Tafuta

Baba Mtakatifu amekutana na Wajumbe wa Shirikisho la vyama vya Ushirika nchini Italia Baba Mtakatifu amekutana na Wajumbe wa Shirikisho la vyama vya Ushirika nchini Italia 

Papa:Ushirikiano,mshikamano,ukaribu ni nyenzo za kupambana na upweke duniani!

Papa Francisko amekutana na wajumbe wa Shirikisho la Vyama vya Ushirika nchini Italia katika Ukumbi wa Paulo VI mjini Vatican wakiwa wanaadhimisha miaka 100 tangu kuanzishwa kwake.Katika hotuba yake amesisitiza juu ya mshikamano,ushirikiano,ukaribu kuwa ndizo nyenzo za kupinga sintofahamu na ubinafsi katika dunia ya utandawazi

Na Sr Angela Rwezaula - Vatican

Tarehe 16 Machi 2019 Baba Mtakatifu Francisko amekutana na wajumbe wa Shirikisho la Vyama vya Ushirika nchini Italia katika Ukumbi wa Paulo VI mjini Vatican wakiwa wanaadhimisha miaka 100 tangu kuanzishwa kwa shirikisho hili. Ninawakaribisha wote na kumshukuru Rais wenu kwa maneno yake. Miaka 100 ya historia ya matendo yao ni mtazamo muhimu sana ambao hauwezi kupita tu kwa ukimya. Miaka hiyo inawakilisha mchakato ambao ni wa kutoa shukrani kubwa kwa kile ambacho wameweza kutenda kwa njia ya kuongozwa na wito wa Hati ya  Rerum novarum ya Papa Leone XIII.  Baba Mtakatifu huyo kwa mtindo wa kinabii alifungua tafakari kubwa juu ya mafundisho ya kijamii ya Kanisa Katoliki. Kuanzishwa kwake kulitokana na kuchanua kwa makini kwamba Injili haiwezi kufungwa tu kwa upande wa mtu au jamii, lakini inazungumzia mtu kamili ili kumfanya awe daima binadamu.  Wakati Papa Leone XIII anandika ilikuwa ni kipindi kigumu lakini kila nyakati Baba Mtakatifu anathibitisha, zina magumu na matatizo yake.

Historia yao ina thamani kubwa kwa jitihada za karne

Akisisitiza zaidi anasema historia yao ni yenye thamani na ambayo inazaliwa na maneno ya Papa na kutambua kufanya mambo ya dhati na kwa ukarimu na jitahada za kudumu sasa kwa karne. Hata leo hii Kanisa linahitaji kusema kwa sauti kubwa Ukweli. Kanisa limekuwa daima na mahitaji ya wanawake na wanaume ambao wanatambua kubadili mali ya dhati, kwa kile ambacho wachungaji wana hubiri na watalimungu wanafundisha. Kwa maana hiyo tendo la leo hii kusema asante kwa miaka 100 ya jitihad ni kama kuwaonesha kufanya  mfano kwa watu wa nyakati zetu ambao wanahitaji kujigundua, si kama  wachukuaji wa mali tu, lakini kama wajasiriamali wa upendo. Mfano wao wa ushirika kwa dhati umeongozwa na mafundisho jamii ya Kanisa Katoliki kwani hurekebisha tabia fulani ya kawaida ya jumuiya na takwimu, ambazo huwa hatari kwa mipango binafsi; na wakati huo huo, huzuia majaribu ya upendeleo binafsi na mfano wa kujikomboa binafsi. Kwa hakika wakati biashara ya kibepari anasema Baba Mtakatifu kuwa, inalenga hasa faida, kinyume ni kwamba faida ya ushirika lengo lake kuu la kuridhika na uwiano wa mahitaji ya kijamii kwa ujumla. Hata hivyo anabainisha kuwa, kwa hakika vyama vya ushirika pia vinatakiwa kuzalisha faida, kuwa na ufanisi na katika shughuli zake za kiuchumi, lakini yote haya yanafanyika bila kupoteza mtazamo wa mshikamano wa ushirikiano! 

Ushirika wa kijamii ni moja ya sekta mpya za ushirikiano na ambazo zinahitajika

Kwa sababu hiyo Baba Mtakatifu anasema mfano wa ushirika wa kijamii ni moja ya sekta mpya ambazo ushirikiano wa sasa umejikita katika ushirika, kwa sababu  unaweza  kuchanganyikana,kwa upande mmoja, mantiki ya kampuni na, kwa upande mwingine, wa mshikamano, ikiwa na maana ya  mshikamano  wa ndani kuelekea wanachama wake na mshikamano  wa nje kuelekea kwa walengwa. Njia hii ya kuishi mfano wa vyama vya ushirika vinafanya zoezi tayari na kuwa na ushawishi mkubwa kwa makampuni ambayo mara nyingi yamefungwa na mantiki ya faida, kwa sababu inawasukuma kugundua na kutathmini athari za wajibu wa kijamii. Kwa maana hiyo Baba Mtakatifu Francisko anawaalika na kuwashauri wasisahua mtazamo wa ushirika, ambao unasimamia juu ya uhusiano na siyo faida, yaani kwenda kinyume na mantiki ya dunia. Ni kwa njia ya kugundua kuwa utajiri wa kweli ni uhusiano na si mali ya vitu, na kwamba ndipo tunaweza kweli kupata mbadala wa kushi na kukaa katika jamii ambayo haitawaliwi na miungu fedha, miungu ambayo inakatisha tamaa na kuacha matokeo mabaya yasiyo ya kibinadamu.

Shukrani kwa kazi ngumu ya mshikamano na ushirikiano wa kibinadamu

Baba Mtakatifu Anawashukuru kwa kazi yao ngumu ambayo inaamini mshikamano na kujielezea ubinadamu katika dunia hii ambayo inataka kufanya biashara kwa kila kitu. Hata hivyo faida kuu muhimu inayoonekana ya mshikamano, anasema ni kushinda ule upweke na kuubadili katika maisha kutoka katika moto wa jehenamu. Iwapo mtu anahisi upekwe anahisi kweli jehenamu. Na kinyume chake iwapo anahisi kuwa siyo peke yake hapo anao uwezo wa kukabiliana na kila aina ya matatizo na ugumu. Dunia yetu imeugua upweke, anabainisha Baba Mtakatifu Francisko na hivyo kuna haja ya kuanzisha mshikamano huo ambao unawezesha kukabiliana pamoja na wengine, kile ambacho maisha yanapendekeza kwa wakati huo. Kutembea pamoja na kufanya kazi pamoja ni kufanya uzoefu wa muujiza mkubwa wa matumaini. kwa kufanya hivyo kila kitu kinaonekana kipya na  kinacho wezekana na hivyo  Baba Mtakatifu anasisitiza kuwa, ushirikiano ndiyo suala la dhati la kuleta matumaini katika maisha ya mtu.

Kila mmoja ajaribu kuondoa kipande cha upekwe kwa mwingine

Hata hivyo Baba Mtakatifu Francisko aliendelea na hotuba yake anabainisha kuwa ushirikiano kwa namna nyingine ya kusema ni ukaribu ambao Yesu alifundisha katika Injili. Kuwa karibu maana yake ni kuzuia mwingine asiwe mateka wa jehanamu la upweke. Kwa bahati mbaya anasisitiza, taarifa nyingi za habari zinaelezea watu wanaojiua wenyewe kwa sababu ya mahanagiko na mara nyingi yanatokana na  upweke. Hatuwezi kubaki na sintofahamu mbele ya majanga haya, na kila mmoja kwa kadiri ya uwezo wake, ajitahidi kuondoa kipande cha upweke kwa wengine. Na ili kuweza kufanya hivyo si kwa njia ya maneno tu, bali zaidi ni jitihada za upendo wa dhati , ujuzi na kujiweka katika mchezo  wa ile  thamani kubwa ambayo ni uwepo wetu binafsi kwa anayehitaji. Ni kwa njia ya kuwa mstari wa mbele tunaweza kufanya utofauti anathibitisha Baba Mtakatifu Fancisko. Akiendelea na hotuba yake anatoa  mfano kuwa  ni mshkiamano wa jitihada za kutoa ajira yenye usawa kwa wote; kuwezesha wakulima ambao ni wadhaifu zaidi kupata soko na kushiriki katika jumuiya inayo watia moyo na kwasaidia; wavuvi walio peke yao kuwa na ushiriki katika makundi makubwa; wachukuzi wa mizigo kuwa ndani ya kikundi na mengineo zaidi. Huo ndiyo mtindo wa kushirikishana na ambao unageuka kuwa wa maisha, anatubitisha Baba Mtakatifu.

Injili ya Makatifu Marko kuhusu Yesu kumponya kiwete

Kulingana na tukio la Injili ya Mtakatifu Marko ambaye ni msaada, Yesu alipoingia kwa upya katika mji wa Kafarnaumu baada ya siku. Watu wengi walikuwandani ya nyumba na watu wengi wamejaa kiasi kwamba hapakuwapo na  nafasi hata mbele ya mlango na Yeye alikuwa akihubiria Neno. Ndipo watu wanne walimleta kiwete na kumshusha kupitia paa la nyumba. Yesu alimponya na kumwambia asimame na kubeba kitanda chake na dhambi zake zote zimesamehewa kutokana na imani (Mk 2,1-5). Tukifikiria sura hii ya Injili, kwa haraka ni kuona muujiza mkubwa juu ya msamaha na baadaye kupona kwa  mwili wa mtu huyo, lakini labda, baba Mtakatifu Francisko anabinisha kuwa, muujiza mwingine wa pili unapotea machoni petu kwani upo ule wa marafiki zake. Watu wanne waliokuwa wamembeba mabegani; wao hawakubaki na sintofahamu mbele ya mateso ya rafiki mgonjwa; hata kuona aibu mbele ya watu wengi waliokuwa wanamsikiliza Yesu. Watu hawa walitimiza ishara kubwa ya muujiza. Kwa pamoja walitengeneza mkakati wa ushindi na ubunifu , wakapata suluhisho  kubwa kuhusu mtu huyo, lakini pia hata kumsaidia akutane na na Yule  ambaye anaweza kumbadili Maisha yake. Na kutokana na ugumu wa kupitia njia rahisi, walipata ujasiri wa kupanda juu ya paa na kulifungua.  Hawa Baba Mtakatifu anakiri kuwa, ndiyo wanamfungulia njia kiwete kumkaribia Yesu na kuweza kubadili kutokana na mkutano huo. Mwinjili anaonesha kuwa Yesu anamwambia mtu huyo:“imani yako imekuokoa, ikiwa na maana imani ya kikundi kizima imewaokoa!

Muujiza wa ushirikiano ni mkakati wa kikundi ambacho kinafungua mlango kwenye ukuta wa sintofahamu

Baba Mtakatifu Francisko anasisitiza, zaid juu ya watu ha ona muujiza huo kuwa tunaweza kusema kuwa ushirikiano ndiyo  njia moja ya kufungua paa la uchumi ambao huko hatari ya kuzalisha mali, lakini kwa gharama ya ukosefu wa usawa kijamii. Ni kupambana na utofauti na ubinafsi ili kuweza kufanya jambo jingine tofauti na siyo tu kulalamika. Anayeanzisha chama anaamini kwa namna nyingine kuzalisha, ya kufanya kazi, ya kukaa katika jamii. Anayeunda chama anao ubunifu kidogo na ujasiri kama ule wa watu wanne marafiki wa kiwete. Na kwa maana hiyo ni kuonesha kuwa  muujiza wa ushirikiano ni mkakati wa kikundi ambacho kinafungua mlango katika ukuta wa sintofahamu inayobagua aliye mdhaifu. Chama kinachogeuka kuwa ukuta, kilichotengenezwa na wimbi la watu wengi wasiofikiria, wala kutenda kama watu, hawana uwezo wa kusifu thamani msingi ya mahusiano. Hawawezi kweli kukutana kama mtu iwapo ni mgonjwa wa sintofahamu na ubinafsi. Kwa maana hiyo hali halisi ya kweli ya kiwete ni umati. Umati ambao umeundwa na watu ambao wanatazama tu mahitaji yao binafsi bila kutambua ya wengine, kwa maana nyingine hao hawawezi kugundua kamwe utimilifu wa hali halisi ya maisha. Ubinafsi unazuia furaha kamili, kwa sababu unabagua upeo wa mwingine!

Ninapobaki kipofu mbele ya mateso na ugumu wa wengine, kwa hakika ni kubaki kipofu mbele yakile chenye furaha

Ninapobaki kipofu mbele ya mateso na ugumu wa wengine, kwa hakika ninabaki kipofu mbele ya kile ambacho kingenifanya niwe na furaha. Hawezekani kufurahia peke yetu binafsi. Yesu katika Injili anasema sentensi moja kwa haraka “yamfaa nini mtu kuupata ulimwengu wote, kama akijiangamiza, au kujipoteza mwenyewe? (Lk 9,25). Baba Mtakatifu anasisitiza tena:Tunaishi katika dunia ambayo inahangaikia namna ya kuwa navyo na ambamo inakuwa na ugumu wa kutambea kama jumuiya moja. Kazi ambayo wao wanapeleka mbele kwa miaka 100 ni ile ya kupingana na uhusiano wa ubinafsi, au kikundi cha kutafuta faida ya ustawi wa wote kwa manufaa ya wachache tu.

Uzoefu wa Baba Mtakatifu alipokuwa na miaka 18

Baba Mtakatifu Francisko  amerudia kusimilia uzoefu wake akiwa na miaka 18 kunako mwaka 1954 wakati anasikiliza Baba yake kuhusiana na tema hii. Na tangu wakati ule anaamini kwamba ushirikiano wa kikristo ni njia ya haki kweli. Labda kwa upande wa kiuchumi inawezakana kuwa ya taratibu lakini ni muhimu na yenye usalama. Kwa maana hiyo anathibitisha alivyopenda hotuba ya Rais wa chama hicho anayewakilisha kwa unyenyekevu mkubwa jitihadza za chama hicho ambacho kimeenea katika nchi na duniani. Kwa namna ya pekee anapendezwa kusik a kuwa wamekweda katika sehemu za pembezoni zenye waathirika wengi. Na ndiyo sehemu mwafaka katika ushuhuda. Kusisitizia juu ya aina hii ya pembezoni  ndiyo uchaguzi ambao alifanya hata Yesu Mwana wa Mungu, kuja kwake duniani. Yeye alichagua pembezoni kama kituo cha utume wake. Yeye hakufanya hivyo kijiografia tu,kuja dunia katika pembezoni mwa utawala wa kirumi, lakini alifanya hivyo kwa kutaka kukutana na kila mtu aliyeachwa pembezoni kwa sababu ya umaskini, magonjwa na au makosa yake binafsi.

Dunia ya sasa iliyojaa utandawazi, tunapaswa kuwa na maelewano yanayoelezwa katika Mafundisho jamii ya Kanisa Katoliki

Katika dunia ambayo imejaa utandawazi kama ilivyo sasa, Baba Mtakatifu anasema, tunapaswa kuwa na maelewano ambayo yanaelezwa katika mafundisho ya Kanisa Katoliki,  mahali ambapo panazungumzia kiini cha mtu. Na Mtakatifu Yohane Pauli II alielezea vizuri katika Hati ya Centesimus annus. Anaandika hivi “Ikiwa mara moja jambo lililokuwa la msingi ni nchi na baadaye mji mkuu, kwa maana ya  wingi wa mitambo na mali  yenye vifaa, leo hii jambo muhimu zaidi ni mtu mwenyewe na  kwa maana [...] uwezo wake wa kuandaa mshikamano, uwezo wake wa kutambua  na kukidhi mahitaji ya wengine” (n. 32). Kwa hiyo Baba Mtakatifu anabainsha kuwa  tunapaswa kuelewa umuhimu wa kupata ujuzi wa kitaaluma na kutoa kozi za mafunzo ya  kudumu, hasa kwa watu hao wanaoishi katika  pembezoni mwa jamii na makundi ambayo hayana fursa zaidi.

Tema ya wanawake inatakiwa irudi kupewa kipaumbele cha maisha endelevu

Baba Mtakatifuu aidha kwa mtazamo huo wa kiini cha mtu  hasa ni wanawake ambao duniani kote wanabeba uzito wa umasikini wa zana, ubaguzi kijamii, na ubaguzi wa utamaduni. Tema ya wanawake inatakiwa irudi kuwa kiini cha  mipango ya kwanza ya maisha endelevu kwa mantiki ya chama. Siyo mazungumzo ya kiitikadi. Badala yake, ni suala la kutiliwa maanani juu ya mawazo ya wanawake kama mtazamo wa hali ya juu wa kujifunza kufanya ushirikiano, si tu kimkakati lakini pia kibinadamu. Mwanamke anaona vizuri nini maana ya upendo kwa uso wa kila mtu. Mwanamke anajua vema jinsi ya kuthibitisha kile ambacho wanaume wakati mwingine tunawatendea kama “mifumo ya juu”. Kwa kuhitimisha, Baba Mtakatifu Francisko hotuba yake anawatakia matashi mema ya maadhimishao ya miaka 100 iliyopita ili wafungue mbele yao jitahada kubwa na mpya  ambayo haijawahi na  kubaki  waaminifu katika mzizi ambayo wamezaliwa kwa maana ya Injili! Wasipoteze mtazamo wa chem chemu hiyo ili kuweza kuendeleza ishara na katika uchaguzi wa Yesu kila ambacho kinaweza kuwasaidia katika kazi yao. Anawabariki na kwa moyo wote anawatia moyo kuonesha matumaini yake kwao, kwa kile ambacho wanatenda kwa dhati. Ni uhakika kuwa ndiyo matumaini mazuri na ndiyo jibu. Na wasiwasahu kusali kwa ajili yake!

16 March 2019, 14:15