Vatican News
Baba Mtakatifu amekabidhiwa na mtoto wa miaka minne aliyepona na saratani mbaya Kijiti kwa ajili ya matumaini Baba Mtakatifu amekabidhiwa na mtoto wa miaka minne aliyepona na saratani mbaya Kijiti kwa ajili ya matumaini  

Mtoto wa miaka 4 amkabidhi Papa ushuhuda wa kijiti cha matumaini!

Mara baada ya Katekesi ya Papa Francisko mtoto wa miaka 4 aliyepona na saratani mbaya,amemkabidhi ushuhuda wa kijiti kwa ajili ya matumaini.Je kinahusika na nini?

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Katika katekesi ya Baba Mtakatifu Francisko, trehe 24 Aprili 2019 wameshiriki pia uwakilishi wa mashindano ya marathon ikiongozwa na kaulimbili: “Kijiti cha  matumaini. Hizi ni mbio za marathon kwa ajili ya ufadhili wa watoto na vijana wa Italia walio na saratani ya damu, saratani kwa ujumla na magonjwa nadra. Mbio hizo za mshikamano zimeanza tarehe 21-24 Aprili 2019, ambapo  wamezungukia mikoa mitano ya Italia (Veneto, Emilia Romagna, Marche, Umbria na Lazio) na kuongeza km 530 kutoka Padova hadi mji wa Vatican, katika uwanja wa Papa Pio XII.

Mtoto wa miaka 4 aliyepona na saratani mbaya

Kufuatia na tukio hilo, hata mtoto wa miaka 4 aliyepona na  saratani mbaya ameweza kumkabidhi Baba Mtakatifu ushuhuda wa kijiti cha  Matumaini. Hata hivyo pia uwakilishi wa mbio umemkabidhi Baba Mtakatifu Francisko bahasha iliyokuwa na ujumbe wa watoto kuanzia miaka 8-13 ambao kwa sasa wako katika tiba na mmoja mwenye miaka 25 ambaye amepona na kumkabidhi pia bango kubwa lililokuwa limeandikwa “mji wa Matumaini” unaojihusisha na Chama kinacho jikita na  shughuli hiyo ya ufadhili ambapo pia Baba Mtakatifu Francisko ametia sahini katika baadhi ya  jezi za wanariadha, hata wanariadha wote ambao wameshiriki marathon hiyo!

Salam kwa mahujaji

Baba Mtakatifu Fracisko pia baada ya katekesi yake amewasalimia waamini na mahujaji kutoka pande zote za dunia, kwa namna ya pekee vijana kutoka Jimbo Kuu Katoliki la Milano nchini Italia waliosindikizwa na Askofu  Mkuu Mario Delpini, mapadre na walimu wao. Anawatakia wakue katika imani na upendo kwa kujikita zaidi katika kuonesha matunda yaliyo mema. Injili anasema, iwe ndiyo Kanuni ya maisha yao na kama ilivyokuwa kwa watakatifu wao Ambrosi na Karoli, ambao kwa upendo wao mkubwa, walibadilisha dunia. Vile vile kama kawaida yake wazo limewaendea vijana wote, wazee, wagojwa na wanandoa wapya. Na kwa  watu wote wanatakia furaha na matumaini yatokanayo na Pasaka ya Kristo. Ili waweza kufanya uzoefu wa Yesu alie hai na  kupokea zawadi ya amani yake na kugeuka kuwa mashuhuda wake duniani.

24 April 2019, 14:01