Tafuta

Papa Francisko Salam za Pasaka: Urbi et Orbi: 2019: Umuhimu wa Wakristo kutumia vyombo vya mawasiliano ya jamii kutangaza na kushuhudia Fumbo la Pasaka. Papa Francisko Salam za Pasaka: Urbi et Orbi: 2019: Umuhimu wa Wakristo kutumia vyombo vya mawasiliano ya jamii kutangaza na kushuhudia Fumbo la Pasaka. 

PASAKA YA BWANA 2019: Salam na Matashi mema ya Pasaka!

Ilikuwa ni tarehe 17 Aprili 1949, Papa Pio XII, kwa mara ya kwanza katika historia, alipotuma ujumbe wa Pasaka “Urbi et Orbi” kwa njia ya Televisheni ya Ufaransa akiwatakia waamini heri na baraka za Sherehe ya Pasaka. Katika ujumbe huo, alikazia umuhimu wa Khalifa wa Mtakatifu Petro na waamini katika ujumla wao kukutana katika uwanja wa mawasiliano na kwa wakati huo, Televisheni.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya ujumbe wake wa PasakaUrbi et Orbi”, Jumapili tarehe 21 Aprili 2019, ametumia nafasi hii pia kutoa salam na matashi mema ya Sherehe Njema ya Pasaka kwa waamini na mahujaji kutoka ndani na nje ya Italia, waliohudhuria kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican. Baba Mtakatifu ametumia fursa hii, kuwakumbuka pia waamini na watu wote wenye mapenzi mema waliofuatilia tukio hili kwa njia ya televisheni, radio na mitandao ya kijamii, utajiri mkubwa na maendeleo katika tasnia ya mawasiliano duniani!

Ilikuwa ni tarehe 17 Aprili 1949, Mtumishi wa Mungu Papa Pio XII, kwa mara ya kwanza katika historia, alipotuma ujumbe wa Pasaka “Urbi et Orbi” kwa njia ya Televisheni ya Ufaransa, akiwatakia waamini pamoja na watu wenye mapenzi mema heri na baraka za Sherehe ya Pasaka. Katika ujumbe huo, alikazia umuhimu wa Khalifa wa Mtakatifu Petro na waamini katika ujumla wao kukutana katika uwanja wa mawasiliano na kwa wakati huo, Televisheni. Baba Mtakatifu Francisko anasema, kwake hii ni fursa makini ambayo anapenda kuitumia ili kuzihamasisha Jumuiya za Kikristo kuhakikisha kwamba, zinatumia kikamilifu njia mbali mbali za mawasiliano ya jamii zinazotolewa katika ulimwengu mamboleo kutokana ana maendeleo makubwa ya sayansi na teknolojia ya mawasiliano. Njia hizi ziwasaidie kutangaza Habari Njema ya Wokovu kwamba, Kristo Yesu aliteswa, akafa na kufufuka kwa wafu!

Baba Mtakatifu anakaza kusema, kwa njia ya Mwanga wa Pasaka, waamini wajitahidi kuwapelekea jirani zao harufu nzuri ya Kristo Mfufuka hasa kwa wale wanaoishi katika upweke, umaskini wa hali na kipato; pamoja na majanga mbali mbali ya maisha. Waamini wajitahidi kuondoa jiwe la kutojali wala kuguswa na mahangaiko ya wengine. Furaha ya Pasaka kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro amesema Baba Mtakatifu, imefumbatwa kwa uwepo wa umati mkubwa wa watu na maua yaliyotolewa na familia ya Mungu kutoka Uholanzi. Maua yaliyopamba Altare ya Kanisa kuu la Mtakatifu Petro ni zawadi kutoka Slovenia, matendo makuu ya Mungu. Baba Mtakatifu amewashukuru na kuwapongeza wale wote waliojisadaka kutoa na kupamba maua haya, kiasi cha kuleta mvuto na mguso kwa mamilioni ya watu!

Papa: Pio XII
21 April 2019, 14:01