Cerca

Vatican News
Papa Francisko amewaandikia wananchi wa Aquila ujumbe wa imani, matumaini na mshikamano kama kumbu kumbu ya miaka 10 tangu tetemeko la ardhi lilipotokea! Papa Francisko amewaandikia wananchi wa Aquila ujumbe wa imani, matumaini na mshikamano kama kumbu kumbu ya miaka 10 tangu tetemeko la ardhi lilipotokea! 

Papa Francisko: Dumisheni: Umoja, ubunifu, sheria & udugu

Baba Mtakatifu Francisko anaiombea familia ya Mungu Jimbo kuu la Aquila, ili mwanga wa Kristo Mfufuka uwaangazie wote na kuwapatia nguvu ya kushikamana kwa kujikita katika kipaji cha ubunifu, ili Jumuiya ya waamini na jamii katika ujumla wake, ili kuwa ni mashuhuda wa ujasiri, utawala sheria na ujenzi wa mshikamano na udugu wa kibinadamu!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko katika kumbu kumbu ya maadhimisho ya Miaka 10 tangu tetemeko la ardhi lilipotokea mjini Aquila na kusababisha maafa makubwa kwa watu na mali zao, amemwandikia ujumbe Kardinali Giuseppe Petrocchi wa Jimbo kuu la Aquila, Italia, kuwatia shime kusonga mbele kwa imani na matumaini. Anasema, bado anaendelea kuwakumbuka na kuwaombea wale wote waliopoteza maisha na mali zao katika tetemeko hili bila kuzisahau familia zao!

Baba Mtakatifu anawataka kusonga mbele kwa ari na moyo mkuu, huku akiwasindikiza katika ujenzi na ukarabati wa mji wao, wakiwa wameshikamana, ili kazi hii iweze kufanyika kwa haraka zaidi. Ujenzi wa miundo mbinu ya huduma kwa jamii, makazi ya watu binafsi na Makanisa yaliyobolewa, yajengwe kwa haraka, ili watu waanze kupata huduma! Mwishoni, Baba Mtakatifu anaiombea familia ya Mungu Jimbo kuu la Aquila, ili mwanga wa Kristo Mfufuka uwaangazie wote na kuwapatia nguvu ya kushikamana kwa kujikita katika kipaji cha ubunifu, ili Jumuiya ya waamini na jamii katika ujumla wake, ili kuwa ni mashuhuda wa ujasiri, utawala sheria na ujenzi wa mshikamano na udugu wa kibinadamu!

Papa: Aquila
06 April 2019, 15:22