Baba Mtakatifu Francisko ameidhinisha toleo la marekebisho ya sheria za ziada kuhusu “Anglicanorum coetibus" Baba Mtakatifu Francisko ameidhinisha toleo la marekebisho ya sheria za ziada kuhusu “Anglicanorum coetibus" 

Miaka kumi baada ya kutangazwa kwa Katiba ya Kitume ya Anglicanorum coetibus

Miaka 10 baada ya kutangazwa kwa Katiba ya Kitume ya Anglicanorum coetibus,Baba Mtakatifu Francisko ameidhinisha toleo la marekebisho ya sheria za ziada

Katiba ya Kitume ya  Anglicanorum coetibus, iliyotolewa na kutangazwa kunako tarehe 4 Novemba 2009 na Baba Mtakatifu msataafu Benedikto  XVI, inatoa kanuni inayozingatia kuanzishwa kwa hati binafsi kwa waamini wa kianglikani,ambao wanataka kuingia moja kwa moja katika muungano wa Kanisa Katoliki.Kutokana na hiyo, ni miaka 10 baada ya kutangaza Katiba ya Kitume ya Anglicanorum coetibus,Baba Mtakatifu Francisko ameidhinisha toleo la marekebisho ya sheria za ziada.

Maagizo ya binafsi

Katika Katiba hiyo imethibitishwa kwamba, Maagizo ya kawaida binafsi ya waanglikani wanaoingia moja kwa moja ili kushiriki kikamilifu na Kanisa Katoliki wanachaguliwa na Baraza la Kipapa la Mafundisho tanzu ya Kanisa, ndani ya mipaka ya eneo la Mkutano maalum wa maaskofu. Kila mmoja anafurahia utu wa kisheria, katika umma na kwa mujibu wa sheria anafananishwa na jimbo hilo. Pia inasisitizwa kwamba, muhusika anafundishwa na waamini walei, wachungaji na wajumbe wa Taasisi ya maisha ya kitawa au vyama vya kitume, asili kutoka katika Umoja wa Kianglikani; au waamini ambao wanapokea sakramenti ya ukatekemene kwa sheria hiyo ya kawaida. Hivi sasa, kuna makanisa matatu la kwanza ni  Mama Yetu wa Walsingham huko Uingereza, la pili ni Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, nchini Marekani na la tani ni Mama yetu wa Msalaba, Kusini mwa Australia.

Usasishaji wa kanuni  za ziada

Hata hivyo katika Gazeti la Osservatore Romano kuhusiana na hili, linathibitisha kwamba kanuni hizi zimepolewa vema na baadhi ya maono na maelekezo ya kitaalimungu, Kanuni ya Sheria na Uekemene ili kufanya matumizi ya kanuni zaidi kuwa sawa na roho ya Katiba ya Kitume. Sheria iliyoelekezwa na Katiba “Anglicanorum coetibus” inaongezewa na kanuni za ziada zinazotolewa na Vatican. Na  Baba Mtakatifu Francisko amekubali toleo la marekebisho ya sheria hizi.

09 April 2019, 15:35