Tafuta

Vatican News
Papa Francisko akiwa katika tendo la kupaka mafuta ya krisma,altare ya Parokia ya Mtakatifu Giulio wakati wa ziara yake ya kichungaji Dominika tarehe 7 Aprili 2019 Papa Francisko akiwa katika tendo la kupaka mafuta ya krisma,altare ya Parokia ya Mtakatifu Giulio wakati wa ziara yake ya kichungaji Dominika tarehe 7 Aprili 2019  (REMO CASILLI)

Papa Francisko atabaruku Altare ya Parokia ya Mtakatifu Giulio,Roma!

Baba Mtakatifu Francisko amethimisha Misa ya kutabaruku altare baada ya kutembelea na kuona hali halisi ya Parokia ya Mtakatifu Giulio huko Monteverde,Roma,kukutana na kuzungumza na watoto na vijana,watu wa kujitolea na wajenzi wa ukarabati wa Kanisa pamoja wagonjwa na wazee.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Baada ya mikutano na makundi mbalimbali ya Parokia ya Mtakatifu Gulio na kuungamisha baadhi ya watu, Baba Mtakatifu Francisko Jumapili, tarehe 7 Aprili 2019, ameongoza liturujia ya kutabaruku Altare ya Kanisa hili pamoja na kuadhimisha mafumbo ya Kanisa. Ni maadhimisho yenye utajiri mkubwa  wa liturujia lakini hakufanya mahubiri. “Piteni katika Malango ya Bwana kwa utenzi wa neema na nyimbo za shukrani, ndiyo maneno aliyotamka Baba Mtatifu Francisko wakati wa kufungua Mlango wa kuingia katika Kanisa la Mtakatifu Giulio, huko Monteverde, ikiwa ni parokia ya 19 alizotembelea tangu kuanza huduma yake ya kichungaji kama khaarifa wa mtume Patro. Hili ni Kanisa lililokarabatiwa na kufunguliwa mara baada ya miaka 3. Baba Mtakatifu kabla ya kuanza misa takatifu, kama kawaida yake amweza kuwaungamisha vijana watatu na mama mmoja.

Papa hakutoa mahubiri

Katika liturujia ya kutabaruku Altare,wamenyunyizia maji na baadaye ya kusomwa Injili, na  Baba Mtakatfu Francisko hakutoa mahubiri, badala yake amebaki kwa kimya cha sala akiwa ameinamisha kichwa chake.  Baada ya sala ya Nasadiki ambayo ni imani ya kikristo na kusoma litania  ya watakatifu, wameweka chini ya altare Masalia ya watakatifu ya Mtakatifu Yohane Bosco, Margherita Maria Alacoque pamoja na Mtakatifu Maria Goretti. Hii yote imewezekana kutokana na wanaparokia kushirikiano kwa pamoja kwa mika mitatu ili kukamilisha ukarabati wa Kanisa hili kwani paa liliporomoka na kuharibi Altare hiyo.

Maji, mafuta na mwanga

Mafuta ya krisma yaliyo barikiwa  yametumika kupataka altare nzima ya Kanisa la Mtakatifu Giulio. Mikono yake imegusa jiwe kubwa na ambalo ni msingi hakika, unaokumbatia meza ambayo inatoa sadaka ya Ekaristi. Vile vile amefukizia ubani, na arufu ikajaza Kanisa, kama harufu ya Kristo ambayo Kanisa linaitwa kueneza ulimwenguni kote. Altare hiyo aidha  imefunikwa na kitambaa cheupe lakini kikiwa juu na  mwanga wa mishumaa, ambayo inataka kutafakari mwanga wa dunia ambao Yesu, anaungaza kwa watu wote. Baadaye vimeletwa vipaji, kwa Baba Mtakatifu ambavyo ni  maji na divai, mkate na kuongeza kikapu cha matunda. Mwisho wa maadhimisho hayo, Paroko wa Parokia ya Mtakatifi Giulio, padre Dario Frattini mwanashrika wa Bikira Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili ameelezea furaha yao kwa niaba ya jumuiya nzima kutembelewa na Baba Mtakatifu Francisko. Amemwahidi kumsindikiza Baba Mtakatifu kwa sala za kila siku.

Paroko ametoa shukrani kwa Papa kuitembelea parokia  

Anamshukuru kwa zawadi ya kufika na zaidi ya kutabaruku Kanisa na Altare. Kabla ya ziara hiyo, amethitisha kwamba wamejandaa kwa sala na kwa maana wao ni watu  wa Mungu  ambao wako katika mchakato wa  safari kuelekea kwa Bwana. Zawadi ya Parokia kwa Baba Mtakatifu ni mchango mdogo ulio kusanywa kwa wiki nne za Kwaresima kwa ajili ya Caritas . Huu ni mpango wao kwa ajili ya watu wasio kuwa na makazi.

08 April 2019, 10:00