi ambazo zinaweza kuunda uwezo mkubwa kwa umma ili kukimbilia mahitaji ya watu!

Wilaya ni kilele cha ngazi za umma

Baba Mtakatifu Francisko aidha anasema, Wilaya ni kilelelezo cha ngazi hizi ambazo zimeundwa na uwezo wa umma na zimejaa historia. Hizi zinazaliwa na muungano wa maeneo ambayo yanaundwa na historia na umaduni mmoja unaojieleza kwa miaka mingi na zenye uwezo wa kuwakilisha ulazima wa nchi  katika utawala, pamoja na kuendeleza tabia, uwezo maalum na mtindo tofauti katika  uchaguzi na usimamizi wake. Wao wanahamasisha kulinda sehemu mahalia kwa ajili ya Serikali, Bunge na nguvu za kiuchumi na kijamii, ili  kuunda jambo msingi la makubaliano na kuwa chachu zaidi ya matendo kwa ajili ya kusaidia wenye kuhitaji zaidi katika jumuiya mahalia.

Ulinzi wa ardhi na maeneo yote hatarishi

Dhama ya sasa katika Wilaya za Italia, Baba Mtakatifu anasema, zinajielezea kwa uwezo wake ambao ni msingi wa kutunza na kuingilia kati katika kulinda ardhi na uthibiti wa maeneo hatarishi, kama vile mtandao wa barabara ndogo ndogo na kubwa zinazo unganisha hadi kufikia  vituo vya miji mikubwa, hata usimamizi wa shule za sekondari kwa kuhakikisha usalama na uendeshwaji wake. Hiyo ni shughuli muhimu inayohitaji kuwajibika ili kuhakikisha kuwa hali ya mazingira ya eneo kama vile ya barabara na shule haviaribiki au kutojali kwa ajili ya ukarabati wake ili kuzuia madhara yake  ya mazingira na hatari zake. Inahitaji kuhusisha na kueneza uelewa zaidi wa  mazingira. Hata kwa wazalendo wote wanaowakilishwa katika taasisi il kutambua umuhimu wa kutunza nyumba ya pamoja katika mantiki yake.

Watambue taifa ambalo kwa hekima ya kuwekeza fedha na rasilimali za binadamu 

Baba Mtakatifu aidha anawakumbusha kwa jinsi gani wao wanajua umuhimu wa kupanga kwa pamoja na kuongeza mipango na sera za kisiasa badala ya kukuza utelekezaji wa maeneo na  ili kutunza mazingira yote ya kihistoria. Aidha wao wanatambua umuhimu wa shule na barabara zake ili kuhakikisha maisha ya taifa na kama ilivyo kwa kila maendeleo bora. Wao wanatambua ni kwa jinsi gani wanaweza kuwa taifa ambalo kwa hekima ya kuwekeza fedha na rasilimali za binadamu ili kuwa na usimamizi na kuzuia uharibifu. Baba Mtakatifu anahitimisha kwa kuwatakia wote wafuate njia hiyo kwa ujasiri na msimamo thabiti wa kazi yao kwa namna ya kufanya ili Wilaya zao ziwe vituo vya dhati na vyenye kuwa na mawazo ya kupendekeza malengo ya maendeleo endelevu na kujiwekea pamoja mtandao wa mahusiano yanayoundwa na asili, historia, kazi za kizazi na kizazi kilichotangulia.

27 April 2019, 13:58