Tafuta

Alhamisi Kuu: Ekaristi Takatifu, Daraja takatifu & Amri ya Upendo: Mapadre 2, 000 wameshiriki Misa ya Kubariki Mafuta Matakatifu; 10 wamepata chakula cha mchana na Papa Francisko. Alhamisi Kuu: Ekaristi Takatifu, Daraja takatifu & Amri ya Upendo: Mapadre 2, 000 wameshiriki Misa ya Kubariki Mafuta Matakatifu; 10 wamepata chakula cha mchana na Papa Francisko. 

Alhamisi kuu: Mapadre wapata chakula na Baba Mtakatifu Francisko

Mapadre watambue kwamba, wamepakwa mafuta ili kubariki na kuwatakatifuza watu wa Mungu! Mara baada ya Misa Takatifu, wakati wa mchana, Baba Mtakatifu Francisko, amepata chakula cha mchana na Mapadre kumi wanaotekeleza utume wao Jimbo kuu la Roma. Imekuwa ni nafasi yakubadilishana, uzoefu, mang’amuzi na changamoto za maisha na utume wao wa Kipadre!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Alhamisi Kuu, Mama Kanisa anakumbuka Siku ile Yesu alipoweka Sakramenti ya Ekaristi Takatifu, yaani Mwili na Damu yake Azizi, chanzo na kilele cha maisha na utume wa Kanisa. Hii ni Sakramenti ya Sadaka: Shukrani, Sifa na Utukufu kwa Baba wa milele; Ni Kumbukumbu ya mateso yaletayo wokovu na kwamba, hii ni sadaka ya uwepo wa Kristo kwa Neno na Roho wake Mtakatifu. Mama Kanisa anakumbuka pia Siku Yesu alipoweka Sakramenti ya Daraja Takatifu.

Hawa ni Makuhani waoliopewa dhamana ya kufundisha, kuongoza na kuwatakatifuza watu wa Mungu, katika Nafsi ya Kristo ambaye ni kichwa cha Kanisa lake! Hii ni Siku ambayo Kristo alikazia huduma ya upendo kwa kuwaosha mitume wake miguu, kielelezo cha upendo unaomwilishwa katika huduma kwa watu wa Mungu! Baba Mtakatifu Francisko, Alhamisi kuu, tarehe 18 Aprili 2019, ameadhimisha Ibada ya Misa Takatifu na kubariki Mafuta Matakatifu, kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican. Katika mahubiri yake, amekazia neema ambazo waamini wanapata kwa kujenga na kudumisha mahusiano na mafungamano yao na Kristo Yesu katika maisha.  

Hii ni neema ya kumfuasa Kristo, kushangaa na kujazwa furaha kwa kukutana naye katika maisha, ili kuweza kufanya mang’amuzi yanayobubujika kutoka katika sakafu ya moyo wa Neno wa Mungu aliyefanyika mwili. Maskini na wale wote walioelemewa na mifumo ya umaskini, walitangaziwa Habari Njema ya Wokovu; mwaliko kwa waamini kuwa kweli ni Wasamaria wema, ili kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao! Taarifa zinaonesha kwamba, Mapadre elfu mbili wameshiriki katika Ibada ya Kubariki Mafuta Matakatifu pamoja na kurudia tena ahadi zao za utii kwa Baba Mtakatifu.

Baba Mtakatifu amewataka wakleri kupenda kuwa kati ya watu na kuwahudumia kwa unyenyekevu na upendo mkuu; watambue kwamba, wamepakwa mafuta ili kubariki na kuwatakatifuza watu wa Mungu! Mara baada ya Misa Takatifu, wakati wa mchana, Baba Mtakatifu Francisko, amepata chakula cha mchana na Mapadre kumi wanaotekeleza dhamana na utume wao Jimbo kuu la Roma. Imekuwa ni nafasi ya kuweza kubadilishana, uzoefu, mang’amuzi na changamoto za maisha na utume wa Kipadre Jimbo kuu la Roma!

Papa: Wakleri wa Roma
19 April 2019, 12:25