Tafuta

Papa Francisko amemtumia salam na matashi mema Rabbi mkuu wa Roma Riccardo Shemuel Di Segni kwa maadhimisho ya Sherehe ya "Passover", "Pesach" Papa Francisko amemtumia salam na matashi mema Rabbi mkuu wa Roma Riccardo Shemuel Di Segni kwa maadhimisho ya Sherehe ya "Passover", "Pesach" 

Pasaka ya Bwana 2019: Salam na matashi mema kwa Rabbi Di Segni

Katika Kipindi hiki cha Pasaka, Baba Mtakatifu anapenda kuimarisha urafiki na majadiliano ya kidini yanayofumbatwa katika huduma kwa maskini na wale wote wanaosukumizwa pembezoni mwa jamii. Amechukua fursa hii, kumhakikishia uwepo wake kwa njia ya sala na kumwomba hata yeye amkumbuke katika sala zake! “Chag Sameach”.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko pamoja na Rabbi mkuu wa Roma Riccardo Shemuel Di Segni, wametumiana salam na matashi mema katika maadhimisho ya Siku kuu ya Pasaka, kwa Wakristo na “Passover, Pesach, kwa Wayahudi inayo sherehekewa mwaka huu kuanzia tarehe 19 Aprili – tarehe 27 Aprili 2019. Katika salam zake, Baba Mtakatifu anamwombea ili Mwenyezi Mungu mwingi wa huruma aweze kumsindikiza na kumkirimia baraka, amani na utulivu.

Katika ujumbe huu wa matashi mema katika Kipindi hiki cha Pasaka, Baba Mtakatifu anapenda kuimarisha urafiki na majadiliano ya kidini yanayofumbatwa katika huduma kwa maskini na wale wote wanaosukumizwa pembezoni mwa jamii. Amechukua fursa hii, kumhakikishia uwepo wake kwa njia ya sala na kumwomba hata yeye amkumbuke katika sala zake! “Chag Sameach”.

Kwa upande wake, Rabbi Riccardo Shemuel Di Segni, ametumia fursa hii ya Maadhimisho ya Sherehe ya Pasaka, kumshukuru Baba Mtakatifu na kumtakia matashi mema, furaha, utulivu na afya njema! Mwenyezi Mungu aendelee kumlinda pamoja na kuimarisha urafiki na ushirikiano na kwamba, sala na maombi anayomtolea Mwenyezi Mungu yaweze kupokelewa!

Papa: Passover
19 April 2019, 14:36