Cerca

Vatican News
Askofu Mkuu Ignatius Ayau Kaigama ameteuliwa kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Abija nchini Nigeria Askofu Mkuu Ignatius Ayau Kaigama ameteuliwa kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Abija nchini Nigeria 

Uteuzi wa Askofu Mkuu mwandamizi wa Jimbo Kuu Abuja Nigeria

Baba Mtakatifu amemteua Askofu Mkuu Ignatius Ayau Kaigama kuwa mwandamizi wa Jimbo Kuu Abuja, hadi sasa alikuwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Jos nchini Nigeria

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu Mkuu Ignatius Ayau Kaigama aliyekuwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Jos kuwa Mwandamizi wa Jimbo Kuu la Abuja nchini Nigeria. Askofu Mkuu Ignatius Ayau Kaigama alizaliwa tarehe 31 Julai 1958 huko Kona, Jimbo katoliki la Jalingo nchini Nigeria.Mafunzo yake ya Taalimungu katika Seminari Kuu ya Mtakatifu Augustine huko Jos.  Alipata daraja la upadre tarehe 6 Juni 1981 kuhudumia  jimbo katoliki la Yola.

Kunako mwaka 1991 aliendelea na Mafunzo ya Shahada ya Kitsaufi katika Chuo Kikuu cha Kipapa Gregoariana Roma. Alichaguliwa kuwa Askofu wa Kwanza wa Jimbo la Jalingo tarehe 3 Februari 1995, na kuwekwa wakfu tarehe 23 Aprili  1995. Alihamisha katika Jimbo Kuu la Jos 14 Aprili 2000. Tangu mwaka 2015 ni Rais wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Magharibi (RECOWA-CERAO), na mjumbe wa Baraza la Kipapa la kuhamasiaha Unjilishaji mpya tangu tarehe 25 Julai 2012. Aliwahi kushika nafasi ya urais wa Baraza la Maaskofu wa Nigeria kuanzia mwaka (2012-2018).

Hadi sasa Jimbo Kuu la Abuja linaongozwa na Kardinali John Olorunfemi Onaiyekan. Huyo alizaliwa huko Kabba, tarehe 29 Januari 1944. Tarehe 3 Agosti 1969 alipewa daraja la upadre, Na tarehe 10 Septemba 1982 kutumika kanisa la Tunusuda na Askofu msaidizi wa Ilorin. Aliwekwa wakfu wa uas kofu tarehe 6 Januari 1983. Na Mtakatifu Paulo II. Tarehe 20 akatangazwa kuwa askofu wa 1984 Ilorin. Tarehe 7 Julai 1990 litangazwa kuwa Askofu Mwandamizi wa Abuja na baadaye akapewa makao makuu  hayo tarehe 28 Septemba 1992. Tarehe 26 Machi 1994. Jimbo la Abuja likapewa heshima ya kuwa jimbo Kuu na yeye akawa Askofu Mkuu wa kwanza wa jimbo Kuu la Abuja Nigeria.

Tangu mwaka 2000 hadi 2006 alikuwa Rais wa Baraza la Maaskofu Nigeria, na wakati huo tangu 2003 2009, aliongoza Mabaraza ya Maaskofu wa Afrika Magharibi wa lugha ya kingereza na kuanzia 2003-2007 alishika nafasi ya rais wa shirikisho la maaskofu wa Afrika ya Mashariki na Madagasar. Mei 2007 alishiriki Mkutano wa Amerika ya kusini huko Aparecida. Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI akamteua kuwa Kardinali wa Kanisa la Mtakatifu Saturnino na kuwekwa wakfu tarehe 24 Novemba 2012.  Ameshiriki uchaguzi wa Baba Mtakatifu Francisko mwaka 2013. Tangu tarehe 3 Julai 2013 hadi tarehe  19 Februari 2019 anashika wadhifa wa utawala za kutume katika Jimbo la Ahiara. Tarehe 28 Oktoba  2016 Baba Mtakatifu alimteua kuwa mjumbe wa Baraza la Kipapa la Ibada na Nidhamu ya Sakramenti.

11 March 2019, 16:18