Tafuta

Vatican News
tarehe 11 Aprili,Baba Mtakatifu amekutana na washiriki wa Mkutano wa kimataifa kuhusu biashara ya binadamu  tarehe 11 Aprili,Baba Mtakatifu amekutana na washiriki wa Mkutano wa kimataifa kuhusu biashara ya binadamu   (Vatican Media)

Papa:Biashara ya binadamu ni uhalifu dhidi ya ubinadamu!

Tarehe 11 Aprili,Baba Mtakatifu Francisko amekutana na washiriki wa Mkutano wa kimataifa kuhusu bishara haramu ya watu,ulioandaliwa na Kitengo cha Wahamiaji na Wakimbizi cha Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo fungani ya binadamu.Japokuwa na juhudi nyingi zilizo tendeka,bado kuna kazi kubwa ya kufanya amesema.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Baba Mtakatifu Francisko amekutana na washiriki wa Mkutano wa kimataifa kuhusu biashara ya binadamu. Akianza hotuba yake, amewakaribisha  wote wakati wa furaha hiyo ya kuhitimisha mkutano wao unaojikita katika hali halisi ya Mwongozo wa  Kichungaji kuhusu biashara wa binadamu na ambapo mwongozo huo ulitangazwa  na Kitengo cha Wahamiaji cha Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo fungamani ya binadamu kwa idhidi ya  Baba Mtakatifu. Amemshukuru P. Michael Czerny kwa ajili ya hotuba yake kwa niaba ya washiriki wa mkutano huo.

Mimi nilikuja ili wote wawe na maisha tele

“Mimi nilikuja ili wote wawe na maisha na maisha tele” ( Yh 10,10). Katika sentensi hii ya Injili ya Yohane, Baba Mtakatifu anasema, inajikita katika utume wa Yesu Kristo wote, ili kuwapa wanaume na wanawake wa kila wakati maisha kamili, kwa mujibu wa ishara za Baba. Mwana wa Mungu alijifanya mtu ili kuwaelekeza watu wote safari ya kukamilisha utu wao kwa mujibu wa umoja na usioweza kurudia kwa kila mmoja. Baba Mtakatifu Francisko, hata hivyo anabainisha kuwa, kwa bahati mbaya katika dunia ya sasa, ni huzuni mkubwa unaojionesha ha hali zenye vizingiti vya kutoweza  kikamilisha utume huo. Kama inonavyoonesha Mwongozo wa Kichungaji juu ya Biashara ya Binadamu, kwamba “ katika kipindi ambacho kimesambuliwa na ongezeko la umimi na ubinafsi, ni katika tabia inayozidi kukua na kufikiriwa na wengine kwa mantiki ya kujinufaisha na kuwapa thamani katika mantiki na vigezo vya urahisi na faida binafsi (n.17

Hizi ni tabia ambazo za biashara ya kuuza mwingine na mbayo Baba Mtakatifu mara nyingi amweza kuelezea. Kati ya kipeo kikubwa sana cha biashara hii, kinazidi kuonekana kwa upya katika biashara ya binadamu. Tabia hizi zinazojionesha na mitindo  mingi kwa dhati zinaleta majeraha ya mwili wa binadamu wa sasa, na kidonda cha kina cha kibinadamu , kwa yule anaye athirika, lakini pia hata anayetenda. Biashara kwa hakika inaharibu ubinadamu wa mwathirika, na kuharibu uhuru wake na hadhi yake. Na wakati huo huo inaondolea ubinadamu kwa yule anayetenda kwa kumkatalia kupata maisha tele. Hatimaye, biashara ya hiyo ina uharibifu mkubwa wa wanadamu kwa ujumla wake na kuangamiza familia ya kibinadamu na Mwili wa Kristo. Biashara ya binadamu aidha haiwezi hata kidogo kuwa na haki kwa maana ya kukiuka uhuru na hadhi ya mwathirika, katika ukuu wake wa kuwa binadamu aliyetamaniwa na kuumbwa na Mungu. Kwa maana hiyo huo  ni uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Anayetenda uhalifu huo dhidi ya binadamu anajiharibu mwenyewe pia

Tabia hizo kwa mfano, zinapaswa kuhukumiwa, kwa maana zinadharau uhuru na hadhi ya kila mwanadamu,wawe wazalendo wa nchi au mgeni. Anaye jichafua kwa uhalifu huo anaweka hasara kwa wengine, lakini hata mwenyewe. Kwa hakika kila mmoja wetu ameumbwa kwa ajili ya kupenda na kumsadia mwingine. Hiyo inamfanya afikie kujitambua. “Hakuna upendo ulio mkubwa kama huo, wa kutoa maisha yake kwa ajili ya marafiki “( Yh 15,13). Katika uhusiano ambao tunaufanya na wengine tunacheza na ubinadamu wetu, kukaribiana au kwenda mbali na mtindo ambao ulipendwa na Mungu na kuoneshwa na Mwanaye aliyejifanya mtu.  Kwa maana hiyo kila aina ya uchaguzi kinyume na ukamilisho wa Mpango wa Mungu juu yetu ni kusaliti ubinadamu wetu na kukataa maisha yaliyo tele ambayo yaliyotolewa na Kristo. Ni kushuka ngazi katika mtelemko, kwenda chini na kuwa mnyama. Kila aina ta tendo linalojikita kukarabati na kuhamasisha ubiadamu wetu na ule wa wengine, ndiyo mstari kiongozi wa utume wa Kanisa, ambao ni mwendelezo wa utume wa wokovu wa Yesu Kristo.  Na Umisionari huo unajionesha katika mapambano dhidi ya kila mtindo wa biashara ya binadamu,na katika jitihada za kuendelea kuwasaidia waathirika; mapambano na jitihada ambazo zinamwezesha kumfungulia njia ya kuelekea katika ukamilifu wa maisha na ndiyo hatima ya mwisho wa maisha yetu.

Mapambano dhidi ya biashara ya binadamu inaendelea lakini bado ipo kazi kubwa

Baba Mtakatifu Francisko anawapongeza kwa ishara hiyo ya dhati katika juhudi ambazo Kanisa mahalia kwa ukarimu wao wameonesha kwa mantiki ya kichungaji. Ni kazi inayostahili kusifiwa na idadi kubwa ya mipango iliyo anzishwa na ambayo wao ndiyo wako msatari wa mbele katika kuzuia biashara ya binadamu na kulinda waathirika na kuwafuatiliwa wahalifu. Baba Mtakatifu amehisi ameonesha shukrano kubwa kwa mashirika mengi ya kitawa ambayo yamefanya kazi kubwa na wanaendelea kufanya hiyo huduma, hata kufanya mtandao kati yao, kama “Mlinzi “ wa matendo ya kimisionari katika Kanisa, dhidi ya mapambano ya kila  aina ya mitindo ya biashara ya binadamu. Wamefanya, na wanaendelea kufanya zaidi lakini, bado kuna mambo mengi ya kufanya. Mbele ya matukio hayo magumu yenye giza kama la biashara ya binadamu ni msingi kuhakikisha uratibu wa mipango ya kichungaji , kwa ngazi mahalia na pia kimataifa. Ofisi zilizo pendekezwa na Kanisa mahalia, Mashirika ya Kitawa, na vyama katoliki vinaalikwa kushirikishana uzoefu na utambuzi, kadhalika kuunganisha nguvu katika matendo ya kimkakati na mbayo inaungwa mkono na nchi asili, mhali msafara unatoka na watu waathirika wanapo pelekwa.

Ili kupamba na janga hili lazima kushirikiana na wengine, wadau wa kisiasa na kijamii

Ili kuweza kujikita kwa dhati katika, matendo  ya Kanisa, lazima yatambue kushirikiana na msaada wa wengine, kama vile  wakala  na wadau wa  kisiasa na kijamii. Utaratibu wa ushirikiano unaoandaliwa na taasisi na mashirika mengine ya kiraia yatahakikisha matokeo mazuri zaidi yanayo onekana na ya kudumu. Amewashukuru kwa moyo wote kwa kile ambacho tayari wamefanya kwa ajili ndugu kaka na dada waathirika, na  wasio kuwa na hatia katika hii biashara ya binadamu. Anawatia moyo wa uvumilivu katika utume huo wa hatari, usiojulikana, lakini ndiyo kwa dhati ushuhuda wa kujitolea bure. Ni lazima kusisitiza kwa sababu ndiyo ukweli. Kwa njia ya maombezi ya Mtakatifu Josephina Bakhita ambaye alifanya uzoefu wa utumwa akiwa mtoto, alinunuliwa na kuuzwa huku na kule, lakini baadaye akakombolewa na sasa anachanua katika ukamilifu, kama mwana wa Mungu. Baba Mtakatifu amewabariki kwa baraka tele wote ambao wanaendelea na mapambano dhidi ya biashara ya binadamu na utumwa na kuwahidia kuwaombea katika sala zake.

 

11 April 2019, 13:52