Papa anasema shule lazima itambue kukaa kama meko ya mfua chuma ili kuhamasisha ushirikishwaji, heshima ya utofauti na mazungumzo kati ya tamaduni zote Papa anasema shule lazima itambue kukaa kama meko ya mfua chuma ili kuhamasisha ushirikishwaji, heshima ya utofauti na mazungumzo kati ya tamaduni zote 

Papa amewasihi wanafunzi wawe wakarimu na simu za mikononi zisiwe kama dawa ya kulevya!

Baba Mtakatifu Francisko amekutana na wanafunzi wa Sekondari ya Viscont mjini Roma na kusisitiza kuwa iwapo hakuna uhuru hakuna elimu na wala wakati ujao.Kadhalika simu za mkono zisigeuke kuwa kama dawa ya kulevya kwa kupunguza mawasiliano ya dhati kati yao na watu wengine!

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Tarehe 13 Aprili 2019, Baba Mtakatifu Francisko amekutana jini Vatican na wanafunzi wa Sekondari ya Viscont ya Roma. Amewakabidhi zoezi la  kupeleka mbele hali halisi ya kihistoria na kijamii inayoongozwa na shauku za kutaka kujua zaidi na kwa ajili ya utamaduni. Baba Mtakatifu katika hotuba yake amesisitiza kwamba shule, lazima itambue kukaa kama meko ya mfua chuma ili kuhamasisha ushirikishwaji, heshima ya utofauti na mazungumzo kati ya tamaduni zote, aidha amewasisitizia vijana wasiwe watumwa wa simu za mkononi.

Uhuru na wakati endelevu

Akiendelea  na hotuba yake amesema thamani ya  kidugu inajikita juu ya uhuru, kwa  kutafuta kwa dhati ukweli; juu ya kuhamasisha haki na mshikamano, hasa mbele ya watu walio wadhaifu. Kwa namna hiyo ukosefu wa usawa, unatokana na ukosefu wa kukabilianana kwa pamoja, na  ndipo inatokea ongezeko la chuki. Baba Mtakatifu anasema: “unapokosa uhuru, hakuna elimu na hakuna wakati endelevu. Iwapo hakuna suala la kutafuta ukweli wa dhati, na wakati huo huo kukimbilia kutafuta ukweli ambao unaondolea uwezo wa kutafuta ukweli wa dhati, ni wazi kwamba hakuna hata wakati endelevu. Kwani ni sawa na kukuondolea ubinadamu”.

Kati kati ya ukimya na mawasiliano

Baba Mtakatifu Francisko kwa wanafunzi hawa pia ametoa ushauri kwamba  wawe makini hasa katika kusikiliza sauti za dhamiri yao, ili wasije geuzwa kuwa kama karatasi ambayo mara moja hupeperushwa na upepo kutoka sehemu moja hadi nyingine. Na zaidi amewashauri wasiwe na woga wa ukimya.  Baba Mtakatifu anasema: “ni kwa njia ya ukimya wa ndani ya moyo yao wanaweza kutambua sauti ya dhamiri  na  kuweza kujua kung'amua kati ya sauti za ubinafsi, nzuri na zile za kupinga nafsi nzuri. Na kwa maana  hiyo anawaalika ili kujikomboa dhidi ya simu za mikono na mambo mengine ambayo vijana wanapendelea japokuwa ni yale yasiyo kuwa na msingi katika maisha.

Ufafanuzi juu ya simu za mkono kwamba ni nzuri zikitumiwa vizuri

Akifafanua suala la simu ya mkono, Baba Mtakatifu anasema: " simu za mikononi ni kwa ajili ya kuwasiliana. Lakini hiyo isiwe kama vile ni dawa ya kulevya au kugeuka kuwa mtumwa". Simu ya mkono wakati mwingine inapunguza mawasiliano ya kuzungumza na watu kwa urahisi na moja kwa moja. Hata hivyo amethibitisha kwamba, “maisha, siyo suala la kutafutana tu, bali ni kuwasiliana kwa dhati.  Simu ya mkono ikitumika vizuri ni msaada mkubwa na wa maendeleo; lakini inapaswa kutumiwa vizuri, ni vema kwa watu wote kuitumia. Anazidi kusisitiza:"unapogeuka kuwa mtumwa wa simu, unapoteza uhuru". Aidha, " Simu ya mkono ni kwa ajili ya kutoa taarifa na kuwasiliana". "Ni jambo zuri kuwasiliana kati yetu, lakini zaidi ni kuwa makini kwa maana ipo hatari kama dawa ya kulevya  amerudia kusisitiza kwa kizazi hiki cha vijana, walimu wao, wazazi wao wakiwa katika ukumbi wa Paulo VI mjini Vatican.

Kuwa na uwezo wa kupenda

Baba Mtakatifu Francisko akiendelea na hotuba yake amewaelekeza vijana juu ya aina mbili za ukuu wa maisha katika mahusiano. "Kujisetiri" na "uaminifu". Ni lazima kupenda kwa moyo mpana kila siku na siyo tu kwa mtazamo wa kijuu juu na kubaki waaminifu, kwa sababu upendo siyo suala la mchezo. Upendo ni jambo zuri sana na ambalo Mungu alitupatia. Upendo unafungua moyo kuwa mpana. Upendo siyo tu kielelezo cha mfungamo wa kupendana kati ya  wachumba au urafiki wa nguvu. Muundo wa upendo unaweza kuonekana hata kwa njia za jitihada za mshikamano kuzielekeza kwa jirani na zaidi maskini. Upendo wa jirani unajionesha katika ubunifu, daima unakwenda zaidi ya... Inakuwa kitu cha kusaidia na kwenda mbele. Ubunifu wa upendo ndiyo jambo mwafaka na hivyo Baba Mtakatifu amewahimiza wasiogope hilo!

Ushindi kwa njia ya ukarimu

Baba Mtakatifu Francisko kadhalika ameshutumu vikali kuhusu janga kubwa jamii Italia la ugomvi wa vijana mashuleni, hasa kuwaonea walio wadhaifu na amewakumbusha suala la  kujitolea na kwamba ni jambo zuri sana, lenye nguvu ambalo  lipo nchini Italia. Kutokana na hilo anatoa ushauri kwao kujiunga ili kujitolea na kwa njia ya ukarimu. Kwa kuhitimisha, amewashauri wanafunzi hao wasiache kuota ndoto ya mambo makubwa, kuota vitu vikubwa! Hili ni jambo jema kwa vijana anasema Baba Mtakatifu, yaani kuota yaliyo makubwa na kuwa na shauku ya ulimwengu ulio bora zaidi kwa wote. Amewashauri wasiridhike na uhusiano usio na mshiko kati yao, badala yake wajaribu kutunza mambo msingi ya undani katika kupanga  na  mipangilio ya wakati wao endelevu, ambapo ni katika  jitihada za ulimwengu wa haki zaidi na mzuri.

 

 

 

13 April 2019, 14:10