Tafuta

Baba Mtakatifu Francisko wakati wa Sala ya Malkia wa Mbingu, amewakumbuka na kuwaombea waathrika wa majanga asilia Afrika ya Kusini na wakimbizi nchini Libya. Baba Mtakatifu Francisko wakati wa Sala ya Malkia wa Mbingu, amewakumbuka na kuwaombea waathrika wa majanga asilia Afrika ya Kusini na wakimbizi nchini Libya. 

Papa Francisko: Wakimbizi nchini Libya & Maafa Afrika ya Kusini

Baba Mtakatifu Francisko anasema, hali ya wakimbizi nchini Libya ni mbaya sana kutokana na vita ya wenyewe kwa wenyewe inayoendelea nchini humo. Baba Mtakatifu ametoa wito, kwa Jumuiya ya Kimataifa kuharakisha mchakato wa kuwaokoa wanawake, watoto pamoja na wagonjwa wanaohitaji msaada wa dharura, jambo linalowezekana kwa njia ya mshikamano wa kimataifa.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya Sala ya Malkia wa Mbingu, Jumapili tarehe 28 Aprili 2019 kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican, amewaalika waamini pamoja na watu wote wenye mapenzi mema kuungana naye, kwa ajili ya kuwaombea wakimbizi na wahamiaji walioko vizuizini nchini Libya. Hali yao kwa sasa ni mbaya sana kutokana na vita ya wenyewe kwa wenyewe inayoendelea nchini humo. Baba Mtakatifu ametoa wito, kwa Jumuiya ya Kimataifa kuharakisha mchakato wa kuwaokoa wanawake, watoto pamoja na wagonjwa wanaohitaji msaada wa dharura, jambo linalowezekana kwa njia ya mshikamano wa kimataifa.

Baba Mtakatifu katika Sala ya Malkia wa mbingu, amewakumbuka na kuwaombea pia wananchi wa Afrika ya Kusini walioathirika kwa mafuriko pamoja na maporomoko ya ardhi huko KwaZulu-Natal pamoja na viunga vya mji wa Durban. Takwimu za hivi karibuni zinazonesha kwamba, watu 70 walipoteza maisha na kwamba, zaidi ya watu 1, 000 hawana makazi maalum baada ya nyumba zao kubomolewa kwa mafuriko pamoja na miundo mbinu kuharibiwa vibaya!

Papa: Libya, Afrika ya Kusini
29 April 2019, 10:45