Cerca

Vatican News
Baba Mtakatifu amekutana mjini Vatican na chama cha kupambana na Saratani ya damu Baba Mtakatifu amekutana mjini Vatican na chama cha kupambana na Saratani ya damu   (Vatican Media)

Kuwa na ujasiri wa kusimama na mateso kama Mama Maria!

Baba Mtakatifu amekutana na wanachama cha kupambana na Saratani ya damu, nchini Italia na mawazo yake yamewaendea kwa namna ya pekee wagonjwa wote wa saratani ili wasihisi upweke

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Tarehe 2 Machi 2019 Baba Mtakatifu Francisiko amekutana mjini Vatican  na wajumbe wa  Chama cha Kupambana na Saratani ya damu nchini Italia, wakiwa wanaadhimisha miaka 50 tangu kuanzishwa  kwa chama hicho. Anawakaribisha moyo  wote, kwa namna ya pekee anawasalimia wagonjwa waliombatana nao, hata wale ambao hawakuweza kufika. Anamshukuru Rais wa Chama hicho Profesa Sergio Amadori, kwa maneno yake, kama ilivyo hata madaktari na wahudumu wa afya, kwa wote wanaojikita katika utafiti, watu wa kujitolea na wanaoshiriki kwa uhai wote kwa ajili ya wema wa chama chao.

Katika liturujia ya siku, Baba Mtakatifu anaeleza kuwa, Kanisa linawaalika kutafakari somo la Yoshua Bin Sira (Ybs 17,1-13 ) kwa zawadi kubwa ambazo Bwana amewatendea watu wake. Baada ya kuwaumba, akawajaza maarifa ya sayansi ya hekima na kuwawezesha kupambanua wema na uovu, aliyaweka mbele yao maarifa ya sayansi, akawapa sheria ya uzima kuwa urithi. Baba Mtakatifu anaongeza kusemakama ambavyo tayari amekumbusha mara nyingi kwamba sayansi ni chombo chenye nguvu ya kutambua vema, iwe asili ambayo ituzunguka na hata iwe afya ya binadamu. Dhamiri yetu inaendelea na kwayo inaongezeka kwa njia ya vyombo na teknolojia ambavyo ni muhimu kuwezesha si kutazama muundo wa kina zaidi cha viungo hai na mtu kamili, lakini pia hadi kufikia kuingilia kati kwa namna ya kina na ustadi wa hadi kuwezesha kubadili vinasaba (DNA). (Hotuba ya Mkutano wa IV wa Kimataifa ulioandaliwa na Baraza la Kipapa la Utamaduni, juu ya madawa mbadala, 28 Aprili 2018).

Kanisa linatoa pongezi na kutia moyo kila jitihada za tafiti na kuweka matendo katika sura ya tiba ya mtu anayeteseka. Na kwa maana hiyo Baba Mtakatifu katika fursa ho baba Mtakatifu anatoa pongezi kwa Chama kwa kile ambacho wawezesha kufikia kwa miaka hii. Katika shughuli yake ya thamani ya chama hiki uwepo  wake umegeuka kuwa muhimu sana katika maeneo ya kitaifa kwa kujikita juu ya huduma kwa wagonjwa na kushirikiana na Vituo mbalimbali maalum. Matendo yao msingi na yanayowaongoza yanaonesha matokeo ya dhati kwa utafiti wa kisayansi, huduma ya afya na mafunzo kwa wahadumu. Kwa namna ya pekee katka mantiki hizi tatu wanajikita ndani ya nafasi ambayo inaitwa mtu mwenyewe.

Katika utafiti wa kisayansi wanaofanya uchunguzi  wa ukuu wa baiyolojia ya binadamu, ili kuweza kutoa faraja ya ugonjwa, kwa matendo ambayo wakati mwingine ni katika kuzuia ,na tiba ambayo ni ya dhati. Katika huduma yao ya kusaidia jirani anayeteseka, kwa kumsindikiza, katika kipindi cha mateso yake, ili hasiwepo mtu ambaye aweze kuhisi upweke au hisia za kuachwa pembenikwa heshima katika mantiki ya kijamii. Hatimaye kwa tiba na mafunzo kwa wahudumu ili kuendelea matendo yao kwa ajili ya kufanya kazi kwa ujumla na mtu mgonjwa ili kufikia mapatano ya tiba msingi kwa wagonjwa na wahudumu wa afya mabao wanakabiliana na uzoefu huo kila siku.

Baba Mtakatifu amependa kuwambia jambo moja ambalo limemgusa moyo miaka sita iliyopita alipofika Roma. Ilikuwa ni mmoja wa watu wa kujitolea wa Italia. Kwa upande wao anasema wana mambo matatu makubwa ambayo yanajikita katika chama chao na msingi yaani utaratibu kati yao, kujitolea na ushirikiano kati yao ni msingi, tofafuti na kujishughulisha. Katika zoezi hili wao wanawasindikiza kwa namna  maalumu ya ushuhuda wa watu wa kujitolea na ukarimu ambao unaoneshwa kwa wanaume na wanawake ambao wanatoa muda wao ili kuweza kukaa na wagonjwa. Kama Maria alivyobaki chini ya miguu ya Yesu Msalabani, hata wao wako chini ya kitanda cha mateso na watimiliza usindikizwa ambao ambao unaleta faraja kubwa. Ni uwepo wa ukarimu na faraja ambayo ndiyo amri ya upendo usio na mapaka wa kindugu aliofundisha Yesu (Mt 12,31). Tabia hizi za ukaribu ni muhimu mbele ya mgonja na hali ambayo ni ngumu kwa kumtambua mgonjwa na umuhimu wake.

Baba Mtakatifu anatambua ni kwa jinsi gani mgonjwa wa siku nyingi isivyo kuwa  rahisi kwa sababu ya  ugonjwa unazimisha kukaa sehemu moja na majaraibi ya kuhisi umetengena na dunia nzima, kama mahusiano na maisha ya kila siku. Ugonjwa unafanya ujiuliza maswali mengi na wagonjwa wengi wanaishi na uzoefu ambao unapaswa kuwa na uhakika kwa  Bwana ambaye kamwe hawaachi maana naye alijaribiwa na uchungu na yupo nao daima karibu. Uwepo wa watu ambao wanashirikiana na kipindi hiki kigumu ni ishala kubwa sana na kama faraja ya Yesu na mama yake Bikira Maria ambaye ni mama na faraja ya  wagonjwa wote . Baba Mtakatifu amekumbuka watu ambao wanashirikisjana na Kanisa na watuambao wanateseka na magomjwa mbalimbali kama vile Mapadre,m mashemasi na wahudumu wa Ekaristo , kwa ushuhuda wao kiroho na kidugu ndiyo jumuiya nzima ya waamni ambao wanafariki na kuwa jumuiya ya tabibu ambayo inafanya shauku ya fhau ya Yesu kuoneakana kwa maana ili wote wawe wamoja kuanzia walio wadhaifia na waathirika (Yh 17,21).

Nafasi ya madaktari, wauguzi wanasayansi na mafundi wa maabara  daima wana msimamo, si katika nafasi ya taaluma na mafunzo ya kisayansi  lakini pia katika kambi ya kitasaufi  mahali ambamo wanaalikwa kutibu mtu kwa ujumla wake wa roho na mwili. Tiba haipo katika ugonjwa wa kiungo au kiini, lakini ni katika mtu kamili. Mtu katika roho yake ni pamoja na mwili wake; kwa maana roho inatoka juu na kuwa ndani ya mwili kwa kujumuisha maisha na hadhi yake kuu ambayo siyo ya kibailojia bali ya mtu mwenyewe na roho yake. Katika historia ya miaka 50 matokeo ya utafiti na maendeleo ya kisayansi yameendelea na kuwa chachi kwa ajili ya kupyaisha sura ya kutibu na ubora wa maisha ya mtu mgonjwa. Jitihada zao zinaweza kuendeleza kuhamaisha daima kila mtu katika utamaduni wa zawadi na kutibu mwingine, kwa uhai na kuishi  kila jumuiya ya kibinadamu.

 

02 March 2019, 13:44