Papa Francisko katika picha ya pamoja na washiriki wa mafungo ya kiroho,kwa viongozi wa Umma na Kanisa wa Sudan Kusini Papa Francisko katika picha ya pamoja na washiriki wa mafungo ya kiroho,kwa viongozi wa Umma na Kanisa wa Sudan Kusini 

Ishara ya kihistoria ya Papa kubusu miguu kwa ajili ya amani Sudan Kusini

Katika nyumba ya Mtakatifu Marta mjini Vatican Baba Mtakatifu amebusu miguu ya Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir Mayardit,makamu wake,Riek Machar na Rebecca Nyandeng De Mabio.Hii ni ishara ya kuomba amani katika nchi yao.Amefanya hivyo mara baada ya kuhitimisha siku mbili za mafungo ya kiroho kwa viongozi hawa wa raia na kanisa.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Maombi ya moyo ni ishara inayovunja kila protokali zote na unafika kwa namna hii isiyotarajiwa na ambayo haipo katika maandishi yoyote, lakini ni ile ya kuhisi kwa nguvu zote kutoka ndani ya moyo kwa ajili ya kutafuta upatanisho ambao ndiyo njia mojawapo ya kufuata. Baba Mtakatifu ameinama na kupiga magoti wakati huo akiomba kwa moyo wa kina amani kwa ajili ya nchi hiyo ndogo barani Afrika. Baba Mtakatifu Francisko akiwa katika makao yake ya  nyumba  ya Mtakatifu Marta na  aliyo wakubalia wafanyie mafungo ya kiroho kwa siku mbili, hakuweza kuficha hisia zake akizungumza hivi wazi kuhusu matatizo ya wakati ujao, lakini pia hata kisisitiza kuomba. Amefanya hivyo kama kaka na kujiachia moyo wake uzungumze,amefanya hivyo akiwaomba viongozi hawa wajikite katika changamoto na waweze kuwa rahisi na kama baba wa Taifa.

Mlitia sahini ya Mkataba wa amani,bakini katika amani 

Baba Mtakatifu anasema; ninyi watatu mlitia sahini ya Mkataba wa amani, ninawaomba kama kaka yenu, kubaki katika amani .Ninawaomba kwa moyo, Twende mbele. Kutakuwapo na matatizo, lakini yasiwaogopesha nendeni mbele na kusuluhisha matatizo. Ninyi mmeanzisha mchakato, ambao unaisha vizuri .Kutawapo na mapambano kati yenu wawili; ndiyo, Hata hayo yamo ndani ya ofisi; lakini mbele ya watu, unganisheni mikono. Na hivi kwa kufafanya hivyo kwa urahisi wa wazalendo mtakakuwa Mababa wa Taifa. Niruhuui kuwaomba kwa moyo  kwa hisia zangu za kina. Ninaomba kwamba moto wa vita uzimike daima, mtazame kile kinacho unganisha na siyo kinacho tengenisha na wakati endelevu wa Sudan uweze kuwa ishara ya amani na mapatano. Baba Mtakatifu Francisko akisoma hotuba yake aliyoiandaa akiwa na  moyo wa furaha yeye anakuwa sauti ya matumaini na kuwashukuru wote walio kuwapo viongozi wa umma na Kanisa kutoka nchi za Afrika, na ambao wamesaidia kuendesha mafungo ya kiroho yaliyofanyika katika nyumba ya Mtakatifu Marta Vatican. Anasema, ni siku mbili za neema kwa ajili ya kuomba na kupokea amani. Aliye anzisha wazo hili na Askofu Mkuu wa Canterbury Justin Welby na Maratibu wa Kanisa la Presibateriani wa Scotland, Mchangaji John Chalmers.

Amani ni hali kwa mwafaka kulinganisha na heshima na haki za binadamu

Hata hivyo neno amani ndilo limesikika mara nyingi wakati wa akitoa salam za kutia moyo na kwamba, faraja ya Bwana mfufuka aliye jitokeza katika karamu Kuu. Amani ni zawadi ya kwanza Baba Mtakatifu aanathibitisha, aliyo wapatia mitume wake baada ya uchungu wa mateso na baada ya kushinda kifo. Lakini amani pia ndiyo zoezi la kwanza kwa viongozi  wa Taifa ambapo wanapaswa kuifuata, hali msingi kwa ajili ya kuheshima ya  haki za kila mtu na kwa ajili ya maendeleo fungamani ya watu wote. Baba Mtakatifu amesema:Hata mimi ninawasalimu na salam hiyo hiyo ninyi mliotoka katika mantiki kubwa ya mahangaiko kwa ajili yenu na kwa ajili ya watu, watu ambao wamejaribiwa na matokeo ya migogoro. Na maneno hayo yaweze kusikika katika karamu ya nyumba hii, kama ile ya Mwalimu na  kwa namna ya kwamba wote na kila mmoja anaweza kupata nguvu kwa ajili ya kupeleka mbele shauku za maendeleo ya taifa lenu kijana na kama moto wa Pentecoste, kwa ajili ya jumuiya kijana ya kikristo inaweza kuwa mwanga mpya wa matumaini kwa ajili ya watu wa Sudan Kusini. Na kwa maana hiyo kwa moyo wangu wote ninasema “amani kwenu”

Anayeongoza watu anawajibishwa na Mungu

Baba Mtakatifu Francisko katika hotuba yake pia anaweka bayana  mwanga wa uzoefu ambao wameufanya. Hasa  anakumbusha kuwa mafungo ya kiroho yanajikita juu ya kwenda mbali katika eneo maalum na faragha, lenye tabia ya kujiumbia ndani ya moyo kwa sala na imani, kwa kutafakari kwa kina na mkutano wa upatanisho, ili kuweza kupata matunda mema. Ni kukaa kwa pamoja mbele ya Mungu , kuwa na utambuzi wa uwajibikaji mkubwa sana kwa watu wa Sudan waliopo na watakao kuja baadaye; ni jitihada, ni ahadi na mapatano kwa ajili ya kujenga nchi yao, anasisituza Baba Mtakatifu.  Anafafanua zaidi kwamba: Hata hivyo pia ni kutambua kuwa kwa Mungu lazima kuwajibika na kwamba huduma ambayo imehitimishwa ni kusikiliza kilio cha masikini ambao wana njaa na kiu ya haki. Kaka na dada tusisahau kwamba sisi, viongozi wa kisiasa na kidini, Mungu alitukabidhi zoezi la kuwaongoza watu; alitukabidhi sana, na kwa maana hiyo atataka zaidi kutoka kwetu. Atauliza tulichotenda katika huduma yetu na katika tawala zetu na wajibu wetu kwa ajili ya amani na wema uliotimishwa kwa ajili ya watu wa jumuiya zetu kwa namna ya pekee wanaohitaji zaidi na waliowekwa pembezoni, kwa maneno mengine , atatuuliza juu ya maisha yetu, lakini pia hata kwa ajili ya maisha ya wengine.

Mtazamo wa Mungu

Baba Mtakatifu Francisko akiendelea na hotuba yake amekumbusha kuwa mafungo ya kiroho pia ni namna ya kujiweka mbele ya macho ya Yesu. Ni mtazamo ambao unabadilisha mwelekeo wa maisha kama ilivyo tokea kwa Petro, aliye itwa pamoja na kaka yake Andrea. Mtazamo wa kwanza ni ule wa uchaguzi ambao ulijitokeza shauku nyingi kwa ajili ya utume maalum. Baadaye kuna mtazamo unaogusa moyo wa Petro, aliyetubu mara baada ya kumkana  Yesu na ambaye anasababisha uongofu wake. Na mwisho kuna mtazamo baada ya Ufufuko, akiwa kando ya ziwa la Tiberia, mahali ambapo alikabidhiwa kwa mara nyingine tena utume wa kuchunga zizi lake; utume huo unahitimishwa na sadaka ya maisha. Je mtazamo wa Yesu juu yangu ni upi? Baba Mtakatifu Francisko ameuliza.

Mafungo ya kiroho kwa viongozi wa Sudan Kusini, sasa ni kuchagua

Baba Mtakatifu Francisko anasema:Tunao uhakika ndugu wapendwa kuwa wote tupo chini ya mtazamo wa Yesu. Yeye anatutazama kwa upendo na kutuomba chochote , anatusamehe, kitu na kutupatia utume. Yeye anatuonesha imani kubwa. Kuchagua daima kuwa wahudumu katika ujenzi wa dunia ya haki zaidi, Sisi tunao uhakika kwamba mtazamo wake unatufahamu kwa kina, anatupenda na kutubadili, anatupatanisha na kutuunganisha. Mtazamo wake wa wema na huruma unatutia moyo ili kukataa njia zitupelekazo katika dhambi na mauti na kutusaidia tufuate njia ya amani na wema.

Watu wanasubiri amani

Mtazamo wa Mungu ni mtazamo wa amani na unaojilezea katika shauku kubwa ya haki, ya mapatano. Baba Mtakatifu amejaribu kujiweka katika nafsi ya wale wanaoishi Sudan Kusini na kuwa na matajaio makubwa ya kuona hatima ya siku hiyo ya kihistoria ya amani. Anasema, watu wanasubiri kurudi kwenye matarajio ya kwamba kuna upatanisho   kati ya watu wote na amani mpya kwa ajili ya wote. Mawazo ya Baba Mtakatifu yamempelekea hata kutazama watu walipoteza kila kitu katika vita na katika vurugu ambazo zimepelekea vifo, njaa, uchungu na maombolezo! Ni vilio vingapi vya maskini na watu ambao wanahitaji, tumevisikia kwa nguvu zote na kupenyeza katika mbingu hadi katika moyo wa Mungu Baba ambaye anataka kuwapa haki na kuwapa wao amani.  Na roho hizi za wanaoteseka, Baba Mtakatifu anaongeza:ninawafikiria kila wakati  na kuomba ili moto wa vita uweze kuzima daima na kuwawezesha watu warudi nyumbani mwao na kuishi kwa utulivu. Ninamwomba Mungu mwenyezi ili amani iweze kufika katika nchi yenu, na ninawaombea hata  watu wenye mapenzi mema ili amani iweze kufika katika watu wenu.

Amani inawezekana

Baba MtakatifuFrancisko aidha anaonesha msimamo wake na kuwa na imani na kurudia kusema tena kwamba  amani inawezekanana kwamba ni zawadi kutoka kwa Mungu lakini pia ni jitihada  za nguvu za  watu hasa katika  kuelekea kwenye mazungumzo, mchakato na msamaha na ndiyo safari ya kuendelea kuwa mfanyakzi wa amani katika roho ya kindugu na kimshikamano. Ninawasihi zaidi kutafuta kile kinachounghanisha kunzia mahali manapoishi wenyewe  na kushinda kila aina ya kinacho watenganisha. Watu wamechoka na kukinai vita vilivyo pita; kumbukeni kuwa katika vita ni kupoteza kila kitu! Watu wenu leo hii wanatafuta wakati endelevu ulio bora , kwa njia ya mapatano na amani. Akikumbuka mkataba wa amani uliotiwa sahini mwezi Septemba mwaka jana, Baba Mtakatifu amewapongeza kwa msimamo walio uonesha, pia  utayari katika upatanisho. Anawalika wasitishe vizingiti na kuheshimu mikataba, washinde migawanyo ya kisiasa na kikabila na ili kulijenga  Taifa lao!

Shauku ya Papa

Ni matarajio ya Baba Mtakatifu kwa wakristo wa Sudan Kusini waweze kuwa wahudumu wa amani kwa sala na kwa ushuhuda  kwa mwongozo wa kiroho na kusindikizwa kibinadamu: Ninathibitisha shauku yangu na matumaini yangu ya kuweza kutembelea kwa neema ya Mungu  nchi yenu pendeka, pamoja na ndugu zangu wapendwa Askofu Mkuu wa Canterbury na ambaye alikuwa ni mratibu wa Kanisa Presibiterian.

Sala ya Papa kwa ajili ya Sudan Kusini

Katika  kuhitimisha mkutano na kabla ya kufanya ishara kubwa ambayo itabaki kuwa ya kihistoria kwa viongozi hao wa Sudan Kusini, Baba Mtakatifu amesali pamoja sala hii  kwa ajili ya upatanisho: Baba Mtakatifu mwenye ukarimu usioisha; Wewe unatuita kujipyaisha katika Roho yako na kujionesha ukuu wako hasa kwa neema ya msamaha. Tunatambua upendo wako na Ubaba wako,hasa unaposali kwa ajili ya ugumu wa moyo wa mwanadamu na katika dunia inayo chafuliwa na mapambano na kukosa mapatano wewe unawawezesha kufikia upatanisho wako. Mara nyingi watu wamevunja agano lako, lakini Wewe  hukuwaacha, uliwakumbatia kwa uhusiano mpya kwa njia ya Yesu, Mwanao na mkombozi wetu; ni muungano thabiti ambao hakuna awezaye  kuuvunja. Tunakuomba utende kwa nguvu za Roho, katika ndani ya mioyo ili maadui wapate kufungua katika mazungumzo, wapinzani washikane mikono kwa nguvu na watu wakutane katika upatanisho. Kwa njia ya zawadi yako ee Baba, utafutaji wa amani ya kweli, utofautishwe na ule wa majivuno, upendo ushinde chuki na visasi vizibitiwe kwa njia ya msamaha, kwa sababu katika  kuamini wewe peke  yako na katika huruma yako, tunapata njia ya kurudi kwako, na kwa kujifungulia matendo ya Roho Mtakatifu na tunaishi maisha mapya katika Kristo, tukisifu daima jina lako na katika huduma kwa ndugu. Amina.

12 April 2019, 09:17