Vatican News
Ajali mbaya ya ndege nchini Ethiopia iliyoteka tarehe 10 Machi 2019. Baba Mtakatifu ametuma salam za rambi rambi Ajali mbaya ya ndege nchini Ethiopia iliyoteka tarehe 10 Machi 2019. Baba Mtakatifu ametuma salam za rambi rambi 

Papa:Salam za rambi rambi kwa wanafamilia wa waathirika wa ajali ya ndege

Baba Mkatifu Francisko ametuma salam za rambi rambi kufuatia na ajali ya ndege nchini Ethiopia aina ya Boeing 737 siku ya Jumapili tarehe 10 Machi 2019 asubuhi majira ya saa 2:48 kwa saa za Afrika Mashariki

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Telegram ya Baba Mtakatifu Francisko iliyotiwa sahini na Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican, kufuatia na ajali ya ndegu nchini Ethiopia.Katika telegram  hiyo Baba Mtakatifu Francisko anaonesha masikitiko yake makubwa kufiatia na ajali ya ndege ambapo anasali kwa ajili ya waathirika wote kutoka mataifa mbalimbali na anawakabidhi roho za marehemu katika huruma ya Mungu Baba. Aidha anawatumia salam za rambi rambi wana familia na  wale wote ambao wanaomboleza kufuatia na kupoteza wapendwa anaombea baraka na faraja kwa Mungu kwa ajili yao.

Ajali ya ndege  Ethiopia aina ya Boeing 737: Ndege ya shirika la ndege la Ethiopia imeanguka siku ya Jumapili asubuhi majira ya saa mbili na dakika arobaini na nne kwa saa za Afrika Mashariki tarehe 10 Machi 2019 ikiwa na abiria 149 pamoja na wafanyakazi 8. Msemaji wa shirika hilo ambaye athibitisha juu ya taarifa hiyo ambapo imetajwa ndege hiyo ilikuwa ikielekea mjini Nairobi nchini Kenya.  Na Waziri mkuu wa Ethiopia aliandika katika ukurasa wake wa Twitta  Jumapili, tarehe 10 Machi 2019 ujumbe wa kutoa pole kwa familia za waliofiwa kufuatia ajali hiyo mbaya katika ndege la Ethiopia aina ya Boeing 737.

Ndege hiyo ilitarajiwa kuwasili mjini Naorobi kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo kanyatta saa nne unusu kwa saa za Afrika Mashariki. Taarifa ya Kampuni ya ndege ya Ethiopian ilisema abiria kutoka nchi 33 waliosafiri kwenye ndege iliyopata ajali wote walikufa, kulingana na Msemaji wa Kampuni hiyo Asrat Begashaw. Taarifa ya Shirika la ndege la Ethiopia ilisema walipoteza mawasiliano na ndege iliyopata ajali dakika sita baada ya kuondoka kwenye uwanja wa ndege wa Adis Ababa.

Takriban wasafiri 149 na wahudumu wanane waliokuwemo ndani ya ndege hiyo hakuna hata mmoja aliyeweza kunusurika na wote wamekufa. Mkurugenzi mtendaji wa Ethiopian CEO, Tewolde Gebremariam ameuambia mkutano wa waandishi wa habari kwamba miongoni mwa waliokuwemo kwenye ndege hiyo ni pamoja na: Wakenya 32 , raia wa Canada 18, raia tisa wa Ethiopia, wataliano 8, Wachina 4,wamarekani 8, waingereza 7  , Wafaransa 7 , Wamisri 6, Wajerumani 5 , Wahindi 5 na 4 kutoka Slovakia. Waastralia 3, Waswis 3, Warusi 3, Wakomoro 2, Wahispania 2, Wapoland 2, Waisraeli 2. Kulikuwa pia abiria mmoja mmoja kutoka nchi za ubelgiji, Indonesia, Somalia, Norway, Serbia, togo, Msumbiji, rwanda, Sudan, Uganda na Yemen. Afisa wa itifaki wa Somalia ameripotiwa kuwa mmoja wa watu waliokufa kwenye ajali hiyo, kulingana na kituo cha kibinafsi cha Radio Dalsan, kinachomilikiwa na redio ya Somalia.

11 March 2019, 15:59