Papa anasema kukaa kimya,unyenyekevu na kushinda vishawishi vya ushindani wa ibilisi ili kuweza kufikia wokovu wa Ufalme wa Mungu Papa anasema kukaa kimya,unyenyekevu na kushinda vishawishi vya ushindani wa ibilisi ili kuweza kufikia wokovu wa Ufalme wa Mungu 

Papa Fancisko katika Jumapili ya Matawi amehimiza kuiga ukimya wa Yesu!

Baba Mtakatifu ameongoza maandamano na maadhimisho ya Jumapili ya Matawi tarehe 14 Aprili 2019 katika Uwanja wa Mtakatifu Petro.Katika mahubiri yake,anashauri kufuata mfano wa Yesu, kukaa kimya,unyenyekevu na kushinda vishawishi vya ushindani wa ibilisi ili kuweza kufikia wokovu wa Ufalme wa Mungu.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Tarehe 14 Aprili 2019 ambayo Mama Kanisa anaadhimisha siku ya Matawi, ikiwa ni mwanzo wa Juma Kuu Takatifu la Mateso, Kifo na Ufufuko wa Bwana, Baba Mtakatifu Francisko ameongoza maandamano na maadhimisho ya Jumapili ya Matawi tarehe 14 Aprili 2019 katika Uwanja wa Mtakatifu Petro Vatican. Katika mahubiri yake anashauri kufuata mfano wa Yesu, kukaa kimya, unyenyekevu na kushinda vishawishi vya ushindani wa ibilisi ili kuweza kufikia wokovu wa Ufalme wa Mungu. Mara baada ya masomo yote ya siku Baba Mtakatifu ameanza  kusema: ni shangwe za kuingia katika mji wa Yerusalemu na unyenyevu wa Yesu. Sauti za shangwe na hasira za watu. Mafumbo haya mawili ndiyo yanasindikiza kila mwaka  katika  kuingia Juma Kuu Takatifu,katika sehemu hizi mbili zinazoongozwa na tabia ya maadhimisho haya. Yaani maandamano na matawi ya mitende na mizeituni tangu mwanzo na baadaye kusikiliza somo linalosimulia mateso hayo. Tuache tuhusishwe na matendo hayo yanayoongozwa na Roho Mtakatifu, ili kuweza kuona kile  ambacho tumeomba katika sala. Bwana wetu Mkumbozi atusindikize kwa imani katika njia yake na uwepo wake daima katika mafundisho yake makuu ya mateso kama mtindo wa maisha na ushindi dhidi ya roho ya ubaya. Anasema Baba Mtakatifu.

Tangu mwanzo wa siku arobaini hadi mwisho Yesu anasukumiza mbali kishawishi

Yesu anatuonesha namna ya kikabiliana na wakati mgumu na vishawishi zaidi vinavyo tusonga, kwa akituhifadhia moyo wa amani ambayo haiko mbali, haipitiki  au kuwa ya  juu zaidi, bali yenye kujiachia kwa imani ya Bwana na mapenzi yake ya wokovu, wa maisha, wa huruma; na  zaidi yeye katika  utume wake wote, amepitia katika njia ya vishawishi na kufanya kazi yake ya kumchagua Yeye kwa namna ya kuweza kutufungamanisha na utii wa Baba. Tangu mwanzo katika mapambano kwa siku arobaini katika jangwa hadi mwisho katika mateso Yesu anasukumia mbali na kishawishi hiki kwa imani kwa njia ya nyenyekevu katika Baba. Hata leo hii, Baba Mtakatifu Francisko anasema kuwa, kuingia katika Yerusalemu, Yeye anatuonesha njia. Kwa sababu katika tukio lile la ubaya, Mfalme wa dunia hii alikuwa na karata ya kucheza: Karata ya ushindi na Bwana alimjibu kwa kubaki thabiti katika imani katika njia yake na njia ya unyenyekevu. Baba Mtakatifu anabainisha kwamba, ushindani unatatufa kukaribia ushindi kwa njia za mikato, za uongo na ahadi. Ni kutazama kupanda juu ya gari la mshindi. Mshindani anaishia kwa ishara na maneno, lakini ambayo hayakupitia katika mateso ya msalaba; anajikuza kwa kujilinganisha na wengine akiwahukumu daima walio wabaya, wenye makosa, na walioshindwa… Mitindo  ya kichini chini ya mshindani ni roho ya kiulimwengu na ambayo ni mbaya sana na hatari, ni vishawishi zaidi vya ulaghai vinavyotishia  Kanisa ( De Lubac). Yesu anajaribu ushindani kwa njia ya Mateso yake.

Ki ukweli Bwana alishirikisha na kufurahi na watu, akiwa na vijana walio kuwa wakipaza sauti

Ki ukweli Bwana alishirikisha na kufurahi na watu, akiwa na vijana walio kuwa wakipaza sauti kwa jina lake na mkutakuza Mfalme na Massia. Moyo wake ulikuwa unafurahi kuona shauku na sikukuu ya masikini wa Israeli. Hadi kufikia mfalisayo kuomba awakaripie mitume wake kwa ajili ya kashfa ya kutangaza hivyo na Yeye aliwajibu:“Kama hawa akinyamaza, mawe yatapasa sauti”( Lk 19,40) Unyenyekvu hauna maana ya kukataa hali halisi na Yesu ni Masiha na Mfalme wa kweli. Lakini wakati  huo huo Moyo wa Yesu ulikuwa katika njia nyingine , katika njia takatifu ambayo yeye Peke yake na Baba walikuwa wanatambua; Njia ambayo inatoka katika “hali ya kuwa Mungu” na kuingia kuwa katika “hali ya mtumishi”, njia ya “unyenyekevu katika utii hadi kifo na kifo cha msalaba”.(Fil 2,6-8) Yeye anatambua kwamba ili kuweza kufika katika ushindi wa kweli, lazima kutoa  nafasi kwa Mungu; na ili kutengeneza nafasi ya Mungu, kuna aina moja tu ambayo ni kujivua, na kujikana binafsi. Kukaa kimya, kusali na kunyenyekea. Hakuna mjadala katika Msalaba au ni kuukumbatia au kuukataa. Kwa njia ya unyenyekevu wake Yesu alipenda kutufungulia sisi njia ya imani na kututangulia katika njia hiyo.

Nyuma yake Yesu alikuwapo Mama yake Maria

Baba Mtakatifu anasema kuwa, nyuma yake  ambaye alikuwa wa kwanza kuipitia njia alikuwa Mama yake Maria, ndiye mfuasi wa kwanza. Bikira Maria na watakatifu ambao waleweza kutesaka kwa kutembea katika Imani na  katika mapenzi ya Mungu. Mbele ya matukio magumu na machungu ya maisha,  kujibuakwa imani inayo gharimu kwa namna ya pekee ugumu wa moyo ( Mt. Yohane Paulo II katika Waraka wa Redemptoris Mater, 17). Ni usiku wa imani Baba Mtakatifu anabainisha. Lakini ni kwa njia tu ya usiku wa imani, jua la ufufuko litachomoza. Chini ya miguu ya Msalaba, Maria alifikiri maneno ambayo aliambiwa na Malaika kuwa mwanao “atakuwa mkuu (…); Bwana Mungu atampatia kiti cha Daudi baba yake na atatawala milele katika nyumba ya Yakobo na ufalme wake hautakuwa na mwisho “(Lk 1,32-33). Maria akiwa juu ya Golgota alijikuta mbele ya uongo kwa ujumla, kuhusiana na ahadi ile. Kwa maana Mtoto wake yupo na maumivu makali sana juu ya msalaba kama jambazi. Na hivyo ushindani, ulioharibiwa na unyenyekevu wa Yesu ndiyo ulikuwa na uharibifu wa moyo wa Mama; wote wawili walitambua kunyamaza.

Siku ya vijana duniani kwa ngazi ya kijimbo

Wakitatanguliwa na Maria, idadi kubwa ya watakatifu wa kike na kiume wamefuata Yesu katika njia ya unyenyeve na utii Baba Mtakatifu Francisko amethibitisha. Leo hii ikiwa ni Siku ya Vijana duniani Baba Mtakatifu Francisko amependa kuwakumbuka watakatifu wengi wa kike na kiume vijana, kwa namna ya pekee  anasema wale ambao wanaishi “milango ya jirani”, ambao ni Mungu peke yake anawatambua, na mara nyingi amesisitiza Baba Mtakatifu, Yeye anawapenda na kutuonesha kwa njia ya  mshangao. Kutokana na hilo, anasema: Vijana wasiwe na aibu ya kuonesha kwa Kristo, shauku yao na kushangilia kuwa Yeye anaishi, na kwamba yeye yupo katika maisha yao. Na wakati huo huo wasiwe na hofu ya kufuaa katika njia ya msalaba. Iwapo watahisi kuwa anawaalika kuacha yote, katika kuvua usalama wao, basi wawe na imani dhabiti na kujikabidhi kwa Baba ambaye yuko mbinguni, na kwa maana hiyo wasifu na kushangilia! Baba Mtakatifu ameongeza: “ mko katika  njia ya Ufalme wa Mungu!

Shangilio la sikuu na hasira

Baba Mtakatifu akiendelea anasema shangilio la sikukuu na hasira ni ajabu ya ukimya wa Yesu katika Mateso yake, Yeye anaacha hata kile kishawishi cha kujibu. Katika kipindi hiki cha  mahangaiko, inabidi kunyamaza, kuwa na ujasiri wa kunyamaza, japokuwa ukimya uwe wa unyenyekevu pasipo kinyongo. Upole wa ukimya utatufanya kuonesha kuwa wadhaifu zaidi, wanyenyekevu zaidi, na ndipo shetani atafichuka na kuonekana wazi, Baba Mtakatifu anasisitiza. Lakini hiyi inahitaji kuvumilia katika ukimya, kubaki na msimamo, lakini wakati huo huo ndiyo tabia ya Yesu. Yeye anatambua kuwa, vita kati ya Mungu na Mfalme wa ulimwengu huu na havipo ili uchukue silaha mkononi, bali ni kubaki na utulivu na kuwa na  msimamo katika imani. Ni katika saa ya Mungu na katika saa ambayo Mungu atatelemka katika uwanja wa mapambano na lazima kumwacha afanye hivyo. Na nafasi yetu ya usalama itakuwa chini ya vazi la Mama Mtakatifu wa Mungu. Na wakati tunasubiri Bwana arudi  ili kutuliza dhoruba (Mk 4,37-41), kwa ukimya wetu wa ushuhuda katika sala, tujikabidhi sisi na wengine  katika sababu ya matumaini yaliyomo ndani mwetu (1 Pt 3,15). Hii itatusaidia anathbitisha Baba Mtakatifu, kuishi katika mivutano kwenye kipindi hiki kitakatifu cha kumbu kumbu za ahadi na hali halisi ya kelele zilizopo katika msalaba na matumaini ya ufufuko.

14 April 2019, 12:07