Tafuta

Ulinzi wa watoto,Motu Proprio ya Papa Francisko na sheria mpya za serikali ya Vatican ndiyo maana ya misingi mipya iliyopo katika hati hizo tatu  zilizotolea tarehe 29 Machi 2019 Ulinzi wa watoto,Motu Proprio ya Papa Francisko na sheria mpya za serikali ya Vatican ndiyo maana ya misingi mipya iliyopo katika hati hizo tatu zilizotolea tarehe 29 Machi 2019 

Ulinzi wa watoto,Motu Proprio ya Papa Francisko na sheria mpya ya Vatican!

Mfumo mpya wa kisheria katika Mji wa Vatican umewekwa ili kuzuia na kupambana na unyanyasaji dhidi ya watoto na watu katika mazingira magumu.Papa anasema Kristo mwenyewe,amekabidhi utunzaji na ulinzi wa wadogo na wasio jitetea.Anayempokea mmoja kati ya hawa walio wadogo kwa jina langu,ananipokea mimi

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Ulinzi wa watoto, Motu Proprio ya Papa Francisko na sheria mpya za serikali ya Vatican ndiyo maana ya misingi mipya iliyopo katika hati tatu zilizotangazwa na Baba Mtakatifu Francisko kwa ajili ya Vatican na Kanisa la Roma tarehe 29 Machi 2019 . Katika Motu proprio juu ya ulinzi wa watoto na watu waathirika, kanuni mpya iliyotolewa kwa ajili ya mji wa Vatican na kupanulia kwa Kanisa la Roma, na miongozo ya kichungaji, ambayo ipo katika hati hizo tatu zilizotiwa sahini na Baba Mtakatifu Francisko,ambazo zinafuatia mara baada ya mkusanyiko wa Marais wa Mabaraza ya Maaskofu duniani uliofanyika mwezi Februari mjini Vatican. Kwa maana nyingine ni kusema kuwa hati hizi zinakilisha tunda kwanza la mkutano huo.

Hati hizi ya   Ulinzi wa watoto, Motu Proprio ya Papa Francisko na sheria mpya za Vatican na Kanisa la Roma

Hizi ni sheria, kanuni na maelekezo muhimu hasa zaidi, yanatazama  hawali ya yote mji wa Vatican tu, mahali ambapo idadi kubwa ya mapadre na watawa wanahuduma lakini pia kuna watoto wachache. Licha ya kufikiriwa  na kuandikwa kwa ajili ya hali halisi moja ya dunia, mahali ambapo sehemu kubwa la viongozi wakuu wa dini  pia  watawala na wanasheria, hati hizi tatu zina maelekezo yanayo fanana na ambayo yanazingatia vigezo zadi  vya hali ya  juu vya  kimataifa. Katika motu proprio moja ya hati ambayo ni muhimu yenye sahini ya Papa; Baba Mtakatifu Francisko anaelelezea shauku zake  na kati ya hizo  anathibitisha   kwamba kuwe na ukomavu wa kutambuzi wa kutoa taarifa juu ya manyanyaso kwa Vongozi wakuu husika na kushirikiana nao katika shughuli za kuzuia na kuthibiti. Hata hivyo Sababu iliyo mfanya awe na uamuzi wa kutia sahini yeye binafsi hata katika Sheria ya CCXCVII na miongozo na mbayo kwa mtazamo rahisi ingeweza hata kutangazwa moja kwa moja tu na Tume ya Serikali ya Vatican na Makamu wa Mji wa Vatican, ni kutaka kuonesha thamani  yake kuu ambayo inatakiwa katika kanuni hizo. Hati ya kwanza kati ya tatu ni sheria mpya mahali ambao unafafanuliwa kwenye hatua ya kwanza na iliyo wazi ambayo ni kubwa kwa ajili ya aina ya watu waathirika kulinganisha na wadogo.

Mambo mengi mapya katika hati hizi ni mengi, kwa mfano

Inasema “ni mwathirika kila mtu ambaye yupo katika hali ya ugonjwa, kutojiweza kimwili au kiakili au kokosa uhuru binafsi, hata wakati mwingine kuwa na vizingiti vya uwezo wa kutambuliwa au thamani na kwa maana nyingine kukosa ulinzi”. Mambo mengi mapya katika hati hizi ni mengi, kwa mfano kuna kipengele kipya kwamba tangu sasa na kuendelea hualifu wote wote unaojihusisha na manyanyaso ya wadogo na si tu yale na siyo tu kuhusu ngono lakini pua mifano ya mateso, lazima ifuatiwe katika ofisi hata ile ya kukosa kutoa taarifa kwa upande huo inakuwa kosa. Jambo jipya la pili lipo katika utangulizi unaojifafanua kuelezea kuhusu miaka. Hata hivyo inabiki kukumbusha kuwa hawazungumzii juu ya Kanuni za sheria , bali sheria ya hukumu ya mji wa Vatican mahali ambapo hapajawahi kuanzishwa kwa Gombo la Rocco iliyotangazwa nchini Italia katika kipindi cha kifashisti na ambalo ni Gombo la Hukumu ya Zanardelli ambayo uhalifu huu  ulikuwa unaelezea juua ya miaka minne ya uahalifu.

Habari nyingine mpya  muhimu inahusu wajibu wa kutoa ripoti na maagizo kwa afisa wa umma ambaye anaweza kutoa ripoti ya ukiukwaji wa mamlaka ya mahakama ya Vatican mahali ambapo inaweza ikawa imepata habari na ufahamu, bila kuathiri muhuri wa sakramenti, yaani siri ya kukiri. Hii ina maana kwamba wote ambao, wapo katika Serikali kuu ya vatican, na kuendelea hata  kati ya wafanyakazi wa kidiplomasia katika huduma ya ubalozi wanajukumu la la shughuli ya umma (zaidi ya asilimia 90 ya watu wanaofanya kazi katika Vatican au kwa Baba Mtakatifu) wataadhibiwa wakati wa kushindwa kuripoti. Mabadiliko makubwa zaidi na muhimu ni uanzishwaji na taasisi katika mji wa  Vatican katika kitengo cha  Idara ya Afya na Usafi wa Vatican, ya huduma ya kusindikiza waathirika wa manyanyaso ambayo itaendeshwa na mtaalam.

Waathirika watakuwa na mtu na mahali pa kwenda kutafuta msaada wa matibabu na kisaikolojia kwa mwenye sifa inayo faa

Kwa njia hiyo waathirika watakuwa na mtu mahali pa kwenda kutafuta msaada wa matibabu na kisaikolojia, kuwafahamu haki zao na jinsi ya kufanya zipatikane. Habari pia nyingine ni kuhusu uteuzi na kuajiriwa kwa wafanyakazi wa Nyuma kuu a ya Roma. Nawanawa wachaguliwa kulingana na uwezo wa kuhakikisha ulinzi wa watoto. Na hatimaye, Mwongozo wa Kichungaji wa mji  wa Vatican. Inaweza kuonekana kama hati fupi ikilinganishwa na maandishi ya baadhi ya Mabaraza ya Maaskofu, lakini ni lazima ikumbukwe kwamba kuna parokia mbili tu mjini Vatican na watoto wanaoishi ndani ni wachache tu.

Mwongozo huo unaoelekezwa kwa mapadre, mashemasi na  waalimu wa Seminari ndogo ya  Pio X,  makuhani wa parokia na wachungaji wa parokia mbili, kwa watawa wa kike na kiume ambao wanaishi ndani ya Vatican pia, na wote wanaofanya kazi yoyote ile na ya kiwango,mtu binafsi au chama, ndani ya jumuiya ya kanisa la mji wa Vatican. Hata hivyo umefafanua, kwa mfano, kwamba watu hawa lazima  waonekane daima wazi kwa wengine mbele ya watoto, na kwamba imekatzwa kisheria kuanzisha uhusiano wowote wa upendeleo na mtu mdogo, kumgeukia mdogo kwa namna ya kutisha au kushiriki katika tabia isiyofaa kama vile kushauriana kimapenzi, kumwomba mtoto kuweka siri, kumpiga picha au kutengeneza filamu bila idhini ya maandishi ya wazazi wake. Na mengine zaidi.

Makamu wa Vatican kuanzia sasa na kuendelea analazimika kutoa taarifa

Makamu wa Vatican kuanzia sasa na kuendelea analazimika kutoa taarifa kwa wahamasishaji wa haki kwa kila habari kuhusu unyanyaswaji, lakini siyo uzushi, kama tahadhari, kuondoa mhalifu wa madai ya unyanyasaji kutoka katika shughuli za kichungaji. Na yeyote atakaye bainika na makosa ya manyanyaso ataondolewa majukumu yake mjini Vatican. Kama ni padre atawekwa katika michakato yote ya kisheria mabyo tayari ipo. Hati zilizotolewa sasa na kutangazwa mwishoni mwa mkutano  wa Maaskofu mwezi   Februari zitafuatiwa na kuchapishwa kwa upande wa Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa mhutasari wa kitabi dhidi ya kupambana na unyanyasaji kwa ajili ya Kanisa zima duniani na kuundwa kwa mifumo ya njia za kusaidia majimbo yenye kuwa na upungufu wa watu walio na taaluma ya kushughulikia kesi hizi. Hatua ya Baba Mtakatifu Francisko kwa maana hiyo ni wazi na ya usahihi kwamba  Ulinzi wa watoto na watu walio katika mazingira magumu ni sehemu muhimu ya ujumbe wa kiinjili ambapo Mama Kanisa na waamini wake wote wanaitwa kueneza ulimwenguni kote.

29 March 2019, 13:56