Tafuta

Vatican News
Baba Mtakatifu akiwasalimia watu kabla ya katekesi na mvua ikiwa inanyesha mjini Roma, tarehe 10 Aprili 2019 Baba Mtakatifu akiwasalimia watu kabla ya katekesi na mvua ikiwa inanyesha mjini Roma, tarehe 10 Aprili 2019  (Vatican Media)

Katekesi ya Papa Francisko:Kama jinsi tulivyo na haja ya mkate,hata msamaha!

Kama tulivyo na haja ya mkate,ndivyo pia kuwa na haja ya msamaha na,tena msamaha wa kila siku.Ndiyomoja ya msisitizo wa tafakari ya Baba Mtakatifu katika katekesi yake kwa maamini na mahujaji waliofika mjini Vatican tarehe 10 Aprili 2019,ikiwa ni mwendelezo wa ufafanuzi wa sala ya Baba Yetu.

Baada ya kusoma neno la Mungu kutoka barua ya Mtakatifu Yohane isemayo: “Wapendwa Tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo ndani mwetu. Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote” (1Yoh 1,8-9).  Baba Mtakatifu Francisko ameanza kusema:“Wapendwa kaka na dada habari za Asubuhi”, na kuendelea na tafakari ya katekesi yake kwa waamini na wahujaji waliofika kusikikiza katekesi hiyo katika uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican  tarehe 10 Aprili 2019 hata kahali ya hewa ilikuwa ya mvua na mawingu na baridi. Baba Mtakatifu amesema: “baada ya kuomba Mungu Mkate wa kila siku, katika sala ya Baba Yetu, sasa inangia  matendo yetu, katika kambi kuhusu mahusiano na wengine. Yesu anatufundisha kumwomba Baba: “utusamehe makosa yetu kama tunavyo wasahamehe waliotukosea” (Mt 6,12). Na kwa maana hiyo kama tulivyo na haja ya mkate, ndivyo pia haja msamaha. Na huo ni wa kila siku, anathibitisha Baba Mtakatifu!

Mkristo anaye sali, anaomba Mungu kwanza amwondolee dhambi

Mkristo anaye sali anaomba hawali ya yote kwa Mungu ili amwondelee madeni, yaani dhambi zake, mambo mabaya anayotenda. Huo ndiyo ukweli wa kwanza wa kila sala, Baba Mtakatifu anasisitiza. Kutokana na kwamba sisi siyo watu wakamilifu, hata kuwa watakatifu walio angavu ambao  hawaangazii kamwe maisha ya wema, tunabaki daima kuwa watoto wa Baba na ambao kwake yeye tunategemea kila kitu. Hata hivyo Baba Mtakatifu Francisko ameuliza je ni tabia ipi iliyo ya hatari zaidi, ya kila maisha ya kikristo? “Ni kiburi.” Kiburi ni tabia ambayo mtu anajiweka mbele ya Mungu na kufikiri kuwa anahamuru daima na Mungu. Kiburi kinaamini kuwa, kila kitu kiko sawa. Ni kama yule mfarisayo aliyepiga magoti ndani ya hekalu, akafikiri anasali na kumbe alikuwa anajitukuza mbele ya Mungu maana, alisimama akasali kimoyomoyo. “Ninakushukuru Mungu kwa sababu mimi si kama watu wengine”. Baba Mtakatifu anaongeza kusema: huyo ni sawa sawa na wengine wanaohisi kuwa na  ukamilifu, watu ambao wanasengenya wengine, watu wenye kiburi. Hakuna aliye mkalifu, hakuna! Baba Mtakatifu amesisitiza!

Lakini yule mtoza ushuru alisimama mbali, nyuma ya hekalu

Akiendelea na kufafanua Baba Mtakatifu anasema aliyekuwa mdhambi na kudharauliwa na wote, hakuthubutu hata kuinua uso wake kutazama mbinguni; bali alijipiga kifuani kwa majuto na kujikabidhi katika huruma ya Mungu. Na Yesu anabainisha kwa jibu hili: “huyu mtoza ushuru alirudi nyumbani akiwa amehesabiwa haki mbele za Mungu” (Lk 18,14), kwa maana ya kusamehewa dhambi na kukombolewa: je ni kwa nini ? Ni kwa sababu mfarisayo alikuwa na shauku na utambuzi wa vizingiti vyake na dhambi zake. Hata hivyo Baba Mtakatifu Francisko amejikita kufafanua juu ya mitindoa ya dhambi kwamba: zipo dhambi zinazo onekana na zisizo onekana. Kuna dhambi kubwa zinazofanya kelelee sana, lakini pia kuna hata dhambi zilizo pembeni, ambazo zinajibanza na kuweka viota ndani ya moyo, bila hata hata mtu gundua. Na iliyo hatari zaidi Baba Mtakatifu amebainisha, kwamba ni majivuno, ambayo yanaweza hata kuambukiza hata watu ambao wanaishi kwa kina katika maisha ya dini.

Wasafi kama malaika, lakini wana majivuno kama shetani!

Ili kufafanua hili Baba Mtakatifu Francisko ametoa mfano mmoja kwamba: Kulikuwa na konventi moja ya watawa wa kike katika miaka ya 1600-1700, iliyojulikana sana na maarufu ya kipindi cha itikadi za dini fulani yenye tabia ya kifalsafa na kisiasa( mwanzilishi wake ni Giansenio (1585-1638 karne ya XVII), Konventi hiyo ilikuwa inaonekana kama ni yawakamilifu, lakini watu walikuwa wanawasema ni wasafi kama malaika,lakini wana majivuno kama shetani! Jambo hili ni baya! Baba Mtakatifu amethibitisha. Dhambi kwa kawaida inagawanya undugu, dhambi inakufanya ujione bora kuliko wengine, dhambi inatufanya tuamini kuwa tunafanana na Mungu. Kinyume chake, mbele ya Mungu sisi sote tu wadhambi na tunayo sababu ya kujipiga vifua vyetu wote! kama yule mfarisayo katika hekalu. Mtakatifu Yohane katika barua yake ya kwanza anaandika kuwa: “Tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo ndani mwetu”(Yh 1,8) Iwapo unataka kujilaghai mwenye kuwa hauna dhambi, basi unajidanganya mwenyewe, Baba Mtakatifu amesema.

Sisi tu wadhambi kwa sababu tumepokea mengi sana

Sisi tu wadeni hawali ya yote kwa sababu katika maisha tumepokea mengi kama vile uhai, baba na mama, marafiki, maajabu ya uumbaji…. Hata kama kwa wote inatokea kupitia wakati mwingie katika hali ngumu, lakini tunapaswa daima kukumbuka kuwa maisha ni neema, ni miujiza ambayo Mungu ametupatia bure.  Kadhalika sisi ni wadeni kwa sababu, hata kama tunaweza kupenda hakuna hata mmoja wetu ana uwezo wa kutenda hilo  kwa nguvu zake. Upendo wa kweli ni ule ambao tunaweza kupenda kwa neema ya Mungu. Hakuna hata mmoja anangazwa na mwanga wake binafsi!

Kuna kile ambacho wataalimungu wa kale waliikita “mysterium lunae”

Akiendelea na ufafanuzi wa mwanga, Baba Mtakatifu ansema: kuna kile ambacho wataalimungu wa kale waliikita “mysterium lunae, yaani “fumbo la mwezi”. Hii siyo tu katika utambulisho wa Kanisa, lakini pia katika historia ya kila mmoja. Je ina maana gani “mysterium lunae”? Maana yake ni kwamba mwanadamu ni  kama mwezi ambao hauna mwanga wake wenyewe. Mwezi unaangaza kutokana na jua. Hata sisi, hatuna mwanga wetu binafsi, kwa maana mwanga tulio nao ni mwanga uliotokana na neema ya Mungu, neema ya mwanga wa Mungu. Iwapo unapenda ni kwa sababu nje yako kuna mwingine, ambaye amekupa tabasamu ulipokuwa mchanga, kwa kukudunisha kujibu kwa tabasamu. Iwapo unapenda ni kwa sababu karibu nawe, kuna aliye kuamsha katika upendo na kukufanya utambue kuwa katika upendo ndimo kuna maana ya maisha. Kadhalika Baba Mtakatifu Francisko, ameomba kila mmoja ajaribu kusikiliza historia  ya mtu aliye kosea na ambaye amehukumia jela kwa sababu ya madawa ya kulevya… wanajulikana watu wengi ambao wamekosea katika maisha yao. Baada kuwajibishwa, watu wengi mara nyingine wanaulizwa je ni nani anapaswa, kuhukumia makosa.

Hiyo ndiyo fumbo la mwezi

Tunapendwa kwa sababu tulipendwa, tulisamehewa kwa sababu tulisamehe. Na iwapo hujaangazwa na mwanga wa jua unakuwa baridi sana kama ardhi ya kipindi cha baridi. Je inakuwaje nisiweze kutambua hata katika mnyororo wa upendo na kwa uwepo wa pekee wa upendo wa Mungu? Hakuna hata mmoja wetu anayependa Mungu kama alivyotupenda yeye. Kwa maana hiyo ili kuelewa zaidi juu ya upendo huo inatosha kusimama mbele ya msalaba ili uelewe upungufu huo, kwa maana Yeye alitupenda na anatupenda akiwa wa kwanza. Baba Mtakatifu Francisko akihitimisha katekesi yake amesema, tuombe Bwana ili asiche kutusamehe makosa yetu hata kama katikati yetu yupo aliye mtakatifu zaidi.

 

 

 

 

 

 

 

10 April 2019, 13:00