Tafuta

Papa Francisko amesitikitishwa sana na mambulizi ya kigaidi yaliyofanywa dhidi ya Makanisa na kwenye hoteli kadhaa na kusababisha vifo vya watu na mali zao Sri Lanka. Papa Francisko amesitikitishwa sana na mambulizi ya kigaidi yaliyofanywa dhidi ya Makanisa na kwenye hoteli kadhaa na kusababisha vifo vya watu na mali zao Sri Lanka. 

PASAKA YA BWANA 2019: Papa: Mashambulizi ya Makanisa Sri Lanka

watu 101 wamefariki dunia na wengine 450 kujeruhiwa vibaya kutokana na mashambulizi matatu ya mabomu ya kujitoa mhanga huko nchini Sri Lanka, mahali ambako Wakristo walikuwa wamekusanyika kwa ajili ya maadhimisho ya Sherehe ya Pasaka, Jumapili, tarehe 21 Aprili 2019. Baba Mtakatifu Francisko amesikitishwa sana na vitendo hivi vya kikatali dhidi ya watu wasio na hatia.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Zaidi ya watu 101 wamefariki dunia na wengine 450 kujeruhiwa vibaya kutokana na mashambulizi matatu ya mabomu ya kujitoa mhanga huko nchini Sri Lanka, mahali ambako Wakristo walikuwa wamekusanyika kwa ajili ya maadhimisho ya Sherehe ya Pasaka, Jumapili, tarehe 21 Aprili 2019. Bomu la kwanza limelipuliwa kwenye Kanisa la Mtakatifu Anthony huko Kochchikade, bomu la pili limelipuliwa kwenye Kanisa la Mtakatifu Sebastian huko Negombo na bomu la tatu limelipuliwa kwenye Kanisa Batticaloa. Mabomu mengine yamelipuliwa kwenye hoteli nne tofauti huko Colombo. Hoteli hizi ni Shngri, La Kingsbury pamoja na Cinnamon Grand.

Baba Mtakatifu Francisko wakati wa ujumbe wake wa Pasaka “Urbi et Orbi”, Jumapili tarehe 21 Aprili 2019, amewakumbuka na kuwaombea wale wote waliopatwa maafa pamoja na kuguswa na msiba huu mzito huko nchini Sri Lanka. Baba Mtakatifu amechukua fursa hii kuonesha uwepo wake wa karibu kwa Jumuiya za Kikristo nchini Sri Lanka, zilizoshambuliwa wakati waamini wakiwa katika sala. Baba Mtakatifu amewakumbuka na kuwaombea waathirika wote wa vitendo vya kikatili kama hivi. Baba Mtakatifu amewaweka wote waliofariki dunia na wale walioguswa na kutikiswa na mashambulizi haya mikononi mwa Mwenyezi Mungu, mwingi wa huruma na mapendo, aweze kuwafariji walioondokewa na ndugu zao!

Kwa upande wake, Kardinali Malcolm Ranjith, Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Colombo, amesikitishwa sana na mashambulizi haya ya kigaidi ambayo yamesababisha maafa kwa watu wasiokuwa na hatia pamoja na uharibifu wa nyumba za ibada na makazi ya watu. Kardinali Ranjith ameitaka Serikali nchini Sri Lanka kufanya uchunguzi wa kina na kuhakikisha kwamba, wahusika wanafikishwa mbele ya sheria ili kujibu tuhuma zinazowakabili.

Papa: Sri Lanka
21 April 2019, 14:20